Nafasi uenyekiti UVCCM moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi uenyekiti UVCCM moto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 19, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wednesday, 18 May 2011 21:33
  [​IMG]

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Martin Shigela(kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja huo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi Zanzibar, Jamal Kassim Ali makao makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam jana. Fidelis Felix

  Exuper Kachenje

  KINYANG'ANYIRO cha kuwania nafasi ya uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kimezidi kushika kasi baada ya jana, Kaimu Katibu Mkuu wa umoja huo Zanzibar, Jamal Kassim Ali kuchukua fomu na kufikisha idadi ya wanaowania kuwa 12.

  Idadi hiyo ya wagombea, wote kutoka Zanzibar inaashiria kuweka kwa mchuano mkali wa kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Yusuph Masauni ambaye alijiuzulu baada ya kukumbwa na kashfa ya kudanganya umri wake.

  Kwa mujibu wa Katiba ya UVCCM, mwenyekiti wa umoja huo akitokea upande mmoja wa muungano, lazima makamu wake atoke upande mwingine. Kwa sasa, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo ni Benno Malisa hivyo mwenyekiti wake analazimika kutokea Zanzibar.

  Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, kati ya waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni wanawake watano na wanaume saba.

  Wengine Thabiti Jecha Kombo, Bakar Bakar, Omar Mwadi Mwarabu, Asha Suleiman Shibu, Shinuna Kombo Juma, Mwanawewe Usi Yahya, Laila Burhan Ngozi na Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamis.
  Wengine ni Mjumbe wa Baraza Kuu la umoja huo, Khadija Nassor Abdi na Innocent Melleck Shirima na Hamidu Bilal Gharib ambaye ni mtoto wa kaka yake Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal.

  Akizungumzia uchaguzi huo, Shigela kwamba kinachofanyika ni kujaza nafasi ya Masauni ili kukamilisha miaka mitano aliyoianza kabla ya kujiuzulu.

  "Tunajaza nafasi hiyo kukamilisha miaka mitano aliyoianza aliyekuwa mwenyekiti wetu, Yusuph Masauni," alisema Shigela na kuongeza:

  Shigela alisema katika mchakato huo, UVCCM haitarajii wagombea kuchafuana na kwamba umoja huo utakuwa makini katika kufuatilia taarifa zao.

  "Tunazingatia uadilifu, tutakuwa makini katika kufuatilia taarifa za wagombea. Hatutarajii wagombea kuchafuana, pia ni vizuri wagombea tukiwasilisha taarifa sahihi juu ya maisha yao, historia yao na elimu," alisema Shigela.

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu za kuwania nafasi hiyo, Kaimu Naibu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM, alisema ameamua kuwania nafasi hiyo baada ya kuifanyia utafiti.

  Alisema anao uwezo wa kufanyia kazi changamoto mbalimbali zilizopo miongoni mwa vijana katika umoja huo, CCM na taifa kwa jumla.

  Mwenyekiti wa zamani CCJ
  azungumzia kauli ya Mpendazoe

  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Jamii (CCJ) ambacho kimefutwa, Richard Kiyabo jana alijitokeza na kusema kwamba hapakuwa na mwanzilishi mwingine wa chama hicho zaidi yake na aliyekuwa Katibu Mkuu wake Renatus Muabhi na kwamba CCJ imeshakufa hivyo kuizungumzia ni sawa na kumzungumzia marehemu jambo ambalo linatisha.

  Kiyabo ambaye sasa amerejea CCM, alikuwa akijibu madai ya kada wa Chadema, Frederick Mpendazoe ambaye hivi karibuni akiwa Njombe alisema walioanzisha CCJ ni pamoja na Waziri wa Afrika, Mashariki, Samuel Sitta na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

  Jana, Kiyabo katika mkutano uliomjumuisha Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kirumbe Ng'enda alisema Mpendazoe anapaswa kuulizwa kama alipohamia CCJ alipokewa na nani na ili kuthibitisha madai yake, ataje namba za kadi za uanachama na nyadhifa walizokuwanazo ndani ya CCJ viongozi hao. Alimtaka Mpendazoe kusoma mahojiano yake na gazeti hili la Mwananchi yaliyochapishwa Aprili 6 ,2010 ambayo alinukuliwa akimkaribisha Sitta CCJ.

  "Nawashauri Mpendazoe na wenzake waache siasa za udaku, hazitawafikisha Ikulu, Watanzania wanaelewa wala si mbumbumbu," alisema na kuongeza:

  "Chadema wameonyesha kwamba nguvu ya umma siyo kura tena, bali maandamano na vurugu zenye lengo la kuitoa serikali madarakani. Je, wanaiheshimu demokrasia kweli? Watanzania tuwe makini na watu wasio na mapenzi mema na amani ya nchi yetu. Tukumbuke suala la amani ni sawa na nyanya. Nyanya ikitumbuka kuishona tena huwa ni kazi ngumu."

  Kwa upande wake Ng'enda alisema wanaoelekeza tuhuma kwake wakitaka ajivue gamba wamekosea njia kwa kuwa hawakufuata utaratibu ndiyo sababu hawakufanikiwa.

  "Walionituhumu walikosea, hawakufuata utaratibu, ndiyo maana hawakufanikiwa na chama kimewapa adhabu. Utaratibu ukikamilika nami mtaniona najivua gamba. Ukatibu niliupata mwak 2006, kabla ya hapo niliishi vipi? maisha siyo ukatibu, lakini wenzangu walikosea kwa kutofuata utaratibu wa chama na kutumia vyombo vya habari," alisema katibu huyo wa CCM mkoa wa Dar es Salaam.
   
Loading...