Nafasi ya Makamu wa kwanza wa Raisi inaweza isijazwe,mawaziri je?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,858
Katika kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa,nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Raisi inaweza isijazwe na mambo yakaendelea bila kuwa na kikwazo chochote kikatiba.

Lakini je,Raisi wa Zanzibar ataweza kuunda serikali hiyo bila ya kuwa na mawaziri kutoka chama/vyama vya upinzani?

Na je,mtu anaweza kuteuliwa kuwa waziri bila kwanza kuwa mwakilishi?

Kwakuwa Wawaikilishi wote ni kutoka CCM,je hii si sababu tosha ya kikatiba kusema Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ndio imefikia mwisho wake?

Au je,Raisi wa Zanzibar anaweza kuteua mtu kutoka upinzani na kisha kumpa uwaziri na ikawa sahihi kikatiba?

Swali la mwisho na pengine gumu zaidi ni je,Rais anaweza kuunda serikali ya chama kimoja bila kwanza katiba ya Zanzibar kufanyiwa mabadiliko?

Na je,mabadiliko hayo Wazanzibari hasa kutoka Pemba watayaridhia katika kura ya maoni?

Majibu ya maswali haya tutayapata ndani ya siku 7 tangu shein apiishwe.
 
SUK ipo kikatiba, na ili kumpata makamo wa kwanza ilibidi atoke chama kilichofikisha asilimia 10%, hakuna, hivyo sasa hakuna makamo wa kwanza. Mawaziri walibidi kutoka wawakilishi, ambao wote ni CCM!.

Pasco
 
Kama mawaziri ni lazima wawe Wawakilishi na Wawakilishi wote ni kutoka CCM,sasa utaweza kuunda hiyo serikali ya Umoja wa Kitaifa(SUK)?
 
Kufikisha 10% sio kigezo pekee

Kama hakuna 10% inaangaliwa idadi ya wawakilishi.

Kama hakuna chama kingine chenye wawakilishi, basi Rais halazimiki kushirikisha mtu mwingine kwenye maamuzi ya uundwaji wa serikali. Kwahiyo ataunda SUK kwa kutumia busara zake.
 
Haramu huzaa haramu,Rais amepatikana kwa njia za haramu,unategemea nini.
zanzibar.jpg
 
..tatizo linaweza kuwa kwa wale wawakilishi ambao walishapewa vyeti vya ushindi.

..pia kunaweza kuwa na tatizo lingine kuhusu matokeo ambayo Maalim tayari anayo na yalishathibitishwa lakini yalikuwa bado kutangazwa.

..hili suala linaweza kuleta mgogoro wa kikatiba. sidhani kama limekwisha kwa Shein kutangazwa mshindi.
 
Kufikisha 10% sio kigezo pekee

Kama hakuna 10% inaangaliwa idadi ya wawakilishi.

Kama hakuna chama kingine chenye wawakilishi, basi Rais halazimiki kushirikisha mtu mwingine kwenye maamuzi ya uundwaji wa serikali. Kwahiyo ataunda SUK kwa kutumia busara zake.
Anaunda kwa busara zake au kwa kufuata Katiba?Kuna kipengele cha Katiba kinachomruhusu kuamua kuunda SUK kwa kadri anavyoona inafaa?
 
Anafuata katiba.

Katiba ndiyo inayomruhusu kuunda SUK. Ila katiba inamwambis iwapo kuna chama kina 10% ya kura za Rais basi lazima akishirikishe kwenye kuamua nani awe makamu. Makamu sio lazima awe yule aliyegombea Urais.

Kama hakuna mwenye 10%, katiba inamwambia lazima ashirikishe chama chenye wawakilishi wengi zaidi among opposition. Again sio lazima anayeteuliwa awe aliyegombea.

Kama hakuna 10% na hakuna chama kingine chenye wawakilishi, basi Rais halazimiki kuhusisha chama kingine. Kwahiyo anatumia busara zake kuunda SUK.
 
Kama mawaziri ni lazima wawe Wawakilishi na Wawakilishi wote ni kutoka CCM,sasa utaweza kuunda hiyo serikali ya Umoja wa Kitaifa(SUK)?
SUK inatokea endapo mgombea alieshika nafas ya pili amefikisha walau 10% ya kura zote Kama hayupo aliefikisha basi automatically SUK haipo
 
Kitu kikubwa kwa CCM kilikuwa kufuta uchaguzi ambao Seif alishinda na kutangaza uchaguzi mwingine hilo ndilo jambo gumu walilokutana nalo,hivyo vingine vya makamo wa kwanza sijui mawaziri ni vitu vyepesi sana kwao.

Kuwa na subra utaona serikali yao muda si mrefu na atakayeleta fyoko fyoko watamdhibiti.
 
New Somalia in the offing somewhere in the same continent!
 
Salary, suppose anaamua kuchagua mawaziri wote wa ccm mtamfanya nini. Mbona Jecha na kelele zote kafanya kama hivyo. Mtamfanya nini akiamua anavyotaka bila kufuata katiba
 
Katika kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa,nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Raisi inaweza isijazwe na mambo yakaendelea bila kuwa na kikwazo chochote kikatiba.

Lakini je,Raisi wa Zanzibar ataweza kuunda serikali hiyo bila ya kuwa na mawaziri kutoka chama/vyama vya upinzani?

Na je,mtu anaweza kuteuliwa kuwa waziri bila kwanza kuwa mwakilishi?

Kwakuwa Wawaikilishi wote ni kutoka CCM,je hii si sababu tosha ya kikatiba kusema Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ndio imefikia mwisho wake?

Au je,Raisi wa Zanzibar anaweza kuteua mtu kutoka upinzani na kisha kumpa uwaziri na ikawa sahihi kikatiba?

Swali la mwisho na pengine gumu zaidi ni je,Rais anaweza kuunda serikali ya chama kimoja bila kwanza katiba ya Zanzibar kufanyiwa mabadiliko?

Na je,mabadiliko hayo Wazanzibari hasa kutoka Pemba watayaridhia katika kura ya maoni?

Majibu ya maswali haya tutayapata ndani ya siku 7 tangu shein apiishwe.
Kama uchaguzi wa marudio waliridhia basi ujue na katiba wataridhia ibadilishwe!mkuki ulipoingilia ndipo utakapotokea....
 
Kufikisha 10% sio kigezo pekee

Kama hakuna 10% inaangaliwa idadi ya wawakilishi.

Kama hakuna chama kingine chenye wawakilishi, basi Rais halazimiki kushirikisha mtu mwingine kwenye maamuzi ya uundwaji wa serikali. Kwahiyo ataunda SUK kwa kutumia busara zake.

Aaah bwana, mambo ya kikatiba yanahitaji utashi wa busara tena!?

Mimi nadhani hapana. Na kwa kuwa BLW linaundwa na CCM wote, hawana kikwazo.

Wapeleke mswaada wa marekebisho ya katiba ili kuondoa vikwazo hivyo vya kikatiba, warekebishe kisha waendelee na serikali yao tuone mwisho wa yote hayo utakuwa nini
 
Rais anazo nafasi 10 za kuteua wawakilishi kutoka popote.........hata akiwatoa kwenye vyama vya siasa, hawana sifa ya kuitwa wawakilishi kutoka chama fulani cha upinzani, wanaitwa Wazanzibari.
kwa hiyo kwenye hili la Makamu wa kwanza wa Rais na Mawaziri wa kuunda SUK bado ni kizungumkuti; yaani haliwezekani.
 
Sio tu umenijibu, bali umejibu vile nami nilivyokuwa nafikri.

CC: Pasco
 
Back
Top Bottom