NAFASI ZA J.K.T

Samjela Jr

Member
May 23, 2017
51
95
Wadau naombeni msaada wenu kwa wale walio na experience tuu.....
maana kunawatu wanapenda kukatisha watumoyo afu kumbe awajui chochote kile.....
KWASISI VIJANA TUNAO HITAJI NAFASI ZA KUJITOLEO HUKO J.K.T
sehemu ngumu zaidi ni ipi...
1:WILAYANI
2:MKOANI.....??
Na tatizo kubwa linakuwa wap......???
 
psagala1

Senior Member
Feb 18, 2014
146
225
J.K.T haiangalii mahali mkuu mafunzo ni yaleyale ukiwa mkoani ama wilayani hafu huwezi ukataka ulaini kwenye jeshi.....fungua moyo tu harafu kila kitu kitaenda sawa hiyo ndiyo kanuni yakwanza ya J.K.T
 
Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
3,946
2,000
Japo sijaelewa swali lako vema, ila imenibidi tu nitumie akiliza ziada. Kwamba, mafunzo ya JKT hufanyikia kambini na wala hakuna cha mambo ya wilaya ama Mkoa.

Naamini unazungumzia Swala la kupata nafasi ya kujitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Kwanza, tambua kuwa nafasi za JKT hutumwa kwa Wakuu wa Mikoa tu. Barua zinazoanisha idadi pamoja na vigezo vya kujiunga hutumwa kwa Wakuu wa Mikoa. Ndipo Wakuu wa Mikoa hutoa Tangazo kwa Wakuu wa wilaya, nao hutoa taarifa kwa Kata na hata Vijiji.

Baada ya hapo Usahili huanzia ngazi ya wilaya kisha walioweza kupita ngazi hiyo hufanyiwa usahili huo ngazi ya Mkoa kupata idadi ya Vijana wanaotakiwa kutoka katika Mkoa tajwa. Hii huambatana na upimwaji wa afya na kadhalika. Kumbuka, idadi hutofautiana kutoka Mkoa mmoja na mwingine.

Hivyo nahitimisha kwa kusema kuwa, Ugumu wa kupata nafasi upo kotekote hasa Mkoani. Hii ni kwa sababu, mnakutana wote wenye vigezo, lakini watahitajika watakaokidhi vigezo kwa ubora zaidi.

Kama nimeelewa swali lako vibaya, tafadhali nikumbushe.
 
Nashukuru sana mkuu tena sana kwa maelezo yako kwa kina
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom