Nahitaji msaada wa wazo la biashara

Nahitaji msaada wa wazo la biashara

mafioso

Member
Joined
Jan 17, 2008
Posts
34
Reaction score
28
Wadau, salama?

Nakuja mbele zenu leo kuomba msaada wa mawazo juu ya mambo ya biashara. Mm sina uzoefu wa biashara, nimesomea IT, nimeajiriwa mwaka wa tano sasa, lakini nimekuja kugundua kipato changu kiko hali mbaya sababu ya mshahara finyu wa ajira, pesa nayopata ni ya kula na kodi tu ya nyumba, kdg na ada za watoto. Nina familia na nimeshtuka kuwa nisipofanya maarifa mapema maisha yatakuwa magumu huko mbeleni. Umri wangu ni miaka ipatayo thalatha.

Nina kila imani kuwa sasa ni wakati muafaka kutafuta kipato zaidi nje ya ajira yangu, ikibidi nikiweza kuestablish kitu changu basi niache ajira na nikisimamie kikamilifu ili kifanikiwe. Ninaishi Dar, nina budget ya 30M ambazo niko tayari kuziingiza kwenye shughuli nitakayoweza kuidentify ambayo niko tayari kuisimamia kwa nguvu zote.

Huko nyuma nimeshajaribu ufugaji wa kuku wa kizungu haukuwa na mafanikio sana pamoja na kusimamia kwa karibu sana, nikahamia kuku wa kienyeji ambao nafuga mpk sasa lkn kama mnavyojua, wale ukuaji wao ni wa muda mrefu sana, so sijaanza kufanya biashara. Nimeshajaribu kilimo, matunda, mahindi, viazi, maharagwe, lkn haikuwa na matokeo mazuri, nilipata hasara lkn sijakata tamaa katika kuhangaika.

Leo nakuja mbele yenu kuomba mchango wa mawazo maana naona nimestuck, ningependa kupata wazo la biashara, au shughuli ninayoweza kuifanya ikanizalishia kipato cha ziada. Kama nilivyosema, mm si mbobezi/mzoefu sana wa biashara lkn niko tayari kujifunza na kupambana na changamoto nitakazo kutana nazo.

Ni imani yangu nitapata michango chanya toka kwenu wadau, najua waosha vinywa hawatakosekana kwenye uzi huu lkn ndiyo changamoto zenyewe hizo kwenye mkusanyiko wa watu wengi.

Nawasilisha.
 
Elimu yako level gani na una experience muda gani?
 
Mkuu tafuta eneo nje ya mji fungua executive pub inalipa....na bia za jumla....unaweza fungua pia kampuni ya IT and Telecomms
 
Kaka tafuta wholesale wa madawa ya kulevya inalipa sana tena kwa muda mfupi
 
ni vizuri kuwekeza kwenye kitu unachokijua... mi nakushauri chekecha mawazo kwenye it sekta hiyo hiyo..

muhimu ujue kuwin market tu.. maana napo ku create sales nayo ni skills ya hali ya juu
 
nakushauri fungua duka la wine za south. tafuta seheme nzuri. wine huko jumla ni kuanzia rand 30. kwa exchange rate ya 150 inakuja Tsh 4500. anza labda chupa 3,000. cha muhimu uweke mtu mwenye customer care nzuri na anayezielewa wine. pia kumbuka kuna kodi kubwa na shipping cost.
attachment.php
 

Attachments

  • wine-shop-2-1024x768.jpg
    wine-shop-2-1024x768.jpg
    83.8 KB · Views: 462
nakushauri fungua duka la wine za south. tafuta seheme nzuri. wine huko jumla ni kuanzia rand 30. kwa exchange rate ya 150 inakuja Tsh 4500. anza labda chupa 3,000. cha muhimu uweke mtu mwenye customer care nzuri na anayezielewa wine. pia kumbuka kuna kodi kubwa na shipping cost.
attachment.php

Ningependa kujua zaid kuhusu hii kitu.
 
Back
Top Bottom