Nabii Mwamposa: Watanzania ni wavivu, wanapenda umbea

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
57,913
Reaction score
133,926
Muhubiri wa Kanisa la Arise and Shine International, Boniface Mwamposa amesema Watanzania wanapaswa kubadilisha mtindo wa maisha na kuachana na uvivu unaowafanya kupoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii badala ya kujikita katika maendeleo.

Akihubiri Jumapili kanisani Mwamposa amesema Taifa linakumbwa na changamoto ya Watu wengi kupenda umbea na hadithi badala ya kufanya kazi kwa bidii. “Tanzania ni Taifa pekee ambapo hata Mfanyakazi wa ndani anachukua mshahara kuweka bando ili kufuatilia umbea mitandaoni. Watu wanashangaa kwa nini Wawekezaji hawawaajiri wazawa ni kwa sababu wengi hawana nidhamu ya kazi,” amesema.

Mwamposa ameeleza kuwa Mtu yeyote mwenye maono anatafuta Mfanyakazi anayejituma bila kusimamiwa kila mara lakini Watanzania wengi wanahitaji kufuatiliwa kila wakati ambapo amesema hali hiyo inasababisha baadhi ya Watu kuajiri Wageni kwa sababu wanaona wana nidhamu na ufanisi mkubwa kazini. “Mtu mwenye maono anataka Mfanyakazi anayejituma lakini ukiweka Mtanzania kazini unakuwa mtumwa wa kumfuatilia,” amesema.

Pia ameitaka Serikali kuwekeza kwenye mitandao ya kijamii ya kizalendo inayojenga ufahamu wa Watu badala ya kuharibu. “Mitandao ni zaidi ya bangi, na Tanzania ni miongoni mwa Nchi zinazoongoza kwa matumizi ya mitandao ya kijamii lakini si kwa mambo ya maana bali umbea na uvivu. Tukibaki hivi, barabara tunazojenga zitaendeshwa na Wageni kwa sababu vichwa vya Watanzania vinaharibiwa na mitandao,” amesema Mwamposa
 
Wale kima mama wanashinda kañisani siku zote hawazalishi wapo tu .....kanisani wale tunawaitaje? Pia ubivu wao ndio utajiri wako wanakuletea sadaka kwa magunia....au waumini sio wavivu sababu wanaleta zaka ??
 
Watanzania wangekuwa wavivu Mchungaji asingekuwa anapata sadaka ya kutosha kiasi cha kuishi high life.

Watanzania wanajitahidi kupambana shida iko kwa watawala kushindwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kusurvive na kuishi good life.
 
Na yeye aache kutumia sadaka za waumini kwani anachofanya kwenye ibada ni umbea hizo story za miujiza na ushuuda anapata wapi kama sio umbeya.
 
Watanzania wangekuwa wavivu Mchungaji asingekuwa anapata sadaka ya kutosha kiasi cha kuishi high life.

Watanzania wanajitahidi kupambana shida iko kwa watawala kushindwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kusurvive na kuishi good life.
Not the case, uvivu unachangia hao waumini kupatikana. Why? Hao wavivu wanaamini miujiza kuliko kufanya kazi kwa bidii. Siku watu wakifinguka kwenye hiyo point basi watakuwa wa kuhesabika
 
Back
Top Bottom