wajasiriamali wote wanafanya kazi bila mshahara kwa hata miaka mitano. Sasa wewe bila kutaka kujua undani wa nilichoongea unatoa "judgement"
tatizo akili yako inaamini bila kuajiriwa huwezi kufanikiwa. Kwa ushauri kwako na kwa fluid tafuteni kitabu kinachoitwa "rich daddy poor daddy by Robert Kiyosaki" utaelewa ninachosema
kuendelea kufikiria hivyo ndiyo sababu vijana wa kitanzania wenye mtazamo kama wako wamebaki wakitembeza "application kila ofisi bila mafanikio. Unaweza ukafanya kazi bila malipo si kwa sabau wewe ni fisadi ila kwa sababu unatafuta "practical expirience" na "practical skills" na hii imenisaidia na pia watu mengine nimewashauri wamefanya "volunteering" zaidi ya mwaka na sasa wanaajira zao. Na nikuambie kuwa wanaofanya kazi kwa kuangalia mshahara ni watumwa wa kazi.(utafanya kazi x utaona mshahara hautoshi utaomba kazi y, utaona kama mshahara na majukumu haviendani utaamua kwenda kusoma ili upande cheo na mshahara, ukimaliza utaona kama elimu yako na uzoefu wako havistahili huo mshahara utahama ofisi kwenda ofisi yenye mshahara mkubwa zaidi. Yatakuwa ndo maisha yako yote hadi kufa. (kwani wewe huoni vijana wenzenu wanavyohama ofisi hadi ofisi wakitafuta mshahara na sio kazi)