Nabii hapati heshima nyumbani kwake

unprejudiced

JF-Expert Member
Jan 27, 2017
3,505
2,862
Ukisoma nakala nyingi sa humu, huwezi kukuta kijana anayejiita mdemokrasia akinadi sera zake kuhusu ni kwa namna gani, yeye au kiongozi wake wanadhihirisha kwa vitendo Demokrasia ya kweli. Ukitaka kujua mtu kapungukiwa hoja, atakuwa anakaa kuzungumzia watu.

Mwisho wa siku hata paka anajiuliza sasa mtu kavua nguo then anatangaza jirani yake kavua, je baada ya watu kutazama anakoonyesha kidole then watarudi kuangalia vile vidole 4. Watakachoona mje mnisimulie.

Siasa haziondoi heshima ya mtu. Baba yako akiwa hana nguo, usidhani wewe ndo utapata heshima. Maisha ni mafupi na tunapaswa kuishi.

Nchi haitajengwa kwa watendaji kuacha kazi ili wapate cha kusema huku kwa kujificha. Mitandao ina muda tu. Hakikisha siku majina yakiwa wazi, basi wewe heshima yako itabaki palepale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom