Nafasi za kusomea elimu ya afya hewani tayari!!! Ingia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi za kusomea elimu ya afya hewani tayari!!! Ingia

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mmteule, Feb 21, 2012.

 1. m

  mmteule JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,004
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  WIZARA YA AFYA JANA TAREHE 20/2/2012 IMETOA TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO MBALI MBALI NGAZI


  Tangazo la kozi za Afya - 2012 Page 1
  JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA
  WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
  MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO 2012/13
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anakaribisha maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Afya kwa mwaka wa masomo 2012/2013.
  1. Kozi zinazotangazwa ni:
  A. Kozi za ngazi ya Stashahada:
  (i) Afisa Afya ya Mazingira (Health Officer)
  (ii) Fiziotherapia (Physiotherapy)
  (iii)Fundi Sanifu Meno (Dental Laboratory Technologist)
  (iv) Mteknolojia Maabara (Laboratory Technician)
  (v) Optometria (Optometry)
  (vi) Tabibu (Clinical Officer)
  (vii) Tabibu Meno (Dental Therapist)
  (viii) Uuguzi Daraja ‘’A’’ (Diploma in Nursing)
  B. Kozi za ngazi ya Cheti
  (i) Fundi Sanifu Maabara Msaidizi (Laboratory Assistants)
  (ii) Mtunza kumbukumbu za Afya (Health Record Technicians)
  (iii)Tabibu Msaidizi (Clinical Assistants)
  (iv) Uuguzi Daraja ‘’B’’ (Certificate in Nursing)
  C. Mafunzo ya Tabibu kwa njia ya masafa ‘Distance Learning)
  (i) Kozi ya Tabibu
  2. Muda wa Mafunzo:
  (i) Miaka mitatu (3)kwa kozi za Stashahada
  (ii) Miaka miwili (2) kwa kozi za Ngazi ya cheti
  3. Sifa za Muombaji:
  Waombaji watarajali (Pre-service):
  (i) Awe raia wa Tanzania
  (ii) Awe amemaliza kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2007 na kuendelea
  (iii)Ufaulu wa kidato cha nne uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’, kwa masomo ya biologia na kemia , na alama ‘D’ kwa somo la fizikia kwa kozi za Stashahada . Maksi hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mitihani.
  (iv) Cheti chake cha kidato cha nne, kionyeshe ufaulu usiopungua point 28 kwa kozi za cheti. Aidha ni lazima awe na ufaulu usiopungua (minimum) alama ‘D’, kwa masomo ya biologia, Kemia na Fizikia. Maksi hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mtihani.
  (v) Kwa wale waliomaliza kidato cha sita na wanaohitaji kujiunga na mafunzo ya stashahada, wawe na alama isiyopungua ‘E’, kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Ufaulu huu uwe umepatikana katika kikao kimoja tu cha mtihani.
  (vi) Kufaulu somo la Kiingereza na Hisabati ni sifa ya nyongeza.
  Waombaji wa wanaojiendeleza (In-service) kuchukua Mafunzo ya Tabibu kwa njia ya Masafa - Distance learning:
  (i) Awe amemaliza kidato cha nne
  (ii) Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya Waganga Wasaidizi Vijijini mwaka 1999 na kurudi nyuma.
  Tangazo la kozi za Afya - 2012 Page 2
  (iii)Awe na barua ya mwajiri wake
  Waombaji katika kipengele hiki watatakiwa kuchukuwa ‘Bridging course’ kwa miezi 9 na
  kufaulu, ndipo waweze kuendelea na masomo ya Tabibu.
  4. Utaratibu wa kutuma maombi:
  (i) Fomu za maombi zitapatikana kwa wakuu wa kanda za mafunzo zilizoainishwa hapo chini (rejea kipengele Na. viii) chini, waganga wakuu wa wilaya na wakuu wa vyuo vya afya vilivyo chini ya wizara.
  (ii) Waombaji wote watalipia fomu kwa sh. 15, 000/=. Risiti halisi ya Benki kwa ajili ya malipo haya, itawasilishwa pamoja na fomu za maombi. Kiasi hiki cha fedha hakitarejeshwa (Non refundable).
  (iii)Malipo yaingizwe kwenye akaunti ,‘Health Service fund’, Account No. 0111-030-12059 NBC – CORPORATE BRANCH.
  (iv) Maombi yatakayopokelewa na kufanyiwa kazi, ni yale yatakayoambatanishwa na risiti ya malipo ya Benki, inayoonyesha kiwango cha malipo kilichotajwa hapo juu.
  (v) Maombi ambayo hayataambatanishwa na hati ya malipo ya Benki(Pay in Slip) na kivuli cha cheti cha Baraza la Mitihani cha kuhitimu Elimu ya Sekondari, hayatafanyiwa kazi.
  (vi) Maombi yote yatapokelewa kupititia kanda za mafunzo baada ya malipo kufanyika kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu.
  (vii) Fomu za maombi zijazwe na zitumwe kwa wakuu wa kanda kulingana na eneo ambalo muombaji alipo. Kanda ya Mashariki itakuwa na sehemu tatu za kupokelea (No. a, i na j. Anwani za wakuu wa kanda ni kama zilivyoainishwa hapa chini:-
  a) Mratibu wa Kanda ya Mashariki (Mikoa ya morogoro na Pwani) - Chuo cha Mafunzo ya Afya ya Jamii – S.L.P. 1060, Morogoro - (EZ)
  b) Mratibu wa Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma na Tabora) – Chuo cha Tabibu Wasaidizi, S.L.P. 458, Kigoma - (WZ)
  c) Mratibu wa Kanda ya Kusini (Mikoa ya Lindi na Mtwara)– Chuo cha Tabibu, S.L.P. 86, Mtwara - (SZ)
  d) Mratibu wa Kanda ya Kaskazini (Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga)– Chuo cha Mafunzo ya Walimu wa Afya, S.L.P.1162, Arusha - (NZ)
  e) Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini Magharibi (Mikoa ya Rukwa na Mbeya) – Chuo cha Madaktari Waasaidizi, S.L.P. 1142, Mbeya - (SWHZ)
  f) Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mikoa ya Ruvuma na Iringa)– Chuo cha Afya ya Jamii, S.L.P. 235, Iringa - (SHZ)
  g) Mratibu wa Kanda ya Kati (Mikoa ya Singida na Dodoma) – Chuo cha Uuguzi, S.L.P. 595, Dodoma - (CZ)
  h) Mratibu wa Kanda ya Ziwa (Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga) – Chuo cha Madaktari Wasaidizi, S.L.P. 11351, Mwanza - (LZ)
  i) Mkurugenzi wa Taasisi za Sayansi Shiriki za Afya Muhimbili, S.L.P 65005, Dar-es-salaam - (EZI)
  j) Mkuu wa chuo cha Tabibu, S.L.P. 30082, Kibaha - (EZK)
  Mwombaji ajaze kwenye fomu ya benki kanda/chuo ambayo atapeleka fomu zake kwa kujaza herufi zilizo ndani ya mabano hapo juu, zilizoandikwa mwisho kabisa wa anuani ya kila kanda. Herufi hizo zijazwe upande wa kushoto wa fomu ya benki wakati mwombaji wanajaza mambo mengine kwenye fomu. Fomu zitapokelewa kwenye vyuo vilivyoainishwa hapo juu tu.
  5. Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:
  a) Wizara itakuwa na wajibu wa kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali kupitia magazeti, ‘website’ ya wizara na mbao za matangazo wizarani na Kanda za Mafunzo.
  b) Taarifa hizo zitatumwa pia kwenye kanda za mafunzo kama zilivyoainishwa hapo juu.
  6. Muda wa mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Aprili, 2012.
  7. Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 1 Oktoba, 2012.
  Imetolewa na:
  Katibu Mkuu,
  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
  S.L.P. 9083,
  Dar es Salaam.


  NAWASILISHA WAKUU KAMA NILIVYOAHIDI KUZIWEKA HAPA.
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,950
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  ahsante, hivi hakuna diploma za kozi za utabibu kwa masomo ya jioni tofauti na ufamasia?
   
 3. s

  sojak Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  poa mkuu,unaweza kunijuza pia ada kwa kila kozi ni ngapi kwa mwaka huu wa masomo.if possible
   
 4. Asu tz

  Asu tz JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  hv huyu dogo watamchukua yy amefaulu BIOS D na PHYS D anaweza kuchukuliwa kwel jaman msaada.
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mwache ajaribu anaweza akapata...kwani yy ana div ya point gani?
   
 6. Asu tz

  Asu tz JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Yy ana point 32.
   
 7. Bongoclever

  Bongoclever Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jamani matokeo ya waliotuma haya maombi wizara ya afya(2012/2013) mbona yamechelewa sana?
   
 8. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Watu wanasubiri majibu kwa waliomba mbona kuna thread humu wanauliza matokeo lini!kila la kheri maana wale wote mnaotarajia maisha mapya ya chuo.
   
 9. Ben40

  Ben40 Senior Member

  #9
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 195
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Da kweli majibu yamechelewa hv yntoka lini?
   
 10. g

  george daudi Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa taarifa zao walisema tarehe 04/10/2012 lakin mpaka sasa hakuna hivi ni kwa nini wanakuwa watu ambao hawana msimamo?
   
 11. Maayo

  Maayo JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Me ndo nchoka kabisa
   
 12. g

  george daudi Member

  #12
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  je!lin yanatoka rasmi haya majina ya wanafunzi waliochaguliwa vyuo vya afya kwa mwaka 2012/2013?mmake hata maandalizi watafanya muda gani?kama yamechelewa namna hii?...tupen tarehe...
   
 13. J

  John waryoba Member

  #13
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuanzia jumatatu
   
 14. S

  SIR GIVE Member

  #14
  Oct 9, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa hayo maselection lini yanatoka bana maana ziwezi kuita selection coz umekua uduanzi
   
 15. J

  Jerry frank New Member

  #15
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  j3 ndo inapita iyo bila matokeo,sasa tutasubiri hadi lini?
   
 16. G

  Geofrey J Member

  #16
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasemekana dis wiki
   
 17. double click

  double click JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  jaman mlioko Dar mkutane wizaran
  kwan c mnajua viongoz wt
  walikwsha zoea kusukumwa
   
 18. S

  Spenderjak Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama vip warudshe pesa ze2
   
 19. T

  Tawfique New Member

  #19
  Nov 13, 2013
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  majina ya second selection teyari.....!? wizara ya afya kwa diplo na certificate
   
 20. pemgtoonet.com

  pemgtoonet.com JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2013
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 336
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  pumba tupu. Tangazo la mwaka jana.
   
Loading...