Nadhani mlinipenda kwa dhati, asanteni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nadhani mlinipenda kwa dhati, asanteni

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by frank m, Jun 24, 2012.

 1. f

  frank m Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikitizama nyuma naona michirizi ya damu, mioyo iliyoumizwa, nami ni mmoja wa wahanga. Nitakuwa muongo nikisema sijaumiza wengine na mimi. Nimekuwa na wanawake kadhaa, leo niwashukuru kwa kunipenda kwa dhati, japo kuwa mlinitenda na niliowatenda....., LEO NASEMA ASANTENI SANA KWA MAPENZI YA DHATI!

  Wa kwanza nilikuwa na miaka 19,nilimpenda na kumwamini sana. Alikuwa kila kitu kwangu na ilikuwa kama ndiye mwanamke pekee duniani wengine nilikuwa sioni. Yaani kupenda mara ya kwanza we acha tu. Alikuwa that decent girl asiyejua chochote, gumzo la shule, demu wa mfano ambaye kila mtu alimtaka bahati ikanidondokea mimi. Well alikuja kunisaliti, labda kwa kutafuta ladha tofauti, labda kwa kudhani there are greener pastures on the other side! Alishindwa kuficha akaja kuniambia mwenyewe kuwa AMENISALITI, siri ameshindwa kuitunza ukweli ndio utamweka huru. Japo bado nilimpenda sana sikuweza kumsamehe, vilio na maombi yote ya msamaha vikadondokea masikio yaliyozibwa. Nikampiga chini, sijui kama nilifanya maamuzi sahihi? Masikini huyu binti alinipenda, no doubt labda paka kesho anaendelea kunipenda. I can see it in her eyes kila tukikutana. Pamoja na maumivi uliyonisababishia una nafasi ya pekee kwenye moyo wangu na itakuwa hivyo daima.

  Nikasema mapenzi nipumzike kwanza, majeraha yapone. Mwaka mmoja baadae nikakutana na wewe binti mwenye mchanganyiko wa kitusi. U mzuri mama hakuna mjadala. Kwanza niliogopa nikajiambia kwa uzuri huo na uchangamfu huo mbona wengi sana watakuwa wamejiweka hapo! Nilipigwa na butwaa nilipobaini mapenzi wewe ulikuwa bado, kwa babati mbaya, nasema bahati mbaya nikakuingiza kwenye mapenzi. Ukachanganyikiwa nusura uache chuo. Kama si kuwa extra bright mbona ungefeli! Trust me nikitazama nyuma roho inanisuta na naumia jinsi nilivyoshindwa kuufungua moyo nikupende ulivyostahili, nikupende kama ulivyonipenda. Ulikuwa ukatili sana ila ilibidi nikuambie ukweli, nisingeweza kufungua moyo wangu nikupende kama unavyostahili, nikakupa go ahead uolewe na yule jamaa aliekuwa anakupenda hadi ujinga, mara ngapi unapata mwanaume aliye tayari kufa kwa ajili yako? Najua ulinipenda na siku zote nashukuru kwa hilo japo sina hakika kama umewahi kunisamehe. I begged your husband to make sure you are always happy, to love you the way you deserve to be loved.

  Baada ya kuona maumivu niliyosababisha nikasema enogh with the decent girls, nataka mcharuko. Nikatutana na wewe binti wa mjini, kiumri ulikuwa mdogo ila mambo yako mmmmh, kama Lulu vile. Nilijua ulikuwa mwingi japo sikuwahi kukuambia hadi tulipoachana. Niliwajua waume wenza watatu at least ila sikujali mmoja wapo alikuwa kaka yangu wa mjini, sikutaka kukuambia hadi ulipoleta drama wakati wa kuachana. Hakuna raha kama mwanamke kukudanganya na ukajua anakudanganya. Unaniambia "baby sitakuwepo leo namshikia best angu shift kazini" nikimpigia bro ananiambia shemeji yako kipotabo leo yupo kwangu. Unaniambia shangazi ako kafariki unaenda kuzika, bro ananitext nipo na yule chic "Kimodo" tunakula raha Bagamoyo. Lakini kwa nini ulikuwa na mimi wakati hakuna chochote nilichokuwa nakupa? Najua jinsi ulivyokuwa unamchuna bro, hakuwahi kuwa na demu mkali kama wewe na pesa kipindi kile alikuwa nazo. Gemu lilikuwa mipira siku zote, nilipozidiwa siku moja nikauza mechi duuuh, nikajua napokwenda si pazuri, nijipa moyo nikaenda kupima ngoma, kujiona nipo salama nikajua its time to move on, namna nzuri ya kukuacha ilikuwa ni kutembea na beste ako Mary, she is so sex kubali tu, ilikuwa shukrani kwa kuniuzia mafaili yako. ulipokuja juu nikakupa faili lako lote, you were so mad! eti kwa nini siku zote nilikuwa nakuenjoy wakati najua unanidanganya. Anyway naamini ulinipenda, mabwana wengine walikuwa wakikuhonga kweli kweli pamoja na yule dogo wa benki aliyekuongezea pesa unanunu ka RAV 4 kako ila kwangu hukuwahi kutaka kitu.

  Naam, nikampenda binti mmoja Chotara, mama Mholanzi baba Mzigua! Lakini alikuwa mdogo sana miaka 15! Nikasema nimsubiri akue kidogo! Wakati nasubiri akafanya kosa la kiufundi kunitambulisha kwa mama yake. The chemistry! tukawa marafiki kupindukia na mama mtu, alikuwa kanizidi kama miaka 13. Siku moja out of no where akaniambia Frank M una mengi ya kujifunza kuhusu wanawake. Nikamwambia mimi! akaniambia hakika. Tunacheza disko siku moja tukajikuta tunanyonyanda ndimi, safari iliyoanza kama ajali ikaishia kwake tena sebuleni na kitandani. Dogo alikuwa shule ISM moshi. Uzee dawa bwana, namshukuru huyu mama alinifunza mengi kuhusu wanawake, kitandani na nje ya kitanda. Alikuwa na ujuzi ambao sijauona tena kwa mwanamke mwingine. Huyu sijui kama alinipenda kimapenzi lakini alinijali sana, alitaka niwe mwanaume wa kipekee kwa hakika. Alikuwa serious kweli kweli kunipa shule. Ugomvi ulilipuka sababu ya wivu na mwanae, to be honest nilishaamua mwanae atabaki kuwa rafiki tu japo alikuwa anaongezeka uzuri kila kukicha, mama hakuamini at some point tukakubaliani I should get out of their life.

  Nikaamua nitafute dodo changa, nishaonja zee nahitaji kujua ladha ya changa. Jamaa yangu marine biologist alikuwa anamfukuzia demu mmoja voluntia wa kifaransa ila ana asili ya kirusi. Shida mshkaji hakuwa na uzoefu wa kutosha na wazungu, he was struggling na yule binti alikuwa mzuri, acheni ninyi kuna wazungu wazuri. Nikatumia skills nilizozipata kwa mama hapo juu nikampindua jamaa yangu. Najua ulinipenda kila siku zilivyozidi kusonga, ukaanza kufikiri kuolewa na mwafrika, ukaanza kujifunza lugha yetu kwa jitihada, na tamaduni zetu, ukataka kujua mwanamke wa kitanzania anatakiwa aweje, amfanyie nini mumewe hata kanga ukawa unavaa, ugali ukajifunza kusonga. Kitandani ulikuwa unapata kichaa kabisa, ukaweka wazi hauko tayari kunishare na mwanamke mwingine. Nakumbuka ulichomwandikia mama yako, "I have found love" Ukamwambia unapenda kila kitu kuhusu Tanzania, hujawahi kuona uzuri kama huu, unaitazama dunia kwa jicho tofauti. Yeye alikujibu kwa uangalifu mkubwa, alijua zaidi yako kuhusu wanaume, alijua zaidi kuhusu dunia. Alijua vitu vizuri havidumu. Bado nakupenda japo huamini hivyo, na hilo linanisikitisha sana! Ni vile tu nyakati hazikuwa sahihi, tulisafiri kwa kasi mbili tofauti kabisa.

  Malipo ni hapa hapa... namaanisha duniani, nikakutana na guberi haswaaa, pumziko la wabunge, hakianani ......

  Naomba niendelee next Sunday!
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Eeenhe mtoto mzuri frank m hadithi hii inatufundisha nini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,924
  Trophy Points: 280
  stori za kupweketupweketu hizi, badala ya kufariji mioyo ya watu zinaumiza, kuna mtu anapenda kukaa na makunyazi ya moyo siku hizi? haujui kuwa stress zinafupisha maisha? watu tumefanya kazi vichwa vimechoka alafu unakuja kusoma stori ya huzuni na kuweka kunyanzi kwenye moyo kama hii..wekeni stori ambazo basi zitatufanya tucheke tuongeze siku alaaa
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  dah....we kiboko.....
   
 5. f

  frank m Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I will take this into consideration Hute, aksante
   
 6. f

  frank m Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imebidi nicheke tu sweet lady!
   
 7. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Cheka mwaya uongeze siku za kuishi maisha yenyewe mafupi haya kwanini unune bana?
   
 8. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Duhhhh nimesoma hiyo paragraph ya kwanza tu hisia zote zimerudi kwenye kitabu
  Kitamu ambacho ndo Nimemaliza kukisoma
  MAJERUHI WA PENZI by Mzee Mwanakijiji.

  What a brilliant book ..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. f

  frank m Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tell me Afrodenzi, naweza kuandika kitabu? Ni ndoto yangu kubwa tena niandike maisha yangu ila sitajitaja jina
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,834
  Trophy Points: 280
  Mmmmmmmmmmmmh

  TGNP
   
 11. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  My dear kila kitu maishani ni kujaribu ..
  Na kama ni ndoto yako amka sasa kutoka ndotoni na anza kuchangamka ili hiyo ndoto iwe reality ..

  Wasomaji na wapenzi wa kusoma tupo wengi.

  Kila lakhuri. :)
   
 12. G

  GTesha JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 203
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mmh! malizia aisee nangojea kwa hamu
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  duh huyo guberi ndo anakufaa, utakuwaje na binti then umle mama yake?????
   
 14. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,613
  Trophy Points: 280
  nimependa habari yako ilivyo ndefu. mia
   
 15. M

  Mocrana JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 532
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kazi kweli kweli
   
 16. B

  Bolivar JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Umefunguka ehhhh, mwaga vitu! nasubiri jumapili ijayo
   
 17. f

  frank m Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thank you for the encouragement, utakuwa kati ya watu nitakowashukuru kikikamilika
   
 18. f

  frank m Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aksante figganigga
   
 19. m

  mtufulani Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  usisubiri mpaka jpili. maliza utamu wote leo
  .hilo pumziko la wabunge liko aje?
   
 20. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  uo utam unaojisifia wangekuja wenyewe kuthibitisha ndo ingekuwa poa sana.
   
Loading...