NAHISI: Wenyeviti, Naibu Spika na Spika wa Bunge wanaihujumu CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NAHISI: Wenyeviti, Naibu Spika na Spika wa Bunge wanaihujumu CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUJITEGEMEE, Jul 13, 2012.

 1. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Ukirejea uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru M. jinsi kampeni za CCM zilivyoendeshwa ilidhihirika kuwa baadhi ya makada wa chama hicho ama kwa kudhamiria au kwa kupitiwa walihujumu umaarufu wa CCM na kusababisha kushindwa kurejesha jimbo hilo. Wafuatiliaji mnalijua hilo.

  Hisia zangu ni kiwatuhumu viongozi hao wabunge niliowataja ktk kichwa cha uzi huu zinatokana na namna wanavyozidi kupukutisha imani ya wananchi juu uimara waCCM kuendelea kushika hatamu.Hisia hizi zinadhibitishwa na namna viongozi hawa wanavyoshindwa kumudu kuendesha vikao vya bunge mara kwa mara. Maelezo juu ya hilo yapo mengi hapa Janvini (JF). Hivyo nalazimika kuwahisi moja kwa moja viongozi hawa wanashiriki kuihujumu na kuiua kikamilifu CCM ktk siasa za nchi hii.

  Yawezekana viongozi hawa wakadhani wanawadhibiti wabunge wa vyama vya upinzani kutoa michangao yao bungeni kwa imani kuwa hapo wanadhibiti kasi ya vyama vya upinzani kutambulika kwa wananchi wengi, hivyo kufikiri kuwa CCM itaendelea kushika hatamu kwa ukiukwaji huu wa uendeshaji wa vikao vya Bunge. Kama wanadhani hivyo wamekosea. Wananchi wengi wanafuatilia kwa karibu sana kinachoendelea bungeni na namna viongozi hawa wanavyoendesha vikao huko. Matukio haya ya kuwadhibiti wabunge wa vyama vya upinzani wanaoikosoa serikali ya CCM katika mijadala iliyoko bungeni kwa ukali yanawafanya wananchi kuanza kuwahurumia wabunge hawa na hivyo hata wale waliokuwa wanadhani CCM inatenda haki kuanza kuichukia pia.

  Mazingira wanayoyatengeneza viongozi hawa wa Bunge katika hali ya sasa ya siasa za Tanzania nidhahiri yanaihujumu CCM.

  Nimeliona hilo na imenilazimu niliseme.
   
 2. a

  andrews JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​naibu spika na spika wake wote ni majambazi wa kisiasa
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  bitter truth! Halafu wamekuja na kamsemo eti sikutoi nje! Wapuuzi kweli hawa
   
 4. M

  Mbundenali Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 9, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hakuna spika atakayeweza kumfikia sitta, ndugui na makinda hamna kitu ni mipasho tu!
   
 5. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo? Watu wengine vipi, kila mwenye hisia aki post hisia zake hapa JF nafikiri Server ya JF itajaa. Ushauri wa bure ukiwa na hisia discuss na mke wako
   
 6. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hakuna cha wenyeviti, naibu spika wala cha spika wa bunge kuihujumu CCM, CCM inajihujumu yenyewe kwa ahadi zisizotekelezeka na kwa kuwatelekeza waTanzania huku wakubwa wakiendelea kunemeka kwa mikataba mibovu na kutumia vyombo vya dola kukandamiza demokrasia
   
 7. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Akili ndogo kuongoza akili iliyokubwa...mambo hayaendi. Ni sawa na kulazilisha maji ya mto yapande mlimani.
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,922
  Trophy Points: 280
  Mwogope sana Binadamu akifikia mwisho kufikiri maana ni sawa na mfu.Hao uliowataja wamafika mwisho wa kufikiri.
   
 9. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya sana viongozi hawa wakifanikiwa kuizamisha CCM 2015 kwa matendo yao haya, watakuwa wamesababisha chama kitakachopata nafasi ya kuongoza nchi hii katika uchaguzi wa mwaka huo, kuwa na chama kikubwa cha upinzani legelege ambacho hakiwezi kumudu shughuli ya kuikosoa serikali kwa namna viongozi wake walio wengi kushidwa kujenga hoja huku wakiendekeza ushabiki wa kisiasa katika masuala ya msingi yanayowagusa wananchi moja kwa moja.
   
 10. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Naona na Mh.Lukuvi kajiunga na hawa jamaa kuiua CCM.

  Yaani Mh. Lukuvi anataka tuamini kuwa anawahurumia sana CDM wasije wakaadhibiwa kwa kuzungumzia jambo ambalo liko mahakamani kweli? Nadhani sheria inaelekeza ni adhabu gani utapata kwa kuingilia mwenendo wa kesi kwa kuijadili nje ya mahakama. Sina hakika kama CDM wanaweza kukosa weledi juu ya jambo.
   
 11. m

  majoge Member

  #11
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kweli kabisa mkuu,Sitta alikuwa anaijenga ccm na kuonyesha kuwa hakuna kupendelea,sasa hawa vilaza wanakiua chama chao bila kujua ili wasifiwe na JK ambaye anelekea kustaafu.
  Mungu tuepushe na hawa wapenda posho walioko madarakani.!!
   
 12. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  CCM is a walking dead man. Sio kwamba wanaihujuma BALI NDIYO UWEZO WA KUFIKIRI UMEFIKIA MWISHO!

  1. Spika na Naibu Spika kupindisha kanuni za bunge ..... Wanaihujumu CCM
  2. Blunder ya TISS kumteka na kumtesa Dr. Ulimboka ...... Wanaihujumu CCM
  3. Blunder ya Kova kutuletea mtekaji wa "kuchongwa" wa Ulimboka ...... Wanaihujumua CCM
  4. Matusi ya Lusinde, Nchemba, Mkapa Arumeru ...... Wanaihujumu CCM
  5. AG Werema kubaliki mswaada wa mabadiliko ya katiba mbovu ...... Anaihujumu CCM
  6. Mgawo wa Umeme usiokwisha .......... TANESCO inaihujumu CCM
  7. Bilioni 300 zilizofichwa USWISS na vigogo na wafanyabiashara wa Tanzania .......... Wanaihujumu CCM
  8. Mgogoro wa madaktari na serikali ............. Madaktari wanaihujumu CCM

  CCM wamefikia mwisho wa KUFIKIRI hakuna anayewahujumu bali wanajihujumu wenyewe.
   
 13. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  never seen such incompetent ppo like the ones you've mentioned in the history of our parliament.
   
 14. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Loh ! hii hatari, Werema naye kaingia kwenye msafara wa kuizamisha CCM pia. Kauli ya .... sana hii ametoa.

  Mimi nilijua tu kuwa kitendo cha CCM kushindwa kumkaripia 'Mh' Lusinde kwa maneno yake ya aibu/kujiabisha yeye na chama chake wakati wa uchaguzi wa mbunge Arumeru M., basi CCM ilikuwa imegundua njia mpya ya kujizika kwa kuanzisha Chuo Kikuu kipya cha cha kufundisha propaganda ya maneno ya aibu/kujiabisha huku wahitimu wa kwanza wa chuo hicho wakiwa makada wake wakuu.

  Hisia zangu nadhani zaelekea kuwa sahihi.
   
 15. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Sasa ni rahisi kutabiri nikitugani Naibu Spika ataweza kutoa majibu gani pindi anapoomwa mwongozo na mbunge kutoka kambi ya upinzani.

  Rejea shughuli ya bunge leo, jinsi alivyojibu mwongozo wa Mh. Mkosamali na Mh.Lissu. Naibu spika kakiuka kanuni dhahiri inayotaka nusu ya idadi ya wabunge kuwa nusu ndani ya bunge wakati wa kupitisha bajeti.

  Poleni sana wapenda uwepo wa CCM.
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  yote kwa yote nawe unaefatilia BUNGE pole sana,,,,,,
   
 17. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  miaka 50 ahadi zile zile chama kile ,watu wale wale wanabadilshana tu toto baba , mama ,imani itatoka wapi ,pengine ashuke malaika tu.
   
 18. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Jana Ndugai kaingizwa mjini na Lisu bila kujua. Unapoonekana unaitetea Zanzibar halafu kiongozi wa juu serkali ya Muungano anapinga inaamsha hisia mbaya za Wazanzibari dhidi ya muungano ambao sasa ndio kidonda cha CCM. Hivyo Maskini Ndugai alidhani anadhibiti kumbe anatoboa tundu.
   
 19. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tetesi za mgomo wa walimu ni hujuma kwa CCm
  Shida za wazanzibari kwa muugano ni hujuma kwa CCm
   
 20. S

  Samuel Ibambasi New Member

  #20
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 20, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli haya mambo yanasikitisha sana, sidhni kama ni kuihujumu ccm bali huu ni udhihirisho wa uwezo wa watu binafsi maana sasa tunaona gap kubwa kabisa kati ya Mzee Sitta na waliopo sasa, kwa mazingira haya wa kulaumiwa ni ccm wenyewe maana ndivyo walivyoamua kuchagua na hakuna anayewahujumu.
   
Loading...