Nafasi Ukondakta - Msaada

Nafasi Ukondakta - Msaada

The Giant

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2012
Posts
504
Reaction score
96
Habari, wakuu?
Kuna mdogo wangu (kiume) kamaliza form four kitambo kidogo, Ila mambo yakamwendea kombo, hakuweza faulu alikuwa anafanya ya kazi bandari (clearing & forwarding), baada ya sekeseke la magufufuri, kampuni yao ikafungwa na kazi akawa amekosa.

Ana driving license Ila ni ya gari ndogo (binafsi), haimruhusu kuendesha gari ya Abiria.
Anahitaji nafasi ya ukondakta wa daladala, hususani za hapa Dar Kama una connection yoyote na wamiliki, madereva, etc.

Naombeni msaada wakuu, mtaani ni pagumu aisee ila kma kutakuwa na nafasi nyingine ya kazi tofauti, usisite kushare nami, ntaongea na mhusika.
Shukrani.
 
Kwa ninavyojua makonda hugeana kazi kwa kujuana hivyo ukikaa kwenye vijiwe vyao ndiyo unajitengenezea jina na uaminifu.
 
Sio lazima ukonda tu. Kuna mtu aliweka bandiko anatafuta watu wa kuuza ice cream. Jaribu kufatilia ajira yeyote muhimu tu.
 
Dah! Ningekuwa bado namiliki Kirikuu ningempa ajira! Nimewasadia sana vijana wengi kupata uzoefu wa udereva kutokana na kuwaamini. Japo walikuwa malena ila niliwapa gari wakawa wanapiga kazi. Hivi sasa wote ni madereva wazoefu tu!
 
Shukrani kaka kwa msaada wako kwa vijana
 
Back
Top Bottom