Nafasi za wanadamu zikisononeka, Mungu nae atakuchukia.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Vitabu vya Mungu husema Kama ukiona nafsi za wanadamu zinakulalamkikia na kusononeka kwa matendo yako, basi Mungu nae hukuchizwa na matendo yako kutokana na kusononeka kwa nafsi za wanadamu hao. Ndio maana wanadamu wamekuja ja ujumbe usemao "Malipo ni hapa hapo duniani"
 
Ni kweli kabisa mkuu.

Watanzania tulilia na kusononeka sana kuhusu CHADEMA na Mungu akatusikia kikaangukia pua uchaguzi uliopita.

Ahsante kwa kutukumbusha.
 
Anaelilia kilio cha haki mungu humsikiiza zaid,haya nyie mnalia kilio gan?kutumbuliwa au dili kua adimu town?
 
Shida y
Anaelilia kilio cha haki mungu humsikiiza zaid,haya nyie mnalia kilio gan?kutumbuliwa au dili kua adimu town?

Shida yenu uvccm akili yenu haina tofauti na akili ya mzee wenu wa katerero akili zenu zinawatosha nyinyi tu
 
Vitabu vya Mungu husema Kama ukiona nafsi za wanadamu zinakulalamkikia na kusononeka kwa matendo yako, basi Mungu nae hukuchizwa na matendo yako kutokana na kusononeka kwa nafsi za wanadamu hao. Ndio maana wanadamu wamekuja ja ujumbe usemao "Malipo ni hapa hapo duniani"
Kabisa mkuu.hata sodoma na gomora Mungu alichukizwa na zile ishu zao,yaani taifa zima alimtoa Rutu peke yake,hivyo tutafakari upya njia zetu si kila aliye kinyume na wengi ni adui wa Mungu.
 
Mpaka leo hii sinaamini kuwa utumbuaji uliofanywa ulikuwa na uhusiano na ufisadi. Hakuna ushahidi maana hakuna hata mmoja aliyepelekwa kwenye mahakama ya ufisadi.

Ninachojua ni kuwa nidhamu na maadili ya utendaji kazi katika ofisi za umma ulikuwa chini sana. Tulihitaji sana mtu wa kurudisha nidhamu na uadilifu katika utumishi wa umma. Katika eneo hilo kumekuwa na mchanganyiko, kumekuwepo na mafanikio lakini kumekuwepo na walakini pia. Mafanikio kiasi yaliyopatikana katika nidhamu ya utumishi umma yanastahili kupongezwa.

Uchumi wetu kwa miaka mingi umekuwa chini, na ukuaji wake haukuweza kuendana na ongezeko la watu na mahitaji yetu. Tulitegemea utawala mpya ukuze speed kwenye ukuaji wa uchumi. Kwa bahati mbaya kwenye hili tumerudi sana nyuma. Hakuna uwekezaji mpya na baadhi ya uwekezaji uliokuwepo unazidi kufa.

Kwenye demokrasia na utawala hatukuwa nyuma sana japo hatukuwa tumefikia viwango vya kukubalika lakini angalao tulikuwa kwenye hali ya kuvumilika. Kwenye eneo hili tumerudi nyuma sana. Upimaji wa eneo hili hupimwa katika uimara wa taasisi za kiutawala na zile zinazosimamia demokrasia. Hapa inatizamwa mifumo na siyo watu. Katika awamu hii mifumo na taasisi zimekufa badala yake wamebakia watu, mtu mmoja mmoja anatoa maagizo kwa namna yeye anavyohisi au anavyotaka. Hiyo ni kutoka chini mpaka juu. Ndiyo maana leo huyu anatangaza hiki kesho mwingine anatengua.

Kunapokosekana mfumo, ni rahisi sheria na haki za watu kuvunjwa. Kutakuwa pia na watu watakaoonewa. Kuna baadhi ya watu wametumbuliwa, ni watu waadilifu hasa ambao pamoja na utumishi wao wa umma kwa zaidi ya miaka 20 kwenye nafasi za juu hawana hata vitz kwa sababu ya kutokuwa tayari kudokoa kisicho chao lakini wametumbuliwa. Labda kama wanatumbuliwa kutokana na ufanisi mdogo lakini siyo ufisadi. Wanaonewa, sauti na majonzi yao Mungu huyasikia, na laani huliangukia Taifa zima, siyo lazima imwangukie mtumbuaji pekee maana na sisi tunashiriki kwa kushangilia. Na wengine tunafurahia kama wafanyakazi wote wa umma wangetumbuliwa ili au wafanane na sisi au wawe katika dhiki kutuzidi sisi!
 
Madikteta wote hawaamini kuwa hicho kinachoitwa Mungu kipo! Infact wao ni miungu watu! Sononekeni, lieni, ombolezeni, shauri yenu! Mtajiju!
 
Vitabu vya Mungu husema Kama ukiona nafsi za wanadamu zinakulalamkikia na kusononeka kwa matendo yako, basi Mungu nae hukuchizwa na matendo yako kutokana na kusononeka kwa nafsi za wanadamu hao. Ndio maana wanadamu wamekuja ja ujumbe usemao "Malipo ni hapa hapo duniani"
Ni kweli Mimi nili lalamika sana kuhusu Lowasa na wizi wake na kweli Mungu alijibu maombi yangu maana alikatwa CCM na akakatwa na watanzania na sasa ana randaranda kwenye saccos ya ufipa. Namshukuru sana Allah
 
Ni kweli kabisa mkuu.

Watanzania tulilia na kusononeka sana kuhusu CHADEMA na Mungu akatusikia kikaangukia pua uchaguzi uliopita.

Ahsante kwa kutukumbusha.
Nami namshukuru Mungu sana kwani hata DR SLAA amekikimbia kabisa
 
Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana ! Halafu kwenye hili wala hakuchelewa kujibu maombi ya wananchi .

Hakika Mungu ni mwema .
 
Shida y

Shida yenu uvccm akili yenu haina tofauti na akili ya mzee wenu wa katerero akili zenu zinawatosha nyinyi tu
Ugumu unakuja kuamin kua kila mtofauti mawe ni ccm,,,, usiegamie ppote ukitaka kujua mengi
 
Back
Top Bottom