Nafsi "ni wewe usiyeonekana" na ambaye unamiliki kila kitu cha "wewe unayeonekana" ikiwa ni pamoja na roho yako, ambayo ni pumzi ya uhai. Umbo lako kwa ujumla wake pamoja na roho yako vinamilikiwa na nafsi. Kwa mfano huwa wakati mwingine unasema, kichwa changu kinauma, mkono wangu, mguu wangu, ukiwa unamaanisha kuwa wewe siyo kichwa, wala mguu, wala mkono, isipokuwa wewe ni kiumbe unayemiliki vyote hivyo kwa ujumla wake, na mmiliki huyo ndiyo hiyo nafsi yako!