Nahitaji kuanzia biashara ya kukodisha vifaa vya harusi

Zillion

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,358
1,807
Wakuu asalaam,

Leo nimeona nilete mawazo yangu hapa kwa ushauri na maoni na zaidi kupata connection kwa wazoefu.

Nimepanga mwaka 2021 nianze kwa biashara ya kukodisha vifaa vya harusi kuanzia magauni ya send off, magauni ya harusi, viatu, maua, usafiri (full package) kuanzia magari manne (na mimi nitayakodi kwa watu pia) Chakula, watu wa mapambo (nimeshaanza nao mazungumzo), MC na Muziki.

Ninaomba kujua sehemu mbalimbali ambazo naweza kupata magauni na vifaa vingine kwa jumla pia watu mbali mbali ambao wanaweza kunikodishia magari yao kwaajili ya huduma za harusi nitakapohitaji.

Pia ningependa kujua wapi vinapatikana viti vya sherehe kwa bei nzuri za jumla( nataka kukodisha pia)

Nb Napatikana mkoani.
 
Sasa mkuu unaenda kukodisha kwa watu wanaokodisha? Apo sijakuelewa.. maan yule unayemkodisha na yeye anafanya hivyo pia, au ni ukipata tukio mnaingia ubia? Miki nafahamiana na jamaa fulani hivi wanakodi magari ya maharusi

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Sasa mkuu unaenda kukodisha kwa watu wanaokodisha? Apo sijakuelewa.. maan yule unayemkodisha na yeye anafanya hivyo pia, au ni ukipata tukio mnaingia ubia? Miki nafahamiana na jamaa fulani hivi wanakodi magari ya maharusi

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Mkuu
Niweke sawa hili,

Kuhusu magari siwazungumzii wale wanaokodisha kama biashara ila ni kwa watu wenye magari binafsi kwa shughuli zao binafsi mimi nitakuwa nakodi kwake "hasa" siku za jmosi ambapo hakuna shughuli nyingi za kiofisi (kwa wafanyakazi)

Yani kama wewe una gani yako nyumbani na mimi naona inafaa kwa shughuli yangu tunaongea unanikodishia kila jmos namimi nafanyia shughuli yangu then nakurudishia.
Tunakubaliana per day.

Kuhusu viti na vifaa vingine nitanunua halafu nitakodisha.
 
Back
Top Bottom