Habari. Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu cha Dar es Salaam. Nasoma education (biology na geography). Kwa semester hii ya mwisho nina muda wa ziada wa kutosha. Hivyo nachukua fulsa hii kuomba nafasi ya kuwa mwalimu wa ziada kwa shule yoyote ya sekondari iliyopo hapa Dar es Salaam (ikiwa ni shule binafsi ama ya serikali). Muda ambao ninakuwa huru kufanya kazi ni kama ifuatavyo:- jumatatu ni kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa sita mchana. Jumanne ni kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa nane mchana. Jumatano ni kuanzia saa tano asubuhi mpaka saa kumi jioni. Alhamisi ni kuanzia saa tano asubuhi mpaka saa kumi jioni. Ijumaa ni kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa kumi jioni. Kwa yeyote anayefahamu shule inyohitaji mwalimu naomba msaada tafadhari. Mawasiliano: 0766218969, email : mbatianis39@gmail.com. AHSANTENI.