Hili wala siyo tatizo mbona...
Wewe nunua tivii yenye feature ya Picture in picture. Ukiwa nayo ya hivyo wewe unaweza ukaangalia vipindi vyako huku na wao wakijinafasi na akina Pink Panther au Popeye the sailor man na wote mkawa mko kwenye sofa mkiangalia.
Hahahahaaaaaaaaaaaa! kweli nimeamini ukiwa una maudhi ingia jf, utafurahi tu na kutoka roho kwatuuuuuuuuuuuu huku ukiwa umemsamehe kabisa alokuudhi, mweee!
Una DSTV ya kuchakachua wewe, hao waliokuwekea hiyo cable hawakukuambia,,, hiyo channel ya kiswahil ni Africa magic swahili,,, nimeshakumbana na hao jamaa wanataka wanifungie kwa Laki 4 na nitakuwa silipii tena sema masharti yake hakuna plan your view wala dstv touch kucheki timetable,,
Pia kuhusu msaada ni bora ujumuike na watoto wako sitting room ujue wanaangalia nini, na uwajengee kuwa uptodate kwa kuchek television zenye mafunzo like mindset learn, discovery etc,, kama sio mpenzi wa Bar usianze kwenda bar eti unakimbia wanao maana huko utakutana na ma Bar maid wapo kwenye mawindo na shepu zao za mchina wakakuchanganya hadi ukakosa muda wa kurudi nyumbani,,,
Kama mkeo mnashare common interest Jinunulien TV nyingine muweke room kwenu wakati madogo wanaenjoy cartoon, na we na wife mnacheki Room, yaani full happy family no bugudha,,,
nunua TV weka chumbani angalia kwa raha zako na wao wanajinafasi sebuleni
Kilichokufurahisha ni nini hapo Ndyoko? Nimetoa ushauri ambao siyo, au inakuwaje?
Spati picha ya hiyo tv, na hivi nilivyo na shida ya kuona mbali-hata umbali wa mita tano- hivyo nahisi kama ntakuwa napiga chabo mkuu. Wala hujaongea kitu kibaya mkuu.
NN brother umenikumbusha kitambo this cartoonsHili wala siyo tatizo mbona...
Wewe nunua tivii yenye feature ya Picture in picture. Ukiwa nayo ya hivyo wewe unaweza ukaangalia vipindi vyako huku na wao wakijinafasi na akina Pink Panther au Popeye the sailor man na wote mkawa mko kwenye sofa mkiangalia.
vp, mtu wangu! unaiharibu nyumba yako mwenyewe. weka ratiba ya kuangali TV kwa wanao. sio kila saaa. wazingatie kwanza masomo. kwani ni muda gani huo mnagombania remote na watoto? nikidhani wanaporudi shuleni jioni homework kwanza, kufanya matayarisho yao binafsi kwa ajili ya kesho na mengine madogo madogo. utakuta ule muda wa TV ni wakati wa kula tu. tena marufuku mtoto kuangalia TV baada ya saa nne, awe ni wa sekondari au msingi, wote kitandani na kwa wale wakubwa Study room. na wewe ni muda gani huo unao nyumbani wa TV? mipira sio kila siku na wala hizo program unazo sema sio kila siku. ili kuwatia displine weka ratiba kama baba. unachekesha kweli
NN brother umenikumbusha kitambo this cartoons
Uko wapi kwani? Tanzania? Tivii za hivyo hazijafika bongo kwani?
Uko wapi kwani? Tanzania? Tivii za hivyo hazijafika bongo kwani?
NN,Zshafika bwn,bongo c kama mbele tu nwdays!kila kitu unapata,tatizo huku uswazi wa2 watakuona eti unapendaga makuu.
Hili wala siyo tatizo mbona...
Wewe nunua tivii yenye feature ya Picture in picture. Ukiwa nayo ya hivyo wewe unaweza ukaangalia vipindi vyako huku na wao wakijinafasi na akina Pink Panther au Popeye the sailor man na wote mkawa mko kwenye sofa mkiangalia.
Kwa jinsi jamaa alivyocheka nikadhani labda wazo nililolipendekeza lilikuwa la ajabu sana.
Ukipata kitu plasma tena HD 1920x1080i chenye hiyo feature inakuwa mwake sana.
tatizo ukitumia hiyo picture in picture huwezi kusikiliza sauti ya moja, ni animations tu! sasa starehe inapungua inakua kama album ya mpira banaa! ila muhimu pia ni kulea watoto ambao sio selfish. aisee, vitoto vya siku hizi selfish hadi vikikutana na vyenzao kwenye play park anataka kuhodhi treni anasema ya kwake! unatamani kuzabua katoto ka watu ila mamake amenyamaza tu haongei kitu unatamani uhamie kwenye kuzabua mama mtu! kha!
Jamani hii kitu imekuwa inanisumbua kwa muda sasa ndani ya nyumba! Hivi karibuni nimefunga cable service kutoka kwenye kampuni moja hapa nnapoishi. Binafsi hawa jamaa wana channel nyingi za mpira, wanyama, cartoon, movies, yaani ni kama dstv kwa asilimia 100. Kwa bahati mbaya-kwangu- na nzuri kwa watoto, ni kwamba kuna channel moja ya movie za akina kanumba-namaanisha za kiswahili.
Kivumbi ni kwamba karibu watoto wote wanapenda kuangalia kama sio movie za kiswahili basi ni katuni. Yaani muda mwingi wamekuwa wakifanya hivyo, na wanaponiona mimi nakuja, utaona kabisa ni kama wanakosa raha maana wanajua, hapa Baba anakuja kubadili channel na kuweka kama sio channel ya mpira, basi ni discovery world au geographic channe, au animal planet au geographic wild, cnn, sky news au bbc. Hali hii nimeiona kwa muda mrefu sasa mpaka nimefika mahali nimeona kama naingilia uhuru wa members wengine wa familia, kwa maana nahisi wanaanza kuniona mimi kama mbinafsi vile. Imefika mahali sasa nimeamua kutokaa sebuleni, najifungia chumbani na kufanya kazi nyingine huku nikijua kuwa kuna mambo ya maana nayakosa lakini ntafayaje sasa watoto wenyewe wana mind wakiona nahamisha program wanazozipenda.
Kwa kuwa nimehisi huenda wanashindwa tu kusema, nami sijui nifanyeje maana kama kuna mpira au kuna issue ambayo ni 'educative' huwa najikuta nahamisha channel ili kuangalia hiyo progam bila kujali hiyo mipicha yao ya kina kanumba.
Hebu wakuu naombeni ushauri wenu, nifanyeje au nyie mnatumia njia gani, ili watoto waone kuwa na wewe kama mzazi unajali interest zao? Nakwazika, sasa kukosa mpira, kisa katoto ka chekechea kamekomalia remote kuangalia katuni/movie za kina kanumba wakati mie nataka nione Arsenal inavyochabangwa na kina Drogba. Nishaurini wakuu njia nzuri ipi nitumie ili watoto wasione kuwa Dingi Mnoko!
Nawasubiria!