Nahisi nina tatizo la figo, nakata tamaa

Pole sana . Muone daktari akusaidie kukufanyia vipimo. Pima mkojo pamoja na culture na sensitivity, pima damu kuangalia utendaji kazi wa mafigo yako , ultrasound inaweza kuboresha wigo wa kuangalia mafigo na vitu vingine tumboni. Pima na choo. Kukata tamaa kama unavyosema kunaweza kuchangia sana hali ya kujisikia mchovu , mbali na maambukizi.
Ultra sound inaweza kuwa kiasi gan mkuu sina bima
 
Ultra sound inaweza kuwa kiasi gan mkuu sina bima
Niwie radhi sana ndugu yangu naishi ughaibuni hivyo nikiri kwa nyumbani sijui gharama zikoje. Kupima mkojo kuangalia kama kuna maambukizi na kupima damu kuangalia kama figo ni nzima kungesaidia zaidi kuliko ultrasound
 
Hello! JF Doctors

Ninasumbuliwa na U.T.I almost miaka mitano sasa nimetumia dawa mbalimbali lakini hali ikawa inajirudia untill now Nina hili tatizo, Lakini kitu kinachoniogipesha sasa hivi ni kuwa na dalili zingine ambazo zinanitisha zaidi...

Kwa hayo uliyotaja sion hapo ugonjwa wa figo, inawezekana kabisa ni gallstone nenda hospital ukapime upate natibabu sahihi
 
Sawa mkuu
UTI mara kwa mara, maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kiuno kuuma hiyo ina uwezekano mkubwa wa kuwa ni UTI ambayo haikutibiwa vizuri na dawa zenye viwango nadhani na ndiyo maana nashauri kupima mkojo pamoja na culture na sensitivity itakayoonyesha aina ya maambukizi pamoja na dawa inayowaweza wadudu walioonekana.

Gall stones mara nyingi ni maumivu tumboni juu zaidi mbali na kitovu katikati chini ya kifua (kidari) na maumivu huzidi baada ya kula au kunywa. Maumiu ya mgongo huwa ni mgongo wa kati siyo kiunoni.

Fanya kipimo kimoja kimoja utapata ufumbuzi. UTI ya mara kwa mara kuna na uwezekano wa mawe kwenye kibofu na xray ya kawaida inaweza kusaidia kama ultrasound ikiwa ghali.
 
Niwie radhi sana ndugu yangu naishi ughaibuni hivyo nikiri kwa nyumbani sijui gharama zikoje. Kupima mkojo kuangalia kama kuna maambukizi na kupima damu kuangalia kama figo ni nzima kungesaidia zaidi kuliko ultrasound
So sorry en thank for that mkuu
 
UTI mara kwa mara, maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kiuno kuuma hiyo ina uwezekano mkubwa wa kuwa ni UTI ambayo haikutibiwa vizuri na dawa zenye viwango nadhani na ndiyo maana nashauri kupima mkojo pamoja na culture na sensitivity itakayoonyesha aina ya maambukizi pamoja na dawa inayowaweza wadudu walioonekana. Gall stones mara nyingi ni maumivu tumboni juu zaidi mbali na kitovu katikati chini ya kifua (kidari) na maumivu huzidi baada ya kula au kunywa. Maumiu ya mgongo huwa ni mgongo wa kati siyo kiunoni. Fanya kipimo kimoja kimoja utapata ufumbuzi. UTI ya mara kwa mara kuna na uwezekano wa mawe kwenye kibofu na xray ya kawaida inaweza kusaidia kama ultrasound ikiwa ghali.
Shukrani sana mkuu
 
Hello! JF Doctors

Ninasumbuliwa na U.T.I almost miaka mitano sasa nimetumia dawa mbalimbali lakini hali ikawa inajirudia untill now Nina hili tatizo, Lakini kitu kinachoniogipesha sasa hivi ni kuwa na dalili zingine ambazo zinanitisha zaidi....
Umeenda kunuona daktari?
 
Tafuta dawa za mizizi unywe mkuu achana na madawa hayo ya hosp nenda maduka ya dawa asili wakusaidie mapema usije kujutia .
 
Hapana mkuu....mkojo wa rangi ya reddish brown na dark yellow sometyms huwa na viuchafu fulani Ni kama maziwa
vipi kuhusu presha yako na mapigo yako ya moyo yapo sawasawa? possibly inaweza kua kidney stones (uvimbe mdogo ktk kidney) au ingection yoyote kwenye upper urinary tract
 
Back
Top Bottom