Nafasi ya Mkurugenzi Mkuu NSSF moto

MZK

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
236
306
Nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) inaonekana kuwa moto baada ya mfuko huo kumaliza siku ya 22 bila ya kuwa na mbadala wa Dk Ramadhan Dau au kaimu wake.

Jaribio la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama kuziba nafasi hiyo kwa muda lilidumu kwa saa tano tu baada ya kulazimika kutengua uteuzi wa Carina Wangwe Alhamisi iliyopita.

Waziri Mhagama alilazimika kutengua uteuzi huo kwa maelezo kuwa taratibu zilikosewa huku Balozi Ombeni Sefue akieleza kuwa mkurugenzi huyo wa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Jamii (SSRA) alitakiwa kuwa msimamizi tu na si kaimu mkurugenzi.

Jana, juhudi za gazeti hili kutaka kujua maendeleo ya uteuzi wa mtu mpya wa kushika nafasi hiyo ziligonga mwamba.

Balozi Sefue, ambaye hadi jana alasiri alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi, hakutaka kuzungumzia suala hilo akimuelekeza mwandishi kumtafuta Waziri Mhagama.

Lakini Waziri Mhagama hakuweza kupatikana licha ya kutafutwa mara kadhaa. Juhudi za kumpata kwa simu zilishindikana kwa kuwa hakuwa akipokea na hata alipotumiwa ujumbe hakujibu.

Pamoja na kuteuliwa kuwa balozi ambaye atapangiwa kituo baadaye, Dk Dau aliondoka NSSF kwa njia ambayo imewaacha wengi wakiwa midomo wazi.

Akiongoza kikao cha viongozi wa mikoa wa NSSF jijini Dar es Salaam, Dk Dau aliletewa taarifa kuwa alikuwa akihitajiwa na mtu muhimu na hivyo kulazimika kumuachia kikao mmoja wa wakurugenzi wake, kwa mujibu wa habari ambazo Mwananchi imezipata.

Dk Dau hakurejea tena kikaoni na baadaye habari zikitangazwa kutoka Ikulu kuwa ameteuliwa kuwa balozi pamoja na Asha Rose Migiro na Mathias Chikawe.

Habari zinasema kuwa wiki iliyofuata, Dk Dau alianza kuonekana ofisini kabla ya kutaarifiwa kuwa uteuzi wake ulianza mara moja hivyo aachane na kazi za NSSF.

Kutokana na mazingira ya kuondoka kwake, hakuna mtu anayekaimu nafasi yake kati ya wakurugenzi nane walio chini ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.

Habari zinasema kuwa mazingira hayo yamesababisha kuzorota kwa shughuli za shirika hilo kubwa kuliko yote yanayojihusisha na hifadhi ya jamii.

Miongoni mwa mambo hayo ni ufunguzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam ambalo lilitakiwa lianze rasmi kutumika Machi Mosi, ununuzi wa magari ya ofisi za mikoa, mkutano wa wanachama wa mwaka pamoja na wiki ya NSSF ambayo hujumuisha mambo mbalimbali, kama shughuli za kijamii, maonyesho ya huduma za NSSF na michezo.

Wiki iliyopita Balozi Sefue alisema maswali kuhusu uteuzi wa kaimu yaelekezwe kwa Mhagama, ambaye alieleza wakati huo kuwa utaratibu wa kumpata kaimu ulikuwa unaendelea.

Kwa mujibu wa ripoti ya fedha ya mwaka 2011, shirika hilo lilikuwa na wanachama 501, 218, kati yao wafanyakazi waliosajiliwa waliongezeka kutoka 17,666 hadi 18,779, sawa na ongezeko la asilimia 6, huku michango ikiongezeka kutoka Sh300.08 bilioni hadi Sh356.5 bilioni kwa mwaka, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.8.

Kwa mujibu wa muundo wa uongozi wa NSSF, Mkurugenzi Mkuu ndiye kiongozi mkuu wa shirika akiwa na wakurugenzi nane chini yake.

Wakurugenzi hao wanahusika na uendeshaji (DO); utawala na rasilimali watu (DHRA); mipango, uwekezaji na miradi (DPIP); fedha (DF); teknohama (DIT); ukaguzi wa ndani (DIA); uthibiti na usalama wa mali (DARM) na huduma za kisheria (DLS).

Dk Dau, ambaye amebobea katika taaluma ya masoko, ameliongoza shirika hilo kwa miaka 15, tangu mwaka 2001 alipoteuliwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

Source: Gazeti Mwananchi
 
Ngoja tuone nani atavaa viatu vyake, naona wanabwelabwela tuuu mara mganda
 
Sure kbs toka 2001 Wakati wa Benjamin Mkapa, Dk Dau ameiongoza NSSF kwa ufanisi sana ndo mana amedumu ktk awamu Tatu za vipindi vya Urais, ingependeza sana kama JPM angetengua uamuzi wake amrudishe aendelee kulinda pesa zetu pale NSSF
 
Sure kbs toka 2001 Wakati wa Benjamin Mkapa, Dk Dau ameiongoza NSSF kwa ufanisi sana ndo mana amedumu ktk awamu Tatu za vipindi vya Urais, ingependeza sana kama JPM angetengua uamuzi wake amrudishe aendelee kulinda pesa zetu pale NSSF
Sema aendelee kutuibia, kwani amejitajirisha sana kwa pesa yetu kama rais anataka tumuamini katika vita ya ufisadi , aamuru takukuru wamchunguze mali anazomiliki yeye na familia yake waone kama zinalingana na kipato chake halisi
 
Binafsi hua naonaga kama kuyaongoza mashirika haya ya hifadhi ya JAMII na TRA ni rahisi sana, tofauti kabisa na mashirika kama Tanesco, TTCL, ATCL nk. Mashirika haya ya hifadhi ya JAMII na TRA ni kwamba wateja wake wanakuja wenyewe tena kwa lazima, wasipokuja unawashtaki kwenye vyombo husika. Mashirika haya ya hifadhi ya Jamii kwanza yapo machache na kwa sharia ya zamani (nadhani kabla mwaka 2004) ilikua sekta zote zisizo za Umaa wafanyakazi wake wote walitakiwa kua member wa NSSF so wala hukutakiwa kutumia akili kubwa sanaa kuliongoza shirika kama haya, kwangu mm nadhani hajapatikana mrithi wa Dau si kwasabau ya uwezo but mtu wanaye mtaka.
 
atakuja tu siku si nyingi ila si DAU tena yeye sasa ni balozi ,mabalozi wanarudishwa sasa
 
Ni bora wakajiridhisha na kujipa muda wa kutosha kupata mtu mwingine kuliko kukurupuka na kuweka mtu asiyefaa. Dr Dau zama zake zimepita na kitabu chake kimefungwa tungoje mtu mwingine. Ila kama taifa tungetendewa haki nafasi hizi zingekuwa zinatangazwa na watu wanaomba na kufanyiwa usaili objectively, kuliko hivi kupeana peana tu
 
Hakuna wa kuziba nafasi ya dr dau.walikurupuka kumuondoa ndo mana wanatapatapa kumtafuta kaimu na bado hajapatikana.
1457336238682.jpg
1457336238682.jpg


Ukisoma hii habari ukataka kujua ukweli wake basi utamchukia dau milele
 
Nyadhifa kama hii hateuliwa mtu kwa kukurupuka shirika linahitaji mtu makini tena ingefaa watu wange shindanishwa kupitia usaili, lakini ninakataa pia kama dk dau ndo alikuwa anastahili kuendelea, maana amehujumu shirika kwa mambo mengi sana pia swala la udini alilipa kipaumbele sana shirika limejaa Waislamu na pia mkristo akikosea analimwa barua ya kuwa suspended tofauti na Waislamu.
Kaka acha kusingizia udini angalia uwiano wa dini mbili katika wakurugenzi 8 waliokuwa chini ya dr dau.
 
Hakuna wa kuziba nafasi ya dr dau.walikurupuka kumuondoa ndo mana wanatapatapa kumtafuta kaimu na bado hajapatikana.
Acha ulongo mkuu, watu karibu milion hamsin hamna mwenye uwezo kama au zaid ya dau?

Unajua taaluma yangu kwa mfano? Subir nitangazwe nitarudi.
 
DO- Chriss Magori

DPIP -Y KIDULA

DF - L MROSSO

DHRA- C MATESSA

DIT- I HALFAN

DLS- A KAGOMBA

DIA- P MTUNDA

DARM- S SHEMLIWA
Mkuu MZK, Je udini hapo ni dini gani inaongoza? Watanzania ni wabinafsi sana!
 
DO- Chriss Magori

DPIP -Y KIDULA

DF - L MROSSO

DHRA- C MATESSA

DIT- I HALFAN

DLS- A KAGOMBA

DIA- P MTUNDA

DARM- S SHEMLIWA
FUKUZA WOTE, KUANZA UPYA SI UJINGA ----Mrisho Mpoto
 
Sema aendelee kutuibia, kwani amejitajirisha sana kwa pesa yetu kama rais anataka tumuamini katika vita ya ufisadi , aamuru takukuru wamchunguze mali anazomiliki yeye na familia yake waone kama zinalingana na kipato chake halisi
kwani alikua anapokea laki ngapi vile.?
 
rip NSSF,baada ya mradi wa daraja sasa watarudi kutengeza makalavati,maana walaji wanalitolea udenda shirika
 
Kitu ambacho sikikubali ni kuwa hakuna mtu anayeweza kuziba nafasi yake. Ikibidi tuajiri expetriate tufanye hivyo kuliko kuendelekeza uKurunzinza
 
Kaka acha kusingizia udini angalia uwiano wa dini mbili katika wakurugenzi 8 waliokuwa chini ya dr dau.
Hivi unajua bodi iliyo kuwa chini ya dau ilikuwa na Waislamu wengi kwa idadi kijana,na kipindi sio kirefu hiyo bodi ilivunjwa na serikali baada kuona utendaje wake na vikao vyao vilikuwa na siri nzito na udini ndani yake.Kuna nambo yapo nyuma ya pazia nssf yalikuwa yanaratibiwa na dk dau kwa usiri.
 
Back
Top Bottom