Nafasi ya kazi kwa mtu mwaminifu sana

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,188
7,490
Kwanza, naomba kuwashukuru wote walioonesha interest na kazi hii.

Pili, sasa naomba nitoe ufafanuzi kiasi kuhusu kazi yenyewe:

Kazi inahusu biashara ya mifugo na bidhaa zake (sio nguruwe), eneo la biashara zaidi ni dar ila baadae inaweza kuhusisha kusafiri kwenda kijijini,mazingira ya kazi yanaweza kubadilika badilika na mshahara ni maelewano.

Tatu, kutokana na kupokea PM nyingi sana, nimebaini kwamba mbinu niliyokuwa nimepanga kuitumia kwa ajili ya usaili wa uaminifu itanichukulia muda mrefu sana hadi kufikia mwisho kutokana na uwingi wa watu. Hivyo naomba kuanza na hatua ya 1 ya usaili hapa hapa (kutakuwa na hatua 7. Hatua 5 zitakuwa kupima uadilifu na uaminifu na 2 kupima mambo mengine).

Maelekezo: Wote waliookuwa interested wanaweza kujibu maswali, jibu la kwanza linalokuja kichwani mwako baada tu ya kuona swali ndilo sahihi (usifikirie sana majibu maana utakosea na kushindwa usaili). Majibu utajibia humuhumu jukwaani, watakaofaulu nitawapm kwa hatua inayofuata.

MASWALI:

1. Ushawahi kusema uongo? Kama ndio, ni tukio gani moja ambalo ulisema uongo kisha ukajuta?

2. Ushawahi kuiba au kudhulum? Kama ndio elezea kwa kifupi tukio moja lilikuwa je!

3. Kama umeajiriwa kwenye biashara, mwajiri akakuambia bidhaa X uiuze sh.90. Akaja mteja bila kuuliza bei , akakuambia “niuzie bidhaa hii sh.100”? utalishughulikiaje suala hilo hadi kukabidhi mahesabu.

Nawatakia usaili mwema.Watakaofaulu tu ndio watakaopata PM za kuendelea na hatua nyingine.
 
mkuu ungeweka na aina ya kazi ambayo unampa huyu mwana.
"Ni biashara" ila nikiiweka wazi humu watakuja watu wengi na watanisumbua kuwachuja. Nafahamu kuwa kama 95% hivi ya watu kwa sasa ni matapeli na walaghai tofauti tu ni mazingira,viwango na mbinu. Hivyo sitafafanua sana kwa sasa ili niweze kupata aina ya mtu ninayemuhitaji.
 
Natafuta mtu muaminifu sana nimpe kazi maalum.
Sifa, awe anaishi dar,
Awe mwanaumeAwe mchapakazi,
Awe mbunifu,
Asiwe na vijitabia vya ulaghailaghai,
Awe mbunifu na asiwe bishoo.

La muhumu kupita yote: Awe mwaminifu kwa kiwango cha juu sana (uaminifu huo utapimwa kwa kutumia mbinu maalum na ambaye atajitokeza kama sio mwaminifu akadanganya kuwa ni mwaminifu atapata majanga ambayo pengine hajawahi kuyapata tangu azaliwe, kabla ya kuanza kazi).

Mwenye sifa PM.
Naomba hiyo kazi mkuu nipo dar nimeisha Ku PM
 
kazi gani hii jamani mmmh mweke mume au mkeo unajua pa kumkamatia vinginevyo unatafuta majanga
 
Back
Top Bottom