Nadhani tuanze kufikiria kuwatumia wataalam waliobobea na pia kuagiza Chanjo iliyo Salama

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,321
11,315
Hali sio nzuri!

Ila najiuliza, Tanzania yetu ya kupendeza hakuna wataalam wa MICROBIOLOGY au BIOTECHNOLOGY ambao either wamefundishwa huku nchini au nje ya nchi, ambao wakati huu wangekua msaada mkubwa sana kutuongoza katika kutambua chanjo ambazo ziko tayari zinatolewa katika mataifa mengine.

Ni wakati sahihi kwa serikali yetu kuanzisha kitengo kikubwa cha biological warfare ndani ya JWTZ military intelligence unit.

Ni wakati sahihi pia wa kusomesha wataalamu wa hali ya juu wa microbiology, biotechnology, synthetic biology na vitu kama hivyo. Huko tuendako sio kuzuri.

Tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye sayansi kwa ajili ya usalama wetu siku za usoni.

Chanjo zinazofanya vizuri kwa sasa ni za nchi ya ISRAEL na URUSI.
 
Taasisi za utafiti madawa zimetengeneza dawa kadhaa ambazo zinaua virusi vya korona. Dawa hizi ziko kwenye maduka ya madawa. Kuna pia za kinga, ambazo ni bora zaidi kuliko chanjo hiyo ya ughaibuni.

Tukubali, Tujali na Kutumia dawa zetu.
 
Taasisi za utafiti madawa zimetengeneza dawa kadhaa ambazo zinaua virusi vya korona. Dawa hizi ziko kwenye maduka ya madawa. Kuna pia za kinga, ambazo ni bora zaidi kuliko chanjo hiyo ya ughaibuni.

Tukubali, Tujali na Kutumia dawa zetu
Mkuu hizo dawa unasosema , huko mahospital hazipelekwi ? Na kama zinapelekwa mbona watu wanazidi kupukutika, mpaka Hapo zitakua zimesha prove failure
 
Wataalam wanajua kuwapa sapu wanafunzi.
Halafu hizo chanjo zimefeli kwa mdudu wa sauzi.
Iliyofeli ni chanjo moja tu. Ni ile ya Astrazeneca ambayo kwa bahati mbaya Wasauzi ndiyo walikuwa wameagiza. Za Moderna na Pfizer ziko vizuri. Za Wachina na Warusi nadhani hakuna data za kuaminika. Ni suala la kuchagua chanjo mojawapo kati ya hizo, kufanya majaribio ya haraka na kuanza kuchanja watu kama watu wanavyofanya duniani kote.

Hata hii ya Astrazeneca siyo kwamba imefeli kabisa kwa hii variant ya Afrika Kusini. Inatoa kinga fulani na waliochanjwa wakipata kirusi hawaumwi sana kiasi cha kulazwa hata kama ni wazee. Kwa hivyo bado ina faida fulani...
 
Israel hawana chanjo wanatumia Pfizer one. Imefanya vizuri sana kule.

Tatizo inabidi kuwa store under -70 degree.

Sidhani kama tuna uwezo wa kutosha ya kuziagiza,kuzitunza kwenye hospitali zetu zote under such temperature hadi vijijini.

Mengine yote nakubaliana na wewe. Naona vita vya mbele vitakuwa biological or chemical welfare.
 
Tatizo ni kubwa zaidi ya unavyolitazama hapa. Shida yetu hatuthamini wasomi wetu. Mishahara kiduchu, mazingira magumu ya kufanyia kazi na ukosefu wa uhuru katika kazi zao. Kila kitu ni siasa. Hata wakiwepo bila kubadilisha mazingira na utamaduni wataishia kukimbilia nje tu. Tembea tembea huko nchi za nje uone.

Kuna Watanzania wasomi na watafiti wazuri sana wapo kila mahali lakini wamefuata maslahi na muhimu zaidi kuheshimiwa utaalamu wao na mazingira mazuri ya kasi.

Sisi tumewekeza kila kitu kwa wabunge na wanasiasa na kuacha kada zingine hata kama ni za muhimu namna gani. Ndiyo maana brain drain ni tatizo kubwa sana.

Biological warfare wakati dunia nzima imepigwa marufuku. Mtengeneze virusi kama silaha? Hapa Bongo? Sidhani. Mtakwenda kuvitumia wapi bila kuja kutandikwa na wakubwa? Dunia sasa inaelekea katika silaha za Cyber.

Mtu yuko huko Serbia anahack grid yako ya umeme na kuiharibu kwisha. Au anahack masetelaiti yako unayotumia kuongozea drones, mabomu yako, GPS system yako basi kwisha kazi. Hata kama kirusi hiki Wachina wamekitengeneza basi deployment yake siyo ya kitoto na kanchi kadogo kama Tanzania hatuwezi.

Na utengenezaji wa hizi chanjo ni ghali inabidi kujipanga sawa sawa

Screenshot_20210217-214214_Google.jpg
 
Tatizo ni kubwa zaidi ya unavyolitazama hapa. Shida yetu hatuthamini wasomi wetu. Mishahara kiduchu, mazingira magumu ya kufanyia kazi na ukosefu wa uhuru katika kazi zao. Kila kitu ni siasa. Hata wakiwepo bila kubadilisha mazingira na utamaduni wataishia kukimbilia nje tu. Tembea tembea huko nchi za nje uone. Kuna Watanzania wasomi na watafiti wazuri sana wapo kila mahali lakini wamefuata maslahi na muhimu zaidi kuheshimiwa utaalamu wao na mazingira mazuri ya kasi.

Sisi tumewekeza kila kitu kwa wabunge na wanasiasa na kuacha kada zingine hata kama ni za muhimu namna gani. Ndiyo maana brain drain ni tatizo kubwa sana...

Biological warfare...wakati dunia nzima imepigwa marufuku. Mtengeneze virusi kama silaha? Hapa Bongo? Sidhani. Mtakwenda kuvitumia wapi bila kuja kutandikwa na wakubwa? Dunia sasa inaelekea katika silaha za kielektroniki. Mtu yuko huko Serbia anahack grid yako ya umeme na kuiharibu kwisha. Au anahack masetelaiti yako unayotumia kuongozea drones, mabomu yako, GPS system yako basi kwisha kazi. Hata kama kirusi hiki Wachina wamekitengeneza basi deployment yake siyo ya kitoto na kanchi kadogo kama Tanzania can't pull it off...

Na utengenezaji wa hizi chanjo ni ghali inabidi kujipanga sawa sawa
View attachment 1705129
Biological and chemical welfare ll mainly be between super powers. (China, USA, Russia)But we will all suffer the consequences.

Cyber war is kind of zero sum game.

Thing like Corona Virus can wipe out the country slowly, power shifting eastward, over million people already dead and EU, over 100000 in UK. Over 50000 in USA.

Every 20 seconds somebody dies in USA. In could be you.

To get back to that level of economy pre-pandemic taxes ll have to rise. People ll have more difficult life. It ll take USA,UK,EU about 10 years of high taxes to get to the pre-pandemic level.

If China send to US, EU, UK another curceball of pandemic (biological weapon in 5 years time). She ll become super power. Reigning supreme.

You can always say you didn't know about it. While at same limit people to travel in your own country but allow them to go all over the World to spread the disease.
 
Hapa umezungumzia vitu viwili sasa biological war fare na cyber war. kwenye cyber tayari tz wamejizatiti.....but sijui kwa kiwango kipi
 
Hali sio nzuri!

Ila najiuliza, tanzania yetu ya kupendeza hakuna wataalam wa MICROBIOLOGY au BIOTECHNOLOGY ambao either wamefundishwa huku nchini au nje ya nchi, ambao wakati huu wangekua msaada mkubwa sana kutuongoza katika kutambua chanjo ambazo ziko tayari zinatolewa katika mataifa mengine.

Ni wakati sahihi kwa serikali yetu kuanzisha kitengo kikubwa cha biological warfare ndani ya JWTZ military intelligence unit.

Ni wakati sahihi pia wa kusomesha wataalamu wa hali ya juu wa microbiology, biotechnology, synthetic biology na vitu kama hivyo. Huko tuendako sio kuzuri.

Tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye sayansi kwa ajili ya usalama wetu siku za usoni.

Chanjo zinazofanya vizuri kwa sasa ni za nchi ya ISRAEL na URUSI.
Kweli serikali ifanye kitu isipuuze mwisho wa siku ni Taifa linazidi kupoteza nguvu kazi kbs, wataalamu wetu watoke waende basi hata Israel kuzifanyia tafiti hizi chanjo, la sivyo , juhudi inahitajika haraka.
 
Iliyofeli ni chanjo moja tu. Ni ile ya Astrazeneca ambayo kwa bahati mbaya Wasauzi ndiyo walikuwa wameagiza. Za Moderna na Pfizer ziko vizuri. Za Wachina na Warusi nadhani hakuna data za kuaminika. Ni suala la kuchagua chanjo mojawapo kati ya hizo, kufanya majaribio ya haraka na kuanza kuchanja watu kama watu wanavyofanya duniani kote.

Hata hii ya Astrazeneca siyo kwamba imefeli kabisa kwa hii variant ya Afrika Kusini. Inatoa kinga fulani na waliochanjwa wakipata kirusi hawaumwi sana kiasi cha kulazwa hata kama ni wazee. Kwa hivyo bado ina faida fulani...
Ingesaidia basi pengine hata kupunguza vifo huku kwetu. Serikali iamke sasahivi
 
Hapa umezungumzia vitu viwili sasa biological war fare na cyber war. kwenye cyber tayari tz wamejizatiti.....but sijui kwa kiwango kipi
Ndiyo. Biological matumizi yake magumu sana kimataifa. Ndiyo maana nimegusia Cyber. Kama tumejizatiti huko ni sawa japo sina uhakika kama kweli tunaweza kusimama na Waisraeli, Warusi, Wamarekani, Wairani , Wakorea ya Kaskazini, Wachina na wengineo tukafua dafu. Au labda tukilinganishwa na wenzetu huku Afrika ndo tuko vizuri?

Haya mambo siyo ya muda mfupi wala kukurupuka. Yanahitaji uwekezaji na mikakati ya muda mrefu.
 
Biological and chemical welfare ll mainly be between super powers. (China, USA, Russia)But we will all suffer the consequences.

Cyber war is kind of zero sum game.

Thing like Corona Virus can wipe out the country slowly, power shifting eastward, over million people already dead and EU, over 100000 in UK. Over 50000 in USA.

Every 20 seconds somebody dies in USA. In could be you.

To get back to that level of economy pre-pandemic taxes ll have to rise. People ll have more difficult life. It ll take USA,UK,EU about 10 years of high taxes to get to the pre-pandemic level.

If China send to US, EU, UK another curceball of pandemic (biological weapon in 5 years time). She ll become super power. Reigning supreme.

You can always say you didn't know about it. While at same limit people to travel in your own country but allow them to go all over the World to spread the disease.
Bahati mbaya lugha uliyotumia inanipiga chenga dah! Ukiweza ziweke hizi nondo katika lugha yetu pendwa.
 
Back
Top Bottom