Nafasi ya Bakora katika Malezi,

Nafasi ya Bakora katika Malezi,

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,832
Reaction score
6,470
Habari za wakati huu;

Binafsi ni Mlezi wa watoto kadhaa na ushehe.Katika kulea watoto wangu huwa ni mpenzi mzuri wa matumizi ya Bakora hasa pale ninapotaka kusisitza Jambo.

Binafsi huwa natumia bakora kwa watoto wangu kuanzi umri wa mwaka na nusu mpaka miaka 10 nikiamni kwamba katika umri huu mtoto anajenga personality yake.Ofcourse kiwango cha bakora kwa mtoto wa mwaka na nusu huwa ni tofauti na kwa mtoto mkubwa zaidi.Kwa mfano;

Mtoto wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka 3 huwa na muadhibu katika situation zifuatazo,K
  1. Kujisaidia randomly bila kutumia pot au kutoa taarifa,
  2. Kunililia mimi au kumlilia mtu yoyote wakati anapotaka kutoka
  3. Tabia zozote zinazoonyesha insubordination,arrogance au ukorofi usiokuwa na maana.
Kwa mtoto ambaye ana umri wa kuanzia 3 hadi 5 huwa namuadhibu katika makosa yafuatayo
  1. Kukataa kufuata maelekezo yoyte halali kama vile kwenda kulala,kuoga
  2. Kutokuzingatia ratiba hasa ya kufanya homework na kujisomea au kuamka asubuhi kujiandaa kwenda shule
  3. Kutokutunza mali zake kama vile penseli,dafatri,vitabu,bagi na nguo
  4. Kotokuamkia wageni au watu wazima
  5. Kutoka nyumbani kwenda kucheza mbali na nyumbani bila kuaga.
  6. Kutumia maneno yasiokuwa ya staaa ama ya kuokoteza
  7. Kukremisha miziki hasaambayo ina maneno yenye maudhui yasiyofaa
  8. Kukataa kuoga
Makosa haya yote yanapokea adhabu anuai ikiwamo bakora

Kwa mtoto wa miaka mitano na kuendelea makosa yanayoita adhabu ni pamoja
  1. Kupigana ama kupiga wenzake
  2. Kesema uongo wa aina yoyte
  3. Kutokufua nguo ya ndani
  4. Kutokuoga
  5. Makosa yote yaliyoko katika kundi lililotangulia
  6. Tabia zozote ambazozinaonesha,uzembe,kiburi,umajinuni,umbea
Tumaini langu ni kwamba kwa Bakora hizi ni baraka za Mola watoto hawa watakuwa na nidhamu na bidii katika maisha yao wasijeishi maisha ya kijinga kwa kukosa uangalizi

Tujadili zaidi juu ya umuhimu wa bakora katika malezi.Binafsi sina mpango wa kutumia bakora kwa wanangu walio na umri wa 10+
 
Back
Top Bottom