Kote nmekuelewa, ila hapa
"Pesa sio suluhisho, akili yako ndio suluhisho" sjaelewa!!
Pesa ni matokeo ya akili uliyonayo. Pesa ni wazo tu, na ni wazo kubwa sana. Muda mwingine unakuta mtu anapata pesa lakini baada ya miaka kadhaa anakua masikini, au wale wanaofanya biashara ndogo ndogo alafu wanazitumia vizuri wanajenga nyumba za kupangisha wakati mtu anaendeshwa na STL lakini ananyumba moja tu na ndani kila siku anaimba sina hela. Apo pesa sio kitu, ila wazo juu ya pesa ndio kila kitu. Watu wanaweka pesa kama vile ndo kitu pekee maishani.
.
Mfano, kuna siku nilikua na braza angu mmoja katika yard yao wanauza magari, apo bado nakua kua kwaiyo bado nina zile akili za 'sina hela, ela ndio suluhisho'. Nikamshirikisha braza wazo langu alafu nikamwambia tatizo sina hela, akaniambia hata nikikupa hela hutofanikiwa. Nilijisikia vibaya kuniona ivo, nikamuuliza kwanini, akaniambia pesa ni wazo tu, cha muhimu uwe na malengo na kamwe usije ukaweka pesa kwenye nafasi ya malengo. Kweli, baadaye sijui ata pesa nilipataje nikajiendeleza. Nikajifunza achana na izi akili za 'tafuta pesa' badala yake nikaweka akili ya kufanya kitu kitakachosaidia wengine. Cha kushangaza zaidi maisha yanasonga hakuna kilichopungua zaidi ya kuongezewa zaidi.
.
Ukitukuza pesa kwamba itakupatia wanawake, utaishia kuwavutia madanga na wanawake wasiojali kingine zaidi ya pesa zako. Ila wanawake wenye kujielewa sawa watavutiwa nawe ukiwa na pesa lakini kutukuza kwako pesa utajikuta sehemu za kusimama kuwa mwanaume unaweka pesa kama vile ndio suluhisho la kila kitu.
.
Pesa ni muhimu sana LAKINI kwenye sehemu inayohusika.
.
Pesa ukipoteza unaweza kuipata tena, lakini akili usipoikuza uchafu utajaa na maisha yanakua machafu vile vile.