Nahisi kama NMB Wanataka kuniimbia tsh 400,000.

Nahisi kama NMB Wanataka kuniimbia tsh 400,000.

Shy land

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
6,245
Reaction score
2,856
Wakuu naombeni msaada wenu nimefanya mhamala wa kuhamisha pesa kutoka kwenye accaunt yangu ya NMB Saa mbili na asubuhi kiasi cha tsh400000, lakin hadi sasa hela bado haijasoma mpesa. niliwapingia simu voda wakaniambia niwasaliane na NMB.. Wakanipa namba 0764700500 na, 0800112233 nilipowapingia wakaniambia kunamatatizo kwenye NMB MOBILE, lakini mihamala ambayo imekamilika itasomeka baada ya masaa matatu. na kila nikipanga naambiwa itakamilika baada ya masaa matatu.

chakusikitisha zaidi hadi sasa yamepita masaa tisa na hela bado haijasoma mpesa. na nimeenda kwenye atm machine za NMB nikakuta salio limepungua ile laki nne haipo.

siku yangu imeisha vibaya sana kwa leo maana mambo yangu yote yamesimama, nilikuwa na mpango wa kutuma hela kwa watu ili kukamilisha maswala yangu. sasa wale watu wameniona mimi nitapeli maana toka asubuhi nawaahidi nitawarushia baada ya dakika chache.

wadau naomben msaada wenu nifanyaje? kwa sasa.
NB Asanten sana kwa wale muliotia moyo muamala umekamila sasa hv saa 21:26
 
Fanya subra ndugu yangu, ndo negative impact ya ict hiyo

hakuna njia nyingine tofauti na subira? maana kama kusubiri nimesubiri sana lakn naona ni matokeo negative yanayoendelea kuyapata hadi sasa.
 
Achana na matumizi ya NMB mobile ndugu, hiyo kitu sio nzuri kabisa!!! Kuna mtu ilimtokea km hivyo na mpaka leo mwaka umepita hiyo hela hajaipata!!
 
sijawahi kupatwa na tatizo kama la leo tangu nianze kutumia hii huduma,!! aaaa!

Usiogope juzi nimetuma hela kwa mtu wa mpesa ilichelewa sana lkn ilifika, endelea kuvuta subira
 
ukiwa na haraka uctumie mpesa...

maana muhamala unaweza kukamilika zaidi ya masaa 24.
 
hakuna njia nyingine tofauti na subira? maana kama kusubiri nimesubiri sana lakn naona ni matokeo negative yanayoendelea kuyapata hadi sasa.

mkuu njia nyingine tofauti na subira, ni kuwa mvumilivu.
mitandao ya mpesa nk nk ndio inakuwa imepatwa na shida ivo kushindwa kukamilisha transaction, ila ndani ya 24 system uwa zinafanya reconciliation na then kususpend mihamala batili, ivo itabidi wabatlishe huo muhamala na kurudisha hela kwa akaunti, mkuu hauwezi kuibiwa, inafaa ukope kwingine then utarudisha....pole.
 
Aisee hii mambo ya M-PESA unaweza kuaibika mimi kuna wakati nilikuwa nalipia Tiketi ya Fastjet na nilitaka kusafii siku hiyo hiyo pesa imetoka lakini sipati uthibitisho wa Fastjet kama umefika.
 
acha kubabaika jamaa hayo ndio mambo ya system,uwezekano wa hiyo pesa kuludi bank ni mkubwa ila gharama za makato hazitarud
 
Wakuu naombeni msaada wenu nimefanya mhamala wa kuhamisha pesa kutoka kwenye accaunt yangu ya NMB Saa mbili na asubuhi kiasi cha tsh400000, lakin hadi sasa hela bado haijasoma mpesa. niliwapingia simu voda wakaniambia niwasaliane na NMB.. Wakanipa namba 0764700500 na, 0800112233 nilipowapingia wakaniambia kunamatatizo kwenye NMB MOBILE, lakini mihamala ambayo imekamilika itasomeka baada ya masaa matatu. na kila nikipanga naambiwa itakamilika baada ya masaa matatu.

chakusikitisha zaidi hadi sasa yamepita masaa tisa na hela bado haijasoma mpesa. na nimeenda kwenye atm machine za NMB nikakuta salio limepungua ile laki nne haipo.

siku yangu imeisha vibaya sana kwa leo maana mambo yangu yote yamesimama, nilikuwa na mpango wa kutuma hela kwa watu ili kukamilisha maswala yangu. sasa wale watu wameniona mimi nitapeli maana toka asubuhi nawaahidi nitawarushia baada ya dakika chache.

wadau naomben msaada wenu nifanyaje? kwa sasa.

Fatilia sana coz wanasumbua sana mm ilishawahi kutokea 100000 nilipiga cm adi nilikoma wananiambia tu baada ya masaa matatu lakini wapi
Mpaka ilibidi niende NMB house pale wakawpigia cm watu wa nmb mobil ndo wakarudisha.

Ila kwaushauli uwe unatumia tigo pesa ukiamisha kutoka bank nidakika iyoiyo imefika mm niliachanakabisa na mpesa coz wanazingua sana unaamisha asubuhi ela inaingia ucku.
 
ndugu yangu katoa laki nne akakatwa Mara mbili ikawa laki8,na hili amegundua sku ya pili ilikua shida acha kabsa,cjui ndo kunatafutwa hela za uchaguz!
 
ndugu yangu katoa laki nne akakatwa Mara mbili ikawa laki8,na hili amegundua sku ya pili ilikua shida acha kabsa,cjui ndo kunatafutwa hela za uchaguz!

Sitorundia tena kufanya ujinga wa namna hii, mimi kuhamisha tu nimekatwa tsh elfu 8. hapo bado sijatoa mpesa.
 
@NMB
Jitahidini kuwa imara. Mpaa mtu anafika kote huku, basi mmemchanganya.

Biashara inapungua speed namna hii as watu sasa tunakuwa tunajua kuna udhaifu.
 
nmb
Jitahidini kuwa imara. Mpaa mtu anafika kote huku, basi mmemchanganya.

Biashara inapungua speed namna hii as watu sasa tunakuwa tunajua kuna udhaifu.

Kweli ni NMB Tanzania mimi naomba tu, wajitahidi kuweka huduma zao vizuri. maana ni usumbufu wa hali ya juu unafanya muamala nmb mobile sasa moja asubuhi na unakamilika saa 4 usiku.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom