Misterdennis,
Nami nimeigoogle hiyo dll file inayo pop kila mara kwenye pc yako.
Sehemu nyingi haijatatuliwa ipasavyo. Hiyo link aliyotoa shy inaonesha aina ya solution mbalimbali ya kutatua matatizo kama haya. Na mwisho wake wanasema, tu kuwa system kama iko compromised ni bora tu kuformat na kuinstall upya Windows yako.
Fanya backup ya ma file na unayohitaji/ documents na vinginevyo, kisha fanya hiyo format na re-installation. Najua kuna alternatives nyingi, lakini hilo jidubwasha ulilolikwaa 'xlibgfl254.dll' utatuzi wake kwa kutumia njia za antivirus na malware removers nyingine zitakupelekesha mbali kama hauko ndani sana na mambo ya ku-debug computer kupitia system registry n.k.
Kuna pahali pengi wameongelea COMBOFIX kama tool ya kuondoa hiyo compromise, lakini kama ujuavyo, tools nyingine ni kasheshe kutumia, na sehemu nyingi zitakuacha ukiwa umevuruga system yako bila hata mafanikio.
Kumiss kwa dll file inafanyika makusudi na hacking tools, ili waweze kuwa wanakutumia virus na madudu mengine. Na saa nyingine inatokea kama accident kutokana na software unayo iamini kuondoa dll file fulani kwa ajili ya kuruhusu communication baina ya kampuni inayotengeneza hiyo software na wewe.
Kama utakuwa mwingi wa kutatua mambo kama haya; kuna thread fulani hivi inaelezea mengi ambayo mtu unaweza kufanya ili kuondoa virus manually.
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=5078
Pole na tatizo lililokupata, hope utalitatua si muda mrefu.
SteveD.