Mkuu Tunaomba utupe trusted source coz hii inaonekana Kama editing ya kitu hii hapa chini
Said
WIZARA YA Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto,
imetangaza nafasi za ajira
192 kwa dharura, kwa
wataalamu wa fani mbili
za afya ambazo ni Tabibu
wasaidizi (Clinical
Assistant), nafasi 95 na
Wauguzi (Enrolled Nurses)
nafasi 97.
Kwa mujibu wa taarifa ya
Wizara hiyo iliyotolewa leo
Jumatatu Mei 23, 2016 na
kusainiwa na Katibu Mkuu
wa wizara, Iimeeleza kuwa
Wizara imeridhia mpango
wa ajira ya dharura ili
kukabiliana na uhaba
mkubwa wa wafanyakazi
katika sekta hii. “Mpango
huu utaendeshwa kwa
Fedha za mfuko wa CDC
(Centre for Disease Control)
Awards No.
5U2GGH001062-03 kwa
mwaka wa Fedha ulioanzia
Aprili 2016 kwa muda wa
miaka miwili. “Taarifa hiyo
imefafanua.
Watumishi watakaopata
ajira kupitia mradi huu
watapangiwa vituo vya
kazi vilivyoko katika
maeneo yenye uhaba
mkubwa wa watumishi
husika na ambayo
mazingira yake ni
magumu, taarifa hiyo
imeendelea kusema.
Taarifa hiyo ya wizara
imeendelea kufafanua
kuwa watumishi hawa
baada ya kumaliza
mkataba wao, wataingizwa
katika ajira za serikali
kulingana na upatikanaji
wa vibali vya ajira kwa
mwaka husika.
Wizara imewataka wote
wenye nia ya kuomba
watume maombi yao
yakiwa yameambatanishwa
navivuli vya vyeti vya
kumaliza kidato cha nne,
cheti cha taaluma pamoja
na leseni, (kwa wauguzi)
Taarifa kamili soma hapo
chini
JAMHURI YA MUUNGANO YA
TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO
YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA
WATOTO
AJIRA YA DHARURA KATIKA
SEKTA YA AFYA
UTANGULIZI
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeridhia mpango wa Ajira ya
dharura kwa wataalamu wa
fani mbili za afya. Mradi huu
umelenga kuchangia juhudi za
serikali katika kukabiliana na
uhaba mkubwa wa
wafanyakazi katika sekta hii.
Mpango huu utaendeshwa kwa
Fedha za mfuko wa CDC
(Centre for Disease Control)
Awards No. 5U2GGH001062-03
kwa mwaka wa Fedha ulioanzia
Aprili 2016 kwa muda wa
miaka miwili. Watumishi
watakaopata ajira kupitia mradi
huu wanakadiriwa kuwa 192 na
watapangiwa vituo vya kazi
vilivyoko katika maeneo yenye
uhaba mkubwa na ambayo
mazingira yake ni magumu.
Watumishi hawa baada ya
kumaliza mkataba wao,
wataingizwa katika ajira za
serikali kulingana na
upatikanaji wa vibali vya ajira
kwa mwaka husika. Watumishi
hawa ni kama ifuatavyo:
Tabibu Wasaidizi (Clinical
Assistant) 95 na Wauguzi
(Enrolled Nurses) 97. Maombi
yote yaambatanishwe kivuli cha
cheti cha kumaliza kidato cha
nne, cheti cha taaluma pamoja
na leseni (kwa wauguzi)
MSHAHARA NA MASILAHI
Mshahara (kwa kiwango cha
juu cha mshahara wa kila fani
husika)
Posho ya kujikimu ya siku saba
za mwanzo
Bima ya Afya ya asilimia 3%
Kiinua m,gongo cha asilimia
25% ya mishahara baada ya
miaka (2);
Malipo ya pango ya asilimia
30% ya mshahara
Nafasi ya kupatiwa mafunzo
elekezi.
Mwisho wa kupokea maombi ni
tarehe 06/06/2016, Maombi yote
yatumwe kwa njia ya posta:-
Katibu Mkuu
Wizara ya afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
S.L.P 9083
6 Samora Machel Avenue,
11478
Dar es salaam, Tanzania