Nadhani kuna haja kuwalazimisha wahindi wafanye kuunganisha Bajaj hapa Dar es salaam

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,063
40,724
Hii iwe ni executive order, sio ombi wala kubembelezana. Wapewe godown kule chang'ombe, waagize hizo parts toka India na zikifika Dar basi uunganishaji ufanyike kwa lengo la walau kuibia ibia teknlojia ili pengine baadae na sisi tuanze kuzalisha pikipiki za matairi matatu na tuziite Tanzanite.
Pia ajira zitapatikana kidogo angalau...
 
Bajaj hazipakiliwi kwenye container zikiwa zimekamilika. Zinakuja kwenye mabox kama spares tu... zinakuwa assembled hapa hapa Tanzania.. ukitaka kujifunza tembelea wauza bajaj
Aisee.., hii ni habari njema sana...
 
Sio bajaj tu mkuu, pikipiki za matairi 2, na hata baiskeli pia wanaassemble hapahapa.
Pia hapa tunaunda bodi za buses, tunaunda chases za ma semi trailer nk.

Ambacho bado ni kuunda engine, gear box na kuassemble gari.

Sent using Redmi Y2
Nadhani tusikate tamaa, hadi kieleweke, kule Ghana Kantanka motors wanamimina engine wenyewe na kuassemble kila kitu mwanzo mwisho
 
Wakikataa watafanywa nini?
Hii iwe ni executive order, sio ombi wala kubembelezana. Wapewe godown kule chang'ombe, waagize hizo parts toka India na zikifika Dar basi uunganishaji ufanyike kwa lengo la walau kuibia ibia teknlojia ili pengine baadae na sisi tuanze kuzalisha pikipiki za matairi matatu na tuziite Tanzanite.
Pia ajira zitapatikana kidogo angalau...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii iwe ni executive order, sio ombi wala kubembelezana. Wapewe godown kule chang'ombe, waagize hizo parts toka India na zikifika Dar basi uunganishaji ufanyike kwa lengo la walau kuibia ibia teknlojia ili pengine baadae na sisi tuanze kuzalisha pikipiki za matairi matatu na tuziite Tanzanite.
Pia ajira zitapatikana kidogo angalau...
Assembly mbona inafanyika? Pikipiki na Bajaji huletwa vipande vipande ndani ya kasha na kuunganishwa.

Natumaini ulitaka kusema "body" zitengenezewe hapa hapa nchini.
 
tungeigilizia technolojia..maana mbongo atengeneze gearbox ya bajaji aiuze 50000 ni ngumu..au cluch plate auze elfu saba...ni ngumu tunatumia nguvu sana kuliko technologia...tungewekeza huko kwanza la sivyo tukiunda bajaji itauzwa 20m
 
Nadhani suala la bidhaa za Tanzania kuwa bei ghali kuliko bidhaa za nje ni tatizo sugu na lipo katika kila sekta, moja ya suluhisho la hili tatizo ni kupatikana kwa umeme wa bei nafuu, na ndio hasa lengo la Rufiji hydro power
 
Tatizo tulilonalo hatujikiti sana katika Research and Innovations. Fedha zetu nyingi zinaelekezwa kwenye Siasa.
 
Bajaj hazipakiliwi kwenye container zikiwa zimekamilika. Zinakuja kwenye mabox kama spares tu... zinakuwa assembled hapa hapa Tanzania.. ukitaka kujifunza tembelea wauza bajaj
Kuiba teknolojia ya pikipiki mbona rahisi tu .Engine zinauzwa ,tairi zinauzwa ,taa zinauzwa unachotakiwa kufanya ni kununua pikipiki ifumue yote kila kitu tandaza chini tafuta fundi welding akutengenezee lile frame la pikipiki,tanki na nenda kwa wasambaa wakutengenezee kiti Cha pikipiki kile sponji,mtafute fundi umeme wa magari akuunganishie mifumo ya umeme, Kisha Anza kupachika, pachika na hivi ambavyo waweza nunua au agiza nje injini, toka kwa wauza injini za pikipiki,gurudumu,mnyororo,taa,betri nk itest Kama iko viziri Anza kuunda za kwako kasajiri TRA zipate namba pikipiki ulizounda ziite YEHODAYA kwa heshima yangu niliyekupa wazo
 
Back
Top Bottom