Nahisi kuna jambo linapangwa uchaguzi wa madiwani

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,306
6,514
Muamko wa wananchi wa kata zinazotaraji kufanya uchaguzi wa madiwani kuhudhuria mikutano ya wapinzani umeleta kitisho kikubwa kwa chama tawala hali inayopelekea wao kufanya jambo fulani kwenye uchaguzi wa tarehe 26 jumapili ijayo.

Hamahama ya baadhi ya wapinzani huku wote wakitoa sababu moja ya ufisadi ni coverage inayotaka kuaminisha umma kuwa CCM inakubalika ilhali si hivyo.

Nionavyo ushindi wa CCM kwenye kata hizo utatetewa na hali hii ya sasa endapo umma utahoji juu ya ushindi huo.

Wapinzani kuweni makini kwani kwa sasa ccm inatumia ajenda ya hama hama na sababu ikiwa ufisadi, huku mambo kama uchumi, utawala bora na demokrasia yakiwa hayatajwi na wahamaji.

Jumapili tuwe makini maana.....umma unapumbazwa.
 
Back
Top Bottom