Jamani yaani mwenzenu mimi nahisi kama nimerogwa hivi
Tangu nipate ajira nimekuwa mtu wa magonjwa tu yaani kila ikifika Jumamosi na Jumapili kunaibuka ugonjwa wa mpya
Hali hii inanisumbua kidogo, na kila nikifika hospitali hata kabla sijaonana na daktari nahisi napona au ugonjwa unazidi saana
Nilianza na ugonjwa wa mgongo, nikacheki wakaniambia ni maumivu tu mikapona
Nikashikwa na ugonjwa wa shambulio la hofu, nikapona
Nikashikwa na ugonjwa wa tumbo kujaa gesi na chakula kutokusagwa vizuri tumboni nikapona
Nikashikwa na ugonjwa tena wa shambulio la hofu nimepona
Sasa hivi nimeshikwa na ugonjwa wa kichwa nasikia maumivu kisogoni. Na kuna muda nahisi kichwa chepesi au kizitoa na ninasikia kizunguzungu sometime
Sasa sijui magonjwa haya yananitakia nini mimi!