Nahisi harufu ya DAMU!!

Nahisi harufu ya DAMU!!

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
36,455
Reaction score
45,029
Watanzania hamjawahi kupigana hata siku moja - hamjawahi kuona mauaji makubwa huwa mnasikia tu redioni na kwenye luninga zenu.

Harufu ya damu inanukia, dharau zimezidi kati ya watawala na watawaliwa, udini umepandikizwa zaidi- narudia tena harufu ya damu ndugu zangu, tutachinjana zaidi ya wakenya.

Mbaya zaidi hakuna anayekemea, viongozi wa kisiasa hasa walioko madarakani ndiyo kwanzaa wanakoleza moto; hii nchi haitakalika, haya majumba yatabakia magofu - ni hatari sana kuchochea udini, ukabila kwa watu waliochoka na kukata tamaa kimaisha ( they have got nothing to loose ) watakuwa tayari kwa lolote.

way forward:

1. Serikali ya CCM mara moja ikataze mambo haya na hizo kesi kesi za kisiasa ambazo zinafunguliwa kukomoana zifutwe mara moja;
2. Tufanya mjadala wa kitaifa baina ya wakristo na waislam na tutoe madukuduku yote tuliyonayo moyoni - tusameheane.
3. Serikali iweke mazingira ya equal playing ground kati ya CCM na Vyama vya upinzani - Washindane kwa hoja na serikali isijiingize kwenye ushabiki wa kisiasa. sisi wananchi tutachagua pumba ipi na mchele ni upi
4. Mwisho kabisa; TUHESHIMIANE, heshima ni kitu cha bure, kwa mfano baba wa taifa alitupenda na alituheshimu na tukamheshimu pia na ndiyo maana tunamkumbuka mpaka leo ; je wewe kiongozi wa nchi unatimiza wajibu wako? jiulize.

Tukifikia uchaguzi mkuu au hizi ndogo ndogo basi mambo ya kupika pika ya wanasiasa uchara yaachwe mara moja, tusitumie umaskini wa wapiga kura uwe mtaji wa kisiasa, tusitumie udini kama mtaji wa kupata kura na kubwa zaidi Tuheshimu maamuzi wa wananchi (wenye dola), mambo ya kuiba kura yataleta matatizo makubwa mno.

Amani yetu hii ndugu zangu imo mikononi wa serikali ya CCM, itaamua inatupeleka wapi, wao ndiyo wameshikiria kikombe hiki.

Nimetumwa kuja kuwafikishia ujumbe huu muhimu, ukikubali MEZA ukikataa TEMA ila damu inanukia kama mtayapuuza hayo.
 
Jamii ya kimataifa ianze kuiangalia Tanzania kwa jicho la karibu kwani dalili zimeanza kujitokeza mapema. Wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda Koffi Annan aliambiwa akafikiri ni mzaha ila matokeo yalionekana. Najua walioko madarakani wanafikiri nguvu za dola huwa zinatosha hilo wanajidanganya historia inadhihirisha si hivyo. Rai yangu kwa Rais aifanyie kazi hii wapambe wake waache kumpotosha wao wanafaidika nini kutumbukiza Taifa katika shida kama hii hatujachelewa hatua inahitajika it is getting serious wandugu
 
ukimtaja Nyerere wakakusikia hao wanaosema kawakandamiza atakwambia una mfumo kristo,wewe haya ,manake kunawatu wameisha jiandaa kuimalizia hii amani ndogo iliyopo kwa kisingizio walionewa sana.
 
1. Serikali ya CCM mara moja ikataze mambo haya na hizo kesi kesi za kisiasa ambazo zinafunguliwa kukomoana zifutwe mara moja;
2. Tufanya mjadala wa kitaifa baina ya wakristo na waislam na tutoe madukuduku yote tuliyonayo moyoni - tusameheane.
3. Serikali iweke mazingira ya equal playing ground kati ya CCM na Vyama vya upinzani - Washindane kwa hoja na serikali isijiingize kwenye ushabiki wa kisiasa. sisi wananchi tutachagua pumba ipi na mchele ni upi
4. Mwisho kabisa; TUHESHIMIANE, heshima ni kitu cha bure, kwa mfano baba wa taifa alitupenda na alituheshimu na tukamheshimu pia na ndiyo maana tunamkumbuka mpaka leo ; je wewe kiongozi unatimiza wajibu wako? jiulize.
inasikitisha kuona watu ambao wanapewa jukumu la kupiga propaganda uwezo wao ni mdogo na wanafikiria kidhaifu hata zaidi ya watoto wa form IV waliopata sifuri japo wengine wana class A.
Na ni hawa hawa waliopelekea kuheshimiana katika nchi hii kutoweke na kwa upeo wao mdogo hawajui kuwa tukiingia kwenye matatizo nao wataathirika

Kongolo

Umenena Kamanda wangu ila haya yote uliyosema hakika Mwenyenzi MUNGU wetu wa rehema ndiye akasimame na kutunusuru na haya yaliyowazi yakija kwa hakika yeye ndiyo awezaye!

LISEMWALO LIPO NA KAMA HALIPO HAKIKA LAJA.
 
Last edited by a moderator:
Hakika la kufa harisikii. Hatawakiambiwaje bado tu hawasikii. Huzi huu utawaona tu. kwao kila kitu mzaa, wanaona sawa kuwasingizia wenzao ugaidi. Hawachukui hatua zozote kulinusuru taifa.

Hakuna viongizi wenye hekima ngazi za juu kuukemea upuuzi huu? Hamwezi jiuliza nini kilichoko nyuma ya pazia kama Mwangosi aliuawa lakini serikali hii ikakaa kimya. Mipango tu ya juzi ya kumwangamiza Kibanda inausishwa haraka na video ya Lwakatare. Siku sita mtu yuko maabusu, kiongizi wa kitaifa, aliyeheshimiwa na watu na bado anaheshimiwa lakini polisi wanafanya danadana yakumunyima dhama.

Udharirishaji wa namna hii ni waajabu sana. Kama haki hawezi kutendaka kwa viongozi kama hawa inakuwaje mwananchi wakawaida?
 
Tujiulize wazee wa CCM,Mkapa,Ally Hassan Mwinyi,Kingunge,Majaji wakuu wastaafu na wengineo walioshika nyadhifa mbalimbali,huu ni wakati wenu wakuwaambia walioshika madaraka wanayoyapanga kwa faida yao ni balaa kwa Taifa letu.Viongozi wa dini tafadhalini nafasi nii hii likitokea lakutokea hata nyinyi mtalaumiwa maana mko duniani ili muhakikishe watu wa taifa lenu wanaishi kwa amani.Ikipotea siyo Mapdre,wachungaji wala mashekhe watakaosalimika kulaumiwa na kuhukumiwa na mungu wanayemuabudu.
 
Hakika la kufa harisikii. Hatawakiambiwaje bado tu hawasikii. Huzi huu utawaona tu. kwao kila kitu mzaa, wanaona sawa kuwasingizia wenzao ugaidi. Hawachukui hatua zozote kulinusuru taifa.

Hakuna viongizi wenye hekima ngazi za juu kuukemea upuuzi huu? Hamwezi jiuliza nini kilichoko nyuma ya pazia kama Mwangosi aliuawa lakini serikali hii ikakaa kimya. Mipango tu ya juzi ya kumwangamiza Kibanda inausishwa haraka na video ya Lwakatare. Siku sita mtu yuko maabusu, kiongizi wa kitaifa, aliyeheshimiwa na watu na bado anaheshimiwa lakini polisi wanafanya danadana yakumunyima dhama.

Udharirishaji wa namna hii ni waajabu sana. Kama haki hawezi kutendaka kwa viongozi kama hawa inakuwaje mwananchi wakawaida?
yes mkuu, mifano ni mingi sana ya udhaifu wa viongozi wetu, hata hili la uchinjaji wa nyama hebu fikiria lilivyoharibu mahusiano ya kidugu (acha majeraha) kati ya waislam na wakristo.
 
Nashauri tuanze na mali za viongozi popote pale zilipo make hamna amani tena kila kona kila siku umaskini nao umetamarak
 
Nashauri tuanze na mali za viongozi popote pale zilipo make hamna amani tena kila kona kila siku umaskini nao umetamarak
kaka wenyewe hawalijui hilo, mali zao zote zinafahamika - sasa target itakuwa kuziteketeza ili kuanza upya - tunakoelekea ni kubaya -- we better sort it now.

Yaani mwingine anaishi maisha kama ndege mtini mwingine kama peponi, mbaya zaidi wa peponi anamdharau huyu wa jehanam, aisee!!

Tena hizi chuki zimeshaanza, wee kama una kigari chako ukamgusa mtu kwa site mirror kidogo (kwa bahati mbaya) uone reaction yake, as if wewe ndiyo unakusanya kodi zao na ndiyo umesababisha matitizo yote haya kwenye nchi. sasa mtu mwenye matatizo kama haya anakuwa hawezi kufikiri vizuri tena unamwekea mengine ya udini yaani kichwa chake ndiyo kinachemka kabisa tayari kwa lolote.
 
Watauana maskini kwa maskini, matajiri,mashehe,mapadri na wanasiasa watatia bomba na kurudi mambo yakitulia.
 
Kwa hari ilivyo atayepingana nawe huyo atakuwa na agenda ya siri, hari si shwari tena, mambo ya udini kila kona.

Mungu atuepushe na balaa hili lililoingizwa na wanasiasa uchwara wa CCM
 
Kwa hari ilivyo atayepingana nawe huyo atakuwa na agenda ya siri, hari si shwari tena, mambo ya udini kila kona.

Mungu atuepushe na balaa hili lililoingizwa na wanasiasa uchwara wa CCM
mbaya zaidi wanaopandikiza udini ni wanasiasa, sasa tukianza kuchinjana tutakuwa kwa vigezo vya udini na itikadi za vyama, vita kama hizi ikitokea huwa haina kikomo.

Tatizo naloliona mimi ni uto-tayari wa ccm kujikuta wanakuwa chama cha upinzani 2015, ccm hawataki kuamini kwamba CDM inapedwa that much na watu, laiti kama CDM isingekuwa tishio hizi kesi na chokochoko zote zisingekuwapo, hili ni tatizo (janga) na hawa ccm wasipokubali kwamba kuna chama chenye nguvu kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii na kinapendwa na watu -- naapa watanzania vita hii yaja very soon. yeyote mwenye busara atakubaliana na mimi.
 
Join Date : 21st March 2013
Posts : 15
Rep Power : 304
Likes Received6
Likes Given1
 
Nasikitika kuwa Baba wa Taifa ni wako wewe na wengine kadhaa ila kuna wanaomuona ni MSALITI wa dini yao.

Usitegemee mtu akubali KITUMBUA chake kimtoke kirahisi. Atapigana hata kwa kuparua makucha.

Hebu angalia nyumba ya Spika na .......

303374087.JPG

bot2.jpg
NYUMBA+YA+GAVANA+WA+BOT.jpg
Nyumba ya Gavana wa BoT....
 
Back
Top Bottom