Chuo kikuu hakuna combination kijana ila kuna courses /programs mbali mbali.
Kwa mtu aliyosoma comb za arts Kama vile HKL, HGL, HGK, nk chuo kikuu anaweza kusoma bachelor of arts(shahada ya sanaa) Kama vile bachelor of arts with education (unakuwa mwalimu) , bachelor of arts in Sociology ,Community development (unakuwa afisa usatawi wa jamii au afisa maendeleo ya jamii) , Public Administration, Human Resources Management(unakuwa afisa tawala au afisa rasilimali watu /afisa utumishi) Mass communication, Journalism(unakuwa Mwandishi wa habari kwenye magazeti, mtangazaji wa Redio au TV,afisa habari kwenye wizara mbalimbali, kwenye ofisi za wakuu wa mikoa, halmashauri za wilaya na, manispaa na miji au afisa habari wa makampuni mbalimbali ) ,Bachelor of Laws (unakuwa mwanasheria, afisa sheria, wakili, hakimu nk)
Haya wewe ungependa uwe nani hapo baadae?