Nahitaji kupumzika

charrote

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2017
Posts
1,988
Reaction score
4,413
Habari ya uzima
Niende moja kwa moja kwenye mada, nina miezi minne sasa tangu nilipokorofishana na mpenzi wangu na hivi Wiki iliyopita ameamua kuondoka. Sababu hasa ni hii

Ilikuwa asubuhi moja ya mwezi wa tano nilipoamka na kuanza harakati za kujiandaa kwenda kazini(kampuni binafsi). Muda huo mpenzi wangu huyo alikuwa bado kalala na mimi huwa Natangulia kutoka kila siku, yeye hana sababu ya kuwahi kwani anafanya shughuli binafsi.

Baada ya kumaliza kujiandaa nikamuaga nikashika njia kuelekea kazini. Nikiwa njiani nikapokea ujumbe wa simu kutoka kwa mwanaume fulani ambaye niliwahi kufanya nae kazi mahala fulani, alikuwa akiniuliza iwapo nimefika kazini nikamjibu hapana.

Aliendelea kutuma ujumbe lakini sikuweza kuusoma kwasababu nilikuwa natembea. Baada ya kufika kazini nikasoma jumbe zote zilizotumwa na bwana yule kilichonishangaza ni kuwa jumbe hizo zilikuwa za mapenzi ilhali mimi na Yule bwana hatuna mahusiano yoyote.

Nilipochunguza "sent items" yangu nikakuta ujumbe wa mapenzi uliotumiwa kwa yule bwana, hapo nikaamua kumuuliza Yule bwana akasema mimi ndiyo nimemtumia ujumbe asubuhi. Hili jambo liliniudhi na ni dhahiri kuwa mpenzi wangu ndiye aliyetuma ujumbe wa mapenzi kwa huyu jamaa na hapo ikawa mimi ndiye nimemtongoza huyu jamaa.

Nikaamua kumpigia simu mpenzi wangu lakini akanipokea kwa matusi ambayo hayaandikiki, nikakata simu hata hivyo akaendelea kunitumia jumbe za matusi kuhusu mpaka kufikia hatua ya kuniambia ananichukia .

Tangu hapo maelewano kati yetu yakatoweka ,ingawa tunaishi chumba kimoja ila kila mtu akawa anaishi maisha yake. Hali hii sikuipenda japo nilifikiri mambo yataisha ila kadri siku zinavyosonga hali inazidi kua mbaya.
Tukiachana na swala la chakula ambalo kila mtu anajitegemea, lakini hata malipo ya umeme na maji imekuwa juu yangu,, hiyo haina shida..

Mwezi huu nilipanga niondoke nirudi kwetu hivyo nikaandika barua ya kuacha kazi ofisini,, baada ya kuchukua maslahi yangu nikasafiri kwenda mkoa wa jirani kufatilia vyeti vyangu ambapo nililala siku moja na siku iliyofuata nikarejea.

Nilipoingia ndani niliona mabadiliko, nguo zangu zilikua zimemwagwa kitandani begi langu halipo. Begi hilo lilikuwa na pesa zangu robo tatu ya mshahara wangu pamoja na simu yangu ndogo,, havikuwepo..

Nimejaribu kumtafuta kwenye simu hapatikani, nilipowasiliana na ndugu yake akaniambia jamaa yuko nyumbani kwao yaani mkoani... Sikuwa nimetegemea kwasababu kwanza nilimuamin sana ila acha nipumzike........
 
Samahani mkuu,
Ulitaka tukushauri, ulikuwa unatuambia au vipi,
Fafanua kidogo ulikusudia kitu gani kwetu?
Alafu jinsia yako ni ipi mbona stori imekuwa kama wote wa kiume?

Kando ya yote pole kwa maswahibu
 
Pumzika tu mkuu. Pole sana

[emoji252]You get what you work for not What you wish for [emoji252]
 
Mapenzi hayana likizo.
Whether mkae pamoja kila mtu ajishushe myajenge au kila mtu aendelee kujifanya yupo juu muachane.

Zama hizi maisha yamekuwa na frustration nyingi saana inshu ndogo tuu watu wanakuwa wakali kama pilipili usipokuwa makini dah mtaishia kuachana
 
Hata sijaelewa vizuri ni nini kinahitaji.

Atakaye elewa anijuze tafadhali.
 
Kaka yangu

Kwa swala la jamaa kuchukua simu na kuanza kutuma msg za kimapenzi kwa mwanaume kumtongoza ionekane ni yeye katongoza hata me hilo halivumiliki ni wazi alitaftiwa tu kisa

Yanayo likizo, unajipa break kidogo upate relief ya moyo kabla hujagukia kwenye mapenzi mengine.

Madame S
 
Mnaishi chumba kimoja mara kila mtu anaishi kivyake mnaishije nyie?

Wapenzi mnaishi chumba kimoja na chakula mnajitegemea? SMH!

Mnaishi kila mtu kivyake ina mana ana funguo ya chumba chako aliwezaje kuingia kwako?



Madame S
 
jaman kuna watu mnapitia kwenye mahusiano magumu?? hapo tu hujaoana nae analeta mapicha picha! aisee....kweli tumeumbwa tofauti.....tena tofauti mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…