Kwahuku dar zinapatikana duka moja kariakoo, lakini sikumbuki jina lake, mara ya mwisho ilikuwa 1.9 milion.
Lakini kwanini unahitaji hiyo ya cc 150? Niliwahi kuona jamaa mmoja wa bodaboda anauza yakwake nilipomuuliza akaniambia inakula sana mafuta, nilipomuuliza kwanini alinunua hiyo, akasema alikuwa hafahamu kuwa 150cc zinakula mafuta sana kwa kuwa injini ni kubwa sifa yake nikwamba zinanguvu sana lakini kwabiashara ya bodaboda hazifai.
Angalizo jingine nikwamba ukitafuta pikipiki aina hiyo lazima uwe muangalifi kwasababu zipo feki zake muda sio mrefu utaanza kusikia kama manyanga.