Nachukia sana umasikini!

Mkuu nafikiri umenielewa tofauti kinyume cha umasikini sio utajiri hata middle income ( kipato cha kati) pia hawapo kwenye level za umasikini, hawapo huko.

Nilienda nchi moja nikakuta Middle income wanaogopa kukaa kukaa na lower income sababu viwangu vya uhalifu kwa low income (90% masikini) ni vikubwa ukilinganisha na middle income.

Iko hivi kule watu wanaoishi maisha ya raha wanaishi kwenye suburbs (makazi ya kistaarabu yaliyopangika na expensive) alafu wanaoishi maisha ya shida wapo kwenye 'HOOD' (kwetu tunaita uswahilini)

So ukienda police utakuta wauza unga, wakabaji, majambazi, wabakaji, wauaji n.k wanatokea Hood (kwetu tuswahilini) wakati huo suburban (suburbs/ maisha bora) wao wanalala hata milango wazi uhalifu uko chini sana.

Nadhani umepata picha ya ninachomaabisha.
 
Unaongelea Slums na Ghettos ? Hoods ni Uswahilini ? Slums zipo hata Kenya au Brazil, hilo sio tatizo la wananchi per se, sababu huko hakuna security, hakuna polisi au hata hao polisi wanashirikiana na waharifu..., Hata wewe ukiwa tofauti ukitaka kutoka kwenye lindi kama hilo waliokuzunguka watakurudisha (Hio ni scenario tofauti kabisa na umasikini na watu wanaweza wakawa masikini lakini wana upendo na wanaishi kwa sheria)

Scenario ya Ghettos na Slums inasababishwa na marginalization ya tabaka fulani, hata ujenge nyumba nzuri kiasi gani watu waishi (flats na maghorofa) kama watu hao hawana opportunity ya ku-maintain maisha hayo (income earning opportunity inayoendana na gharama za sehemu husika) yatageuka kuwa ghettos, na kama hakuna security wauza madawa wata-prey kwa vijana wa sehemu hizo....

Na hata kama kuna ajira kama hakuna makazi utatengeneza slums..., Kwahio ili sehemu ijengeke (community) inahitaji kuzingatia Social, Economical na Environmental Factors..., wewe peke yako kubadilika katika lindi la waliokuzunguka kama umewaacha nyuma usitegemee kama wewe na familia yako mtaishi kwa furaha...

Kwahio issue sio kuhamia kwenye mitaa expensive; kuondoa mzizi wa fitina ni kwa jamii kuhakikisha mitaa inasecurity na inafaa watu kuishi sababu kama wewe na mitaa yako expensive umezungukwa na ghettos unadhani wadau wa Ghettos pesa za kwenda kubwia unga watatoa wapi ?

Sio kwamba sijakuelewa nimekuelewa ila ninakuelewesha ume-blanket upuuzi fulani kwamba ni zao la umasikini kumbe huenda likawa ni zao la marginalization ya baadhi ya watu.....; Black American na maisha yao ya Hood ni zao la marginalization na kubaguliwa / kutengwa na watu weupe..., Mtu anaona hata akisoma vipi ataishia chini au hawezi kupata opportunity kama mtu mweupe, na waliomzunguka ni wauza ngada.., unadhani hao wauza ngada wanauza sababu ni masikini ?!!! Au unadhani ni bahati mbaya kwa America wengi wa weusi wame-exhale kwenye michezo, sanaa n.k. ? (Sababu huko ndio wanaona kuna opportunity kwahio wengi wanajitahidi waende huko) Ni utamaduni ambao unachukua muda kuingia na kuondoka vilevile... Ni kama mbegu ya Chuki na Upuuzi inayopandwa na watawala wa sasa itakuja kuwatafuna vitukuu...
 
ukiwa uswahilini ndo utajua kuna tofauti ya kuwa hai na kuishi,...kule asilimia kubwa ya watu wako hai lakini hawaishi kutokana na umaskini
 
Marginalization ipo lakini kila mtu ana chance ya kuwa vile anavyotaka, masikini hakuumbwa kuwa masikini au kuishi kwenye slums ni matokeo ya namna ya kufikiri na kuamua njia gani ni sahihi kwa kila mmoja wetu kuishi.

Its more of decision making na sio kulaumu watu au serikali, ni issue ya kupambania tonge kwenye sahani.
 
Mtu anieleweshe maana ya neno " Umasikini" kwa maneno yasiyozidi 5.
 
Marginalization ipo lakini kila mtu ana chance ya kuwa vile anavyotaka, masikini hakuumbwa kuwa masikini au kuishi
Aisee !!!!

Kwamba mtumwa angeweza kuwa mfalme ? Unajua mtu mweusi huko Rhodesia kulikuwa na sheria ya kutokuruhusiwa kuuza almasi ? Yaani akiipata lazima ampe mtu mweupe ili auze (that is what we call marginalization); Kwahio ndoto za kwamba kila mtu ana-chance ya kutengeneza his own destiny sio sasa wala sio enzi zile..., ofcourse wale exceptional wanaweza wakavuka ila wale average ambao ndio majority katika kila jamii usipowapa a level playing field wala ku-invest kwao kwa kutengeneza miundombinu inayofaa kwa zile kodi wanazokupa..., Mfano grants za kuwasomesha wanaotaka kusoma mpaka kikomo chao na sio kutegemea wazee wao wauze mashamba ili wapate mkopo ambao mwisho wa siku wakirudi kitaa hakuna hata uwezekano wa kupata ujira....
kwenye slums ni matokeo ya namna ya kufikiri na kuamua njia gani ni sahihi kwa kila mmoja wetu kuishi.

Its more of decision making na sio kulaumu watu au serikali, ni issue ya kupambania tonge kwenye sahani.
Kuishi kwenye slums ? Unajua mfano zile slums za kule Nairobi zilianze vipi ? Nani anacontrol mipango miji ? Kwa ufupi sababu kulikuwa na income earning opportunity karibu bila makazi ya kueleweka watu walijirundika hapo bila kuwa na miundombinu ya kuwa-absorb; unasema ni decision making ? Unataka waende wapi na wangapi ? Mmoja kama wewe ulivyoweza kutoka au wote kwa pamoja ? Na huko wanakohamia kwa pamoja wana-ujira wa kulipia kile ambacho wanahitaji.... au watabadilisha wanakohamia kuwa slums ?

Slums hazina mazingira ya maji safi na maji taka..., unataka hawa wanaoishi kwenye slums ndio waweke miundombinu ya majitaka au mamlaka husika ambazo zinachukua kodi kufanya hivyo ?

Umeongelea madawa ya kulevya je ni kazi ya hawa wananchi wote wahame ili kuwakimbia wauza madawa au ni kazi ya mamlaka husika kuhakikisha madawa hayauzwi sehemu hizo ? Hii ni Journey sio destination na matatizo ya mtu mmoja mmoja yanaweza kuwa solved na individual mwenyewe ila matatizo ya ujumla wao Mamlaka husika inabidi ziweke miundombinu. Na miundombinu hio ni pamoja jamii husika kuwa na Kiu na elimu wanayopata tangia awali inawajengea nini na kuwafundisha nini - Its a Multifaceted problem na mzizi sio umasikini per se bali mentality na utamaduni wa wakati huo - Wewe unaweza ukasema tumeendelea kuliko mababu zetu waliojisaidia kwenye choo cha shimo kumbe huenda sisi ndio tunajisaidia ziwani kwenye vyanzo vya maji tunayokunywa.... Now tell me who is poor us or them ?!!!

Ni kama alivyosema Confucius
“In a country well governed, poverty is something to be ashamed of. In a country badly governed, wealth is something to be ashamed of.”
 
Asante…!!! Its never too late…!!!! Hata kama kma una 40 yrs…!!! Enjoy/ kula bata japo 10yrs to come
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…