Nahisi mchumba Wangu Ataniletea mikosi

Nahisi mchumba Wangu Ataniletea mikosi

Elementi

Member
Joined
Apr 9, 2019
Posts
60
Reaction score
157
Mimi ni kijana wa miaka 25 nafikilia kuoa sasa.. Kuna Mwanamke nimejuana nae miezi 7 iliyopita

Ni Mwanamke anaenisikiliza na kuniheshimu ,miezi yote niliyo kuwa nae kwenye mahusiano sijaona changamoto mbaya kwake na nilipanga mwezi wa 10 mwaka huu awe Mke Wangu rasmi

Sasa Leo nikiwa napiga nae stori amejikuta ananisimulia mambo ya nyumbani kwao kuhusu Mama yake na Baba yake...

Alipo kua mdogo Akulelewa Kabisa na mama yake, alilelewa na Mama wa kambo kwa mda Mrefu ingawa Mama yake mzazi yupo hai...

Anadai alipoanza kujitambua Bibi yake akamuweka wazi kuwa baba yake na Mama yake ni Ndugu Kabisa lakini kwabahati mbaya walijikuta wanafanya mapenzi na ndipo akapatikana yeye

Yaani kwakifupi Baba yake na Mama yake ni ndugu.. Yeye kapatikana kimakosa tuu...

Sasa hapo niko njia panda wakuu.. Nimeanza kufikilia kumuacha tuu uyu Mwanamke, asije niletea mikosi apo baadae..

Naombeni mawazo yenu kuhusu jambo hili jamani...

)
 
Acha imani potofu mkuu sikatai kwamba kapatikana kutokana na dhambi lakini Mungu angeamua kila mtoto aliyepatikana kutokana na dhambi awe na mikosi basi nina uhakika dunia ingekuwa imeharibika mara kumi zaidi ya ilivyoharibika sasa maana watoto wa aina hiyo ni wengi mno na siyo wote wenye mikosi cha msingi wewe angalia tabia zake na maisha yake binafsi
 
Sijui huwa mnajisikiaga vipi 'Mnapo wa tumia vijana wa watu (Me/ke) na kuwa acha solemba ''

Hii sio Tabia njema kabisa
 
Binti hana kosa lolote hapo. Na mikosi ni dhana tu tunadhania. Nawe usimkosee
 
Wewe labda kama unasababu zako nyingine, umekaa nae miezi saba unamkula leo ndo unamuona atakuletea mkosi.. Sasa huo mkosi utokee wapi hapo hizo imani tu na kama ni mkosi wangepata wazazi wake sio wewe kwasababu yeye wala wewe hamna hatia yeyote.
Hebu muoe acha kusikiliza propaganda za mitaani.
 
Mimi ni kijana wa miaka 25 nafikilia kuoa sasa.. Kuna Mwanamke nimejuana nae miezi 7 iliyopita

Ni Mwanamke anaenisikiliza na kuniheshimu ,miezi yote niliyo kuwa nae kwenye mahusiano sijaona changamoto mbaya kwake na nilipanga mwezi wa 10 mwaka huu awe Mke Wangu rasmi

Sasa Leo nikiwa napiga nae stori amejikuta ananisimulia mambo ya nyumbani kwao kuhusu Mama yake na Baba yake...

Alipo kua mdogo Akulelewa Kabisa na mama yake, alilelewa na Mama wa kambo kwa mda Mrefu ingawa Mama yake mzazi yupo hai...

Anadai alipoanza kujitambua Bibi yake akamuweka wazi kuwa baba yake na Mama yake ni Ndugu Kabisa lakini kwabahati mbaya walijikuta wanafanya mapenzi na ndipo akapatikana yeye

Yaani kwakifupi Baba yake na Mama yake ni ndugu.. Yeye kapatikana kimakosa tuu...

Sasa hapo niko njia panda wakuu.. Nimeanza kufikilia kumuacha tuu uyu Mwanamke, asije niletea mikosi apo baadae..

Naombeni mawazo yenu kuhusu jambo hili jamani...

)
Cha maana na cha kuangalia katika miezi saba hiyo ukupata mkosi wowote, anakupenda wampenda na ni mtu wa muhimu sana kwako jaribu kuangalia ni wanawake au wanaume wangapi ambao wapo wazi kihivyo kuelezea maisha yao yandani kabisa ni wachache sana,yeye kukueleza hayo inamaana amekuamin sana kama ubavu wake.
Wewe chukua mtoto weka ndani maisha yaendelee maana utakapo mwacha utakaye mpata ni maumivu tu
 
Ukimuacha unataka amuoe Nani acha dhambi ukwel wake umemueka huru oa binti huyo haraka
 
Back
Top Bottom