Nahitaji kuongeza uzito

Sukari Yenu

JF-Expert Member
Dec 8, 2014
1,698
1,253
Wadau mimi nahitaji kuongezeka uzito, ila uzito wa afya usio na madhara. Nifanyeje?
Kuna jamaa wa forever living wanazo dawa za kuongeza uzito, kuna mtu anaexperience nazo?
Nipeni ushauri wadau
 
kwani una kilo ngapi? urefu wako pia umri na jinsia......na kipi kinakupelekea kulazimika kuongeza uzito? tatizo nini?
 
Wengine wanahahakupunguza uzito, wewe unatakakuongeza! Kama umri wako ni mdogo usihangaike maana itafikia umri ambao uzito utaongezeka haraka kiasi kwamba utajihisi vibaya na kutamani ku maintain uzito wako. Maranyingi kuanzia miaka 25-35
 
We kijana acha kuhangaika. Kwani wewe blood group yako ni ipi, maana nasikia watu wa blood group fulani huwa ni wembamba hata wale chakula gani. Otherwise namuunga mkono JMF
 
We kijana acha kuhangaika. Kwani wewe blood group yako ni ipi, maana nasikia watu wa blood group fulani huwa ni wembamba hata wale chakula gani. Otherwise namuunga mkono JMF

Blood group gani mkuu?
 
habari wakuuu bmi yangu ni 18.6 aprxmate under weight sasa nahitaji kuongeza kidogo atlast zifike 60 maana now na kama 53 msaada wakuu nmechoka na uwa nakimwili kidogo
 
Duh....pole mkuu. Mi nna kilo 70 nafukuzia zifike 75 nianze kujiskia na mm mtu
 
habari wakuuu bmi yangu ni 18.6 aprxmate under weight sasa nahitaji kuongeza kidogo atlast zifike 60 maana now na kama 53 msaada wakuu nmechoka na uwa nakimwili kidogo

Pole Ndugu. Kwa BMI hiyo ni kweli uko under weight. Mi nikushauri tu ule vyakula vingi vya wanga. Pia upendelee kula tu hata kamahusikii njaa. Yaani usisubirie mpaka usikie njaa ndio ule.
 
Wadau mimi nahitaji kuongezeka uzito, ila uzito wa afya usio na madhara. Nifanyeje?
Kuna jamaa wa forever living wanazo dawa za kuongeza uzito, kuna mtu anaexperience nazo?
Nipeni ushauri wadau

6faa00a9112d20fc0d4b59db0e081cad3544ecc8.jpeg


Kuna wakati maishani unaweza ukawa unafikiria kuongezeka uzito, na hii ni hali ya kawaida. Mimi binafsi nimeshapita katika hali hii. Vilevile, nimeona watu waliokuwa wanatamani kuongezeka uzito, japo kidogo ili kuweza kufikia kilo wanazohitaji. Wakati mwengine hili zoezi huwa gumu kutokana na kutoelewa mbinu muhimu za kufanya vitu kwa usahihi.

Sasa, katika dunia yetu hii ya leo ambapo kila mtu anataka kupungua uzito na kuwa mwembamba, unaweza kukosa sehemu ya kujifunza mbinu bora za kuongezeka uzito. Katika makala hii tunaangalia njia muhimu 7 unazoweza kutumia katika kuongezeka uzito.
Kunenepa ni kitu kizuri, lakini ni vizuri sana kunenepa kwa kufuata njia bora za afya ili uendelee kuufanya mwili kunawiri kuliko kufikia malengo kwa kuharibu mwili moja kwa moja. Unaweza kujaribu njia chache kati ya hizi ili uangalia ipi inafanya kazi vizuri kwako.

1. Kula mara nyingi zaidi


Uzito wa miili yetu hutegemea sana kiasi cha chakula bora tunachokula. Wengi tumezoea kula mara tatu kwa siku. Tatizo huja pale ambapo unakuwa huli chakula kingi sana kwa kila mlo, maana mwili unakosa kupata virutubisho vya ziada vya kuhifadhi mwilini.
Miili yetu inatofautiana, watu wengine hawawezi kula chakula kingi wakati mmoja, ndio maana nashauri ule mara nyingi zaidi katika siku – mara 5 hadi 6 ili upate virutubisho zaidi ambavyo mwili utatumia kujijenga.
Ni muhimu pia kufahamu kuwa vyakula vingi vinavyonenepesha hushibisha haraka sababu ya uwepo wa mchanganyiko wa virutubisho vingi mfano nyuzi nyuzi (fiber), ambazo hukufanya ushibe haraka na kwa muda mrefu zaidi. Hivyo, kula kidogo kidogo mara nyingi kunaweza kusaidia kuongeza uzito.


2. Kula nafaka zisizokobolewa


Mwili unaohitaji virutubisho unatakiwa kula vyakula vilivyojaa virutubisho. Vyakula vilivyokobolewa mara nyingi huwa na virutubisho vichache, na huwa havileti afya sawa na vile visivyokobolewa. Hivyo, kula vyakula visivyokobolewa. Tumia bidhaa zilizotengenezwa na nafaka zisizokobolewa – mkate wa ngano isiyokobolewa, ugali wa dona, maharage n.k


3. Kula kwanza, kunywa baadae


Wengi wetu huwa tunaziba nafasi ya chakula tumboni kwa kuanza kunywa vinywaji kabla ya chakula. Ukianza kupata vinywaji – maji au aina ya kinywaji baridi, mwili hupata hisia ya kushiba na hutoweza kula vizuri. Juisi nyingi tunazotumia hazina virutubisho muhimu zaidi ya sukari na maji, hivyo mwili unapata hali ya kushiba lakini bila ya kuwa na virutubisho muhimu ndani yake ya kuweza kuufanya unawiri.
Ni vizuri ukifiria kwanza kula chakula na kumaliza kabla ya kupata kinywaji chochote. Hii itakufanya ule chakula kingi zaidi. Vilevile, kuwa makini kutokunywa kitu chochote wakati wa mlo, maana pia huweza kukata hamu ya kula.


4. Kula vitafunwa kabla ya kulala


Kula kabla ya kulala ni tabia inayokatazwa kwa kulinda afya zetu na pia kutupa nafasi ya kupumzika vizuri. Kula kabla ya kulala si afya sababu chakula kinachomeng’enywa huhifadhiwa moja kwa moja mwilini – matokeo yake unanenepa. Lakini, hii pia ina madhara maana unaweza kukosa usingizi. Ushauri wangu ni kuwa, ni vizuri kama utakula vitafunwa vichache ili kuweza kuwa na kitu tumboni wakati wa kulala – hii haiwezi kukuzuia kupata usingizi mzuri, lakini pia unakuwa na kitu tumboni kinachoweza kutumiwa na mwili katika kukuongezea virutubisho.

5. Kula vyakula bora kwanza


Si kila kitu unachokula huwa kina matokeo sawa mwilini mwako. Kuna vyakula ambavyo hukupa mafuta, kabohaidreti na protini nyingi kuliko vingine. Mwili unahitaji vyakula vyenye kiwango kikubwa zaidi cha virutubisho ili upate kiasi cha kuhifadhi – hapa ndio utanenena. Hivyo, kuwa makini kula vyakula vilivyojaa mafuta yenye afya, wanga na protini.
Vyakula muhimu vya kuchagua ni – mafuta yaliyo salama – mfano mafuta yanayotokana na mimea, nafaka na viumbe wa baharini. Epuka mafuta hatarishi, yatakuletea matatizo zaidi ya suluhisho. Vilevile, kula zaidi protini – mayai, maharage, nyama ya kuku na ng’ombe. Vyakula vyenye wanga ni kama wali, viazi, chips, ugali, kande n.k.


6. Fanya mazoezi, pata lishe bora


Mwili unajengwa zaidi na misuli. Mazoezi husaidia kujenga misuli. Hivyo, njia mojawapo muhimu ya kuongeza mwili ni kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora. Utakapofanya zoezi, mwili wako utahitaji kula zaidi ili kuweza kufidia nguvu unayotumia lakini pia kupata virutubisho vya kujenga seli za misuli inayoharibika wakati wa mazoezi.


7. Acha vyakula vibovu


Unapokula vyakula visivyoongeza kitu mwilini mwako, mwili haupati virutubisho muhimu, hivyo hutumia kile kilichopo kwenye akiba kukufanya uendelee kuishi. Hii inamaanisha unachokula kinatoka kama uchafu lakini mwili unazidi kutumia kile kilichopo kwenye hifadhi. Ni vizuri kuacha kula vyakula ambavyo havina afya, maana vitakufanya uzidi kupungua balada ya kunenepa.
Hakikisha kila chakula unachokula kina virutubisho vingi muhimu kwa afya yako – tumia juisi za matunda halisi, tumia mboga za majani, nafaka halisi zisizokobolewa, achana na vyakula vya kununua na vya kwenye makopo, vingi havina virutubisho muhimu kwa kujenga afya yako.Misosi | Njia 7 za kuongeza uzito
 
Mzizi mkavu kamaliza kila kitu.Ila pia tengeneza juice ya mchanganyiko wa matunda.kama nanasi passion embe papai usisahau kuweka parachichi na sukari.Juice iwe nzito alaf unakunywa glass moja baada ya kila mlo inaongeza hamu ya kula na afya haraka sana.
 
Nawaonea huruma wanaotaka kuongeza uzito, ningekuwa na uwezo ningekupunguzia
 
Back
Top Bottom