Nafasi za Kazi Gazeti la JAMHURI

Balile

Member
Oct 10, 2011
74
140
TANGAZO:

Kampuni ya Jamhuri Media Limited wachapishaji wa Gazeti la Uchunguzi la JAMHURI inatangaza nafasi 2 za kazi ya uandishi wa Habari.

SIFA:

Mwombaji awe na Shahada ya Kwanza ya Uandishi wa Habari au Mawasiliano ya Umma.

Mwombaji awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika kwa ufasaha Kiswahili na Kiingereza.

Awe amehitimu chuo kinachotambulika si zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Awe tayari kusoma nyaraka za uchunguzi na kuandaa Mpango Kazi wa kuchunguza, kuchakata na hatimaye kuchapisha Habari.

Tuma nakala ya CV yako na habari ya mfano kwenda jamhurigazeti@yahoo.com.

Watakaofikia vigezo ndiyo pekee watakaojibiwa na kuitwa kwenye usahili. Usipige simu bali tuma email kama ilivyoelekezwa.

Mshahara ni maelewano kwa mujibu wa viwango vya kitaifa.

Mwisho wa kupokea maombi ni Mei 24, 2016.

Deodatus Balile,
Mhariri Mtendaji,
Jamhuri Media Limited
 
Mkuu naamini mtapata mwandishi mwenye ueledi ili muendeleze uzalendo wenu kufichua uozo na majipu.Wito kwa watakaoomba fursa hiyo waisaidie nchi hii na sio ukanjanja.
 
Mkuu naamini mtapata mwandishi mwenye ueledi ili muendeleze uzalendo wenu kufichua uozo na majipu.Wito kwa watakaoomba fursa hiyo waisaidie nchi hii na sio ukanjanja.
changamkia iyo fursa badala ya kukaa na kushindilia ugal wa bure ikul na lumumba
 
atimae nafasi niliyoenda kuimba jamhuri wakati linaanza nikaambiwa kuwa nafasi hakuna ndo imetoka leo, sikati tamaa, ntaomba tena maana kipindi kile wara nafasi zilikuwa hazijatangazwa.
 
i

atimae nafasi niliyoenda kuimba jamhuri wakati linaanza nikaambiwa kuwa nafasi hakuna ndo imetoka leo, sikati tamaa, ntaomba tena maana kipindi kile wara nafasi zilikuwa hazijatangazwa.
i mean kuomba!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom