binti wa kikwere
Member
- Sep 5, 2014
- 67
- 34
Nahisi mimi sina MOYO bali nina memory card ambayo ni rahisi kuweka kitu na kukifuta muda wowote ukihitaji naweza nikawa na mpenzi nikampenda kupita maelezo na maisha yakaendelea vizuri tu ghafla nabadili mawazo na kumuondoa kabisa akilini mwangu na nakuwa sitaki tena hata kumuona wala kumsikia na inakuwa mwisho wetu wa mahusiano hata anibembeleze vipi nakuwa siwezi rudisha moyo nyuma, imeshanitokea kama mara tatu hivi hiyo hali hebu nishaurini jamani isije ikawa ndio jini mahaba kama ambavyo huwa nasikia habari zake.