Hapana, ni miaka 10. Mfano leo hii ili ukate bima kubwa inatakiwa hiyo gari iwe imesajiliwa hapa Tanzania kuanzia September 2015 na kuendelea ila ikifika mwakani hutoweza ikatia tena.
Japo kwa magari ambayo usajili wake ni wa zaidi ya miaka 10 kurudi nyuma, ukitaka bima kubwa huwa wanatuma ma assessor wao kwenda kulithaminisha but wanalipa thamani ndogo sana na ili uweze kalikatia bima kubwa inabidi liwe kweny condition nzuri. Kama lina condition ndogo, watakuambia ukatie bima ndogo tu.