Nafasi ya Mtandao Kwenye mabadiliko ya katiba

Math2009

Member
Oct 24, 2008
15
1
Jamani anayejua link ya website ambayo ninaweza kupata katiba ya Tanzania nitashukuru,itakuwa ni vizuri kama tutaituma jamii forums kuijadili katiba,hasa wale walio nje ya nchi kutumia mtandao kutoa maoni juu ya vipengele vilivyomo kwenye katiba,kama unajua kipengele chochote kwenye katiba ambacho unaamini kinaleta utata au kiondolewe, anika wazi watu tutoe maoni yetu,ila tatizo linakuja ni jinsi gani mawazo haya yaweze kuunganishwa na mawazo ya watanzania wengine na kufanyiwa kazi,labda sijui serikali iunde kitengo kitakacho chunguza maoni ya watanzania wanaotoa kwenye mitandao kuhusu mabadiliko ya katiba inaweza saidia,kwasababu sidhani kila mtanzania anaweza kuhudhuria kwenye hiyo midahalo maalumu inayoandaliwa na hao wateule wa rais wa kuchukua maoni ya katiba,lakini asilimia kubwa ya watanzania siku hizi wana wanaunganishwa na mtandao, ni njia mojawapo nzuri sana ya kupata kila wazo la mtanzania kuhusu swala hili nyeti la katiba.
 
Back
Top Bottom