Nachukizwa Sana Na tabia Hizi...!

MzaramoTz

JF-Expert Member
Dec 13, 2017
1,829
2,986
Salaam wote wadau natumai mu-wazima kabisa. Kuna tabia ambazo mimi binafsi huwa nachukizwa nazo kupita kiasi na tabia hizo ni hizi hapa chini :-

1.Kuchunguliana kwenye magari.
Hii tabia siipendi kama nini, utakuta mtu anaendesha gari lakini anachungulia chungulia watu wengine kwenye gari nyingine za pembeni. Na wengine utakuta wanakodoa kabisa macho wanachungulia kwenye madaladala ili iweje, unataka wakuone kuwa unaendesha gari au ni vipi, kwa nini msiendeshe gari mkaangalia mbele na mkonsetreit kwenye barabara, mnawakodolea macho watu wengine mnatafuta kitu gani hasa, hebu acheni kuwakodolea watu madirishani aisee.

2.Kuweka mzigo kwenye seat.
Aisee hii tabia siipendi kupita kiasi, hasa kwa watumiaji wa gari za abiria i.e daladala. Utakuta mtu unagombania mlangoni kuingia kwenye daladala halaf ukifika ndani eti mtu kaweka kipochi kwenye seat, yaani mtu atumie nguvu zake katika kuingia mlangoni halaf wee uweke kipochi kiulaini tu eti uje kukaa, tabia hii pia sikubaliani nayo hata kidogo acheni mara moja.

3.Kugonga body ya gari ukiwa ndani.
Aisee kuna watu utakuta wakipita karibu na gari wanaligonga gonga au kulipiga ngumi nachukia kupita kiasi hili suala, halaf mbaya zaidi wala hawajali kabisa kuwa mwenyewe upo ndani unashangaa mtu anapita kwa anagonga gonga body kwa nini lakini...?

4.Demu kuomba omba hela.
Hii tabia wanayo hasa hasa wakina Mwajuma ndala ndefu, utakuta mmefahamiana siku chache tu keshaanza kuomba omba hela, ni moja ya shida za ku-date na kuku wa kienyeji ambao msingi wao ni kipochi manyoya kila mwenye hela anakifunua, hata kuzoeana bado mtu anaomba hela kwani kabla ya kujuana ulikuwa unaishije, shwayn kabisa. Mwengine ukimuita utasikia nitumie nauli halaf kuja haji hii tabia mkome kabisa, ni bora ukamwambia chukua tu uber ukifika nitalipa kuliko kutuma hela aisee.

5.Kumuita sheikh au Ustadh mtu aliyevaa kanzu au kofia.
Utakuta mtu kajivalia zake tu kikofia kuziba jua utatuka mtu anaita "aloo sheikh sheikh au utaskia wanamuita ustadh ustadh wakati hata sio muislam na wala msikiti haujui, sio kila mvaa kofia ni ustadh aisee, hebu acheni hayo majina mara moja.

6.Wanawake na vikwapa kwenye daladala.
Aisee nachukizwa sana na baadhi ya mavazi ya wanawake utakuta mtu ana kikwapa cheusiiiii tiiiiii halafu nguo aliyovaa makwapa yote yapo nje, kwa nini msivae nguo za kistaarabu...?. Utakuta mwengine kwapa linapumua hewa mbaya kabisa halaf ndio kakaa karibu yako na kikwapa kipo nje, vaeni kistaarabu kama wadada wa kiislamu huwa wanavaa nguo huwezi kuta makwapa yapo nje, kama upo kwenye gari yako sawa ila kama unapanda daladala unashika bomba na kwapa lote linakuwa nje hebu jirekebishe hiyo tabia mara moja.

7.Tabia ya kuongea na simu kwa sauti ya juu mpaka kero.
Tabia ya kuongea kwa sauti ya juu ukiwa unaongea na mtu kwenye simu inakera kupita kiasi, utakuta mtu anaongea kwa sauti ya juu utafkiri huyo mtu yupo mtaa wa 7. Mtu hata akiwa mbali ukiongea kwa sauti ya kawaida atasikia tu hakuna sababu ya kupayuka kwa sauti weeee mpaka unakera wengine haipendezi hata kidogo aisee.

8.Kupumua kwenye gari.
Aisee moja kati ya tabia zinazokera kupita kiasi ni kupumua ndani ya gari kwa kutumia makalio na kupelekea hewa kuwa mbaya sana, hebu jaribuni kuvumilia kidogo mkifika mnapokwenda mpumue weeeeee mpaka mchoke. Mbaya zaidi utakuta madirisha yamefungwa labda mvua inanyesha halaf mtu anaachia kombora hatari kabisa, hii si tabia nzuri hata kidogo aisee.

9.Kwaya au kaswida kwenye gari ya abiria.
Aisee kwenye chombo cha usafiri wa abiria utakuta mtu anafungulia kwaya au kaswida tena kwa sauti ya juu kabisa, hii sio tabia nzuri kwa sababu wanaopanda hizo gari ni watu wa imani tofauti na wewe sasa kwa nini ufungue kaswida au kwaya kwa sauti ya juu na kuwakera abiria...? Haipendezi hata kidogo muache hiyo tabia wenye magari yenu na haswa ni madereva na makonda wenu.

10.Kuchungulia simu ya mtu.
Hivi, unanichungulia simu ya mtu kwa makusudi huwa unatafuta kitu gani haswa...? Utakuta mtu anaacha yake kabisa na kufatilia simu yako kwa nini lakini, hii tabia nayo haipendezi na sio nzuri hata kidogo.

Natumai nawe utakuwa unachukizwa na tabia za baadhi ya mambo hebu weka hapa tabia unayochukizwa nayo.
 
We kweli mzaramo naona kule kwenu dar mnasema mnachamba naona umeamua kuwachamba huko kwenu dar kelo niliyo iona nikuwa na mashoga wengi halafu ni jambo la kawaida
 
Namba 7
Asee inakera sana unakuta mpo kwenye daladala alafu mtu anaongea na simu kwa sauti kubwa kama matangazo.
 
Kuna siku nipo kwenyee daladalaa naonaa kuna jamaaa anatetemekaa mbele yake yopo mwanamkee nikaonaa hili nalo nitatizoo kwenyee usafirii wetuu hususani hapa jijini kwwtu
 
We kweli mzaramo naona kule kwenu dar mnasema mnachamba naona umeamua kuwachamba huko kwenu dar kelo niliyo iona nikuwa na mashoga wengi halafu ni jambo la kawaida

Oya mkuu kausha basi. Aaaaaaagh. 😡
 
Kuna siku nipo kwenyee daladalaa naonaa kuna jamaaa anatetemekaa mbele yake yopo mwanamkee nikaonaa hili nalo nitatizoo kwenyee usafirii wetuu hususani hapa jijini kwwtu

Hahahahah unamaanisha mfadhaiko kiongozi au...? Mambo ya dungadunga hayo. Hahah.

Lol...!
 
So mtoa mada ukiwa kwny haice ukitaka 'kupumua' hua unamuomba konda asimamishe gari ukapumue nje then ukimaliza unarudi kwny gari au?
 
11. Yahusu Kubambiana. Wanawake muache kutugeuzia nyuma zenu hasa kwenye daladala zilizoshona. Mnatupa wanaume nyakati ngumu kumkontroo bwana mkubwa anapoamka in public. Nimemaliza.
 
So mtoa mada ukiwa kwny haice ukitaka 'kupumua' hua unamuomba konda asimamishe gari ukapumue nje then ukimaliza unarudi kwny gari au?

Yakupasa kuvumilia kidogo mkuu, mi huwa naubana mpaka nikifika ndio naachia ili kutokuwakera wengine mkuu.
 
11. Yahusu Kubambiana. Wanawake muache kutugeuzia nyuma zenu hasa kwenye daladala zilizoshona. Mnatupa wanaume nyakati ngumu kumkontroo bwana mkubwa anapoamka in public. Nimemaliza.

Hahahahah kabisa aisee kum-control abdallah kichwa wazi muda mwengine inahitaji moyo aisee, acha kabisa.

Ila wanawake wengine hufanya hivyo kwa makusudi kama vile kurusha ndoano wanajua mwisho wa siku lazma utanasa tu kisha anakuopoa kiulaini kabisa. Inakuwa ni mitego tu ile mkuu.
 
Back
Top Bottom