Straight corner
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 385
- 132
hongera sana mkuu...unataka kuuzia shambani au sokoni..mi nakushauri ongea na madalali waliopo soko jirani ujue bei yao then km vp unaweka kwenye magunia unasafirisha kwenda huko........ukiuzia shambani watakupunja sana.....jaribu kupata connection za hivyo...mi pia ni mkulima
Kila la heri mkuu ila soko utapata tuu......kitunguu bado ni hotAsante kwa ushauri mkuu. Napenda sana niuzie sokoni ila akipatikana mnunuzi kwa bei nitakayoridhika nayo nitauza.
Wanabodi habari!
Nimelima shamba la vitunguu yapata ukubwa wa ekari 1 na sasa vimefikia hatua ya kuweza kuvunwa. Kwa makadirio natarajia kuvuna kama gunia 70. Kwangu naona si haba na nimeamini shamba halimtupi mkulima.
Wakuu naombeni mnisaidie kupata soko kwa zao hili, shamba langu liko Simanjiro jirani kabisa na geti la TPC (darajani), wenyeji wa Moshi wanaweza kufahamu eneo hili.
Naomba yeyote mwenye nia ya kununua, kutoa maoni au ushauri atumie namba hii 0782336657 ili na mimi nifaidi haya matunda ya kilimo.
Hizi ni baadhi tu ya picha halisi ya zao hili katika shamba langu.
View attachment 89643
Mkuu asante kwa mchango wako. Kwa kifupi binafsi ni mara ya kwanza kulima zao hili ila nilikuwa na kijana mzoefu aliyenipa mwongozo.Jitahidi uuze kwa bei unayoona kuna maslahi kwako. Kusema kweli ninakuona wewe kama shujaa kwa kuweza kuvuna majira haya ambayo ni msimu mgumu kabisa kustawisha vitunguu. Msimu huu ndiyo wenye bei ya juu kulika kawaida. Kama hufahamu msimu huu ndiyo huwa unabei kubwa kuliko yote! Tafadhari nakushauri peleleza bei zinazotembea masoko mbali mbali nje na ndani ya mkoa hata ikibidi masoko ya Kenya! Gunia 70 ni mzigo mkubwa huo kuweza kusafirishwa hadi Dar! Ukiwa na mzigo mkubwa na wenye soko hauhitaji kuwa na nauli ya kusafirishia, wasafirishaji watapeleka tu hadi sokoni.
Swali langu tu Mkuu hiyo ni mbegu aina gani, ulinunua kwa bei gani? Hebu na wewe naomba utupe picha ya gharama za kulima zao hilo hapo Moshi. Kama utaona soo kuanika hapa basi PM.
Usipate tabu ndugu yangu ,ngoja nicheki bei hapa zenji watu wavifuate au uvilete huku zenji -kwa taarifa vitu kama vitunguu ,tungule ,carrot ,cabage ,ndimu etc ni hot deal hapa! notakutwangia mwenyewe utaamua!Wanabodi habari!
Nimelima shamba la vitunguu yapata ukubwa wa ekari 1 na sasa vimefikia hatua ya kuweza kuvunwa. Kwa makadirio natarajia kuvuna kama gunia 70. Kwangu naona si haba na nimeamini shamba halimtupi mkulima.
Wakuu naombeni mnisaidie kupata soko kwa zao hili, shamba langu liko Simanjiro jirani kabisa na geti la TPC (darajani), wenyeji wa Moshi wanaweza kufahamu eneo hili.
Naomba yeyote mwenye nia ya kununua, kutoa maoni au ushauri atumie namba hii 0782336657 ili na mimi nifaidi haya matunda ya kilimo.
Hizi ni baadhi tu ya picha halisi ya zao hili katika shamba langu.
View attachment 89643
Mkuu asante kwa mchango wako. Kwa kifupi binafsi ni mara ya kwanza kulima zao hili ila nilikuwa na kijana mzoefu aliyenipa mwongozo.
Kwa ekari 1 nilinunua mbegu Kg 6 (Red Bombay), kuandaa vitalu na kuhudumia kama sh laki 3, kuandaa shamba (kulima na kuweka borders/vitalu) kama sh laki 2.5, kupanda kama laki 2, mbolea ya kupandia na kukuzia (UREA & CAN) kg 50 @.
Baada ya hapo kuna swala la kumwagilia kila wiki *2 sambamba kupiga dawa ya kuua wadudu. Baada ya kama siku 45 niliweka mbolea ya kukuzia tena kg 50. Zoezi la kumwagilia na kupiga dawa linategemea mara nyingi na hali ya hewa (Mvua/ukungu).
La msingi ni hawa watu wanaoitwa wasimamizi wa shamba, anaweza kukuingiza mkenge kwa kumpa dawa na asiipige, au kama si mzoefu anaweza kushindwa kutambua dalili za wadudu waharibifu mapema hadi athari zinajitokeza.
Kwa kifupi ndivyo hivi, wataalam ni wengi humu JF wanaweza pia kuchangia ili kuboresha ulimaji wa zao hili.