Nafasi ya kusahihisha mitihani ya NECTA

Nafasi ya kusahihisha mitihani ya NECTA

Statistics

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2013
Posts
3,762
Reaction score
8,003
Amani na Salama!
naomba kuuliza taratibu zinamwezesha mwalimu kupata nafasi ya kuwa miongoni mwa wasahihishaji Wa mitihani iliyo chini ya baraza la mitihani la taifa.
nawapenda.
teacher Noni
 
Ninavyojua walimu wateule huwa wanaandikiwa barua na baraza kuombwa kwenda kusaisha ata kwenye kutunga huwa wanaandikiwa barua ya kuombwa kutunga
 
Amani na Salama!


naomba kuuliza taratibu zinamwezesha mwalimu kupata nafasi ya kuwa miongini mwa wasahihishaji Wa mitihani iliyo chini ya baraza la mitihani la taifa.


nawapenda.




teacher Noni
wewe ni teacher Noni wa Uusseri?
 
wewe ni teacher Noni wa Uusseri?
Iko hivi, NECTA wanatuma inventory form kwa Mkuu wa shule ajaze majina ya walimu anaowaamini kwenye uchapaji kazi. Ikishajazwa anaituma BARAZA [confidentialy], BARAZA wakipokea hayo majina wanayaweka ktk database yao, wanaweza wakachagua jina lolote tu kulingana na uhitaji wao. Baadae muda muafaka wanatuma barua kwa mkuu wako ya kuwa umechaguliwa kutahini. Shida inakujaga kama mmekwaruzana na huyo Mkuu, anaweza asikupe barua. Baadhi ya shule za binafsi ndo kabisa hata hawapeleki hayo majina.
 
Amani na Salama!


naomba kuuliza taratibu zinamwezesha mwalimu kupata nafasi ya kuwa miongini mwa wasahihishaji Wa mitihani iliyo chini ya baraza la mitihani la taifa.


nawapenda.




teacher Noni
Miongoni mwa sifa ni
1. Uwe na umri wa miaka 5 kazini.
2. Ni lazima usiwe MJAMZITO
3. Uwe hautumii dozi yoyote
4. Uwe mzima wa afya.

Kuhusu kuchaguliwa
Mahitaji ya wasahishaji hutumwa Halmashauri juu ya uhitaji, Halmashauri hutuma mahitaji kwa wakuu wa vituo, Mkuu wa kituo hupendekeza majina ya walimu ambao baadae utachagiliwa miongoni mwa majina hayo.

Njia ya pili ni NECTA hutuma majina ya walimu wanaowataka Halmashauri kisha Halmashauri hutuma kituoni. WALIMU HAWA HUWA NI WALE AMBAO WANASAHIHISHA MARA KWA MARA NA WANAONEKANA KUWA THE BEST.

NI HAYO TU.
 
Back
Top Bottom