karibukwetusingida
JF-Expert Member
- Mar 10, 2014
- 290
- 137
Tangazo kwa Umma: nafasi za kazi kwa mafundi
sanifu wa maabara za shule (school laboratory
technicians)
Serikali inatarajia kuajiri Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule
Daraja la II. Ajira hii ni kwa Fundi Sanifu wa Maabara ya
Shule waliohitimu kati ya mwaka 2013 - 2015.
Hivyo, wenye sifa stahiki na wanaotaka kuajiriwa Serikalini,
wanatangaziwa kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya:
Elimu ya Sekondari (Kidato cha nne na / au Sita);
Taaluma ya Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule na
Cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya uhakiki.
Aidha, mwombaji aambatishe nakala ya wasifu binafsi (CV)
ya Elimu, Taaluma na Uzoefu. Mwombaji aainishe majina
yake matatu kwa kirefu na usahihi.
Mwombaji ambaye katika vyeti vyake vya Elimu na Taaluma
havina jina la tatu, akamilishe taratibu za kisheria kuongeza
jina la tatu na kuwasilisha kiapo stahiki pamoja na maombi
yake.
Nyaraka zote ziwasilishwe kwa barua pepe ifuatayo:
apa@moe.go.tz
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na cheti cha Kidato cha IV au Kidato cha VI
katika masomo ya Sayansi na waliofuzu Mafunzo ya
Laboratory Technology au Laboratory Science and Technology
katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na kupata
Stashahada (National Technical Awards [NTA] Level VI) au
Full Technician Certificate.
KAZI ZA KUFANYA
i. Kutayarisha vitendea kazi vya maabara ya somo la Sayansi
kwa vitendo.
i. Kusaidiana na mwalimu wa somo katika kuandaa masomo ya
sayansi kwa vitendo.
ii. Kupokea na kutunza vifaa na madawa kwa ajili ya maabara
ya shule.
v. Kubaini mahitaji ya vifaa na madawa kwa ajili ya maabara
ya shule.
v. Kufanya majaribio ya awali (Pre-Test) kabla ya majaribio
(Practical) kufanyika na wanafunzi kwa mazoezi na mitihani
ya ndani.
i. Kutunza vitendea kazi na kuhakikisha usafi wa maabara
kabla na baada ya mazoezi ya mitihani na majaribio ya
ndani.
i. Kusimamia usalama wa maabara na waliomo wakati wa
mazoezi ya vitendo (Practicals) kwa kuhakikisha kuwepo
vizimamoto (Fire Extinguisher).
i. Kutunza vifaa vya usalama na huduma ya kwanza kwenye
vyumba vya maabara.
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI NI KAMA IFUATAVYO:-
. Mwombaji anatakiwa ‘ku-scan’ vyeti / nyaraka halisi na
siyo kivuli (photocopy) na kuhifadhi katika ‘file’ moja la
‘pdf’. ‘File’ lipewe majina matatu ya mwombaji kuanzia la
kwanza, kati na la mwisho ndipo litumwe.
. Mwombaji atumie anuani ya barua pepe yake mwenyewe na
siyo ya mtu mwingine kutuma nyaraka zake.
TANBIHI:
. Tarehe ya mwisho kupokea nyaraka ni 20 Februari, 2017.
. Yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa
katika ajira
. Barua pepe za kuwasilisha nyaraka za waombaji zitumwe
mara moja tu na si kwa kurudia rudia ili kuepuka usumbufu.
IMETOLEWA NA
Tarishi M.K.
KATIBU MKUU
30 Januari 2017
source:website wizara ya elimu