Nabii Frank Julius Kilawah mnamsoma?!

Nabii Frank Julius Kilawah mnamsoma?!

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
58,042
Reaction score
134,327
Mungu nisaidie kuamini kama kweli umewapa watu wako uwezo wa kufanya mambo makubwa kiasi hiki. Nimeshuhudia semina za Prophet Frank kupitia Chanel 10 na Star TV.

Daah jamaa ana upako wa kutisha,anaponya within a minute.Kina bibi wanatupa magongo within a minute.Kama Yesu karudi vile kinachovutia zaidi ni kutoa historia ya matatizo ya watu katika namna ya kipekee.

Kwamba "wewe ulilogwa na fulani,mahali fulani,kwa sababu fulani". Anatoa mfano wa kukausha kidonda cha mtu ndani ya dakika 3.Jamani mnamsomaje huyu jamaa
 
biblia inasema kuwa " siku za mwisho wengi watakuja kwa jina langu"
 
Ni tapeli tu na hana akili, unamwambiaje mtu fulani ndie aliekuroga,unatengeneza jamii ya namna gani,watu wengine watamchukuliaje yule alietajwa na nabiu kama mchawi, hii haina tofauti na mganga wa kienyeji.

Ramli chonganishi, lakini pia yawezekana anamtaja mtu wala hayupo na na kwa kuwa yule mgonjwa ametajiwa fasta hana mda wa kuuliza, kukubali au kukataa. " YAKO IMEKUPONYA" shika sana imani yako...
 
Huyu jamaa yupo pale Majestik sinema Tanga ambapo ni karibu sana na hospitali ya Bombo. Kwanini asiende Bombo akawaamsha wale wagonjwa ?? au yeye ni mganga anatibu waliorogwa tu.

Hao aliotibu hata mmoja hafamiki. ni watu tu alio arrange nao before tukio.
Kama nabii kweli aje ocean road atibu watu asituibie wake zetu tu maana asilimia kubwa ya waumini wake ni wanawake
 
ukitaka kujua ni wa kweli ama la,yesu mwenyewe alisema zipimeni hizo roho simple like that,hapa sidhani ka utapata majibu sahihi cz kila mtu nae ana mawazo yake juu yake
 
Ananishangaza sana kilawahi afu kila mgonjwa anaeenda kwake anasema alirogwa
 
Hata mimi nimemshuhudia channel ten ila hana tofauti na wengine kama akina Gwajima,Dr Geo Davie nabii mkuu,Kakobe,Mwingira,mzee wa Upako n.k
Imani yako ndio itakuponya na sio kufuata mkumbo
Amini ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu baaasi na anaishi daima nasi,tuwe na imani naye.
Siku hizi hata wachawi wanafanya miujiza hivyo bila kuwa na imani dhabiti hutaweza kumtofautisha nabii wa kweli na nabii wa uwongo.
Omba neema ya Mwenyenzi Mungu ili uweze kuwatofautisha.
 
ukitaka kujua ni wa kweli ama la,yesu mwenyewe alisema zipimeni hizo roho simple like that,hapa sidhani ka utapata majibu sahihi cz kila mtu nae ana mawazo yake juu yake

tupe namna sahihi ya kuzipima maana mbwa mwitu hujifananisha kabisaaa na kondoo.ila km ni msomaji mzuri wa biblia namana hawa jamaa wanaponya na kutoa unabii ni tofauti kabsaa na alivokuwa anaponya yesu.hawa wanatangulixa mbwembweeeee afu ndo wsnaponya wakati yesu alikuwa anaponya tu hqkuna mbwembwe wala kelele
 
Mungu nisaidie kuamini kama kweli umewapa watu wako uwezo wa kufanya mambo makubwa kiasi hiki. Nimeshuhudia semina za Prophet Frank kupitia Chanel 10 na Star TV.Daah jamaa ana upako wa kutisha,anaponya within a minute.Kina bibi wanatupa magongo within a minute.Kama Yesu karudi vile.Kinachovutia zaidi ni kutoa historia ya matatizo ya watu katika namna ya kipekee.Kwamba "wewe ulilogwa na fulani,mahali fulani,kwa sababu fulani". Anatoa mfano wa kukausha kidonda cha mtu ndani ya dakika 3.Jamani mnamsomaje huyu jamaa

hata shetani anajua historia ya maisha ya mtu... manabii wa uongo walitabiriwa toka zamani sana...
nabii wa kweli lazima aenende kwa sheria na ushuhuda..
hawa wengine wamekalia kuwaahidi watu utajiri,kuponywa,mafundisho yao ni yaleyale kila siku... jamani ufalme wa Mungu ni zaidi ya kuponywa magonjwa,ni zaidi ya utajiri. Mtu ukiwa na shida omba mwenyewe na Mungu atakusikia.
 
tupe namna sahihi ya kuzipima maana mbwa mwitu hujifananisha kabisaaa na kondoo.ila km ni msomaji mzuri wa biblia namana hawa jamaa wanaponya na kutoa unabii ni tofauti kabsaa na alivokuwa anaponya yesu.hawa wanatangulixa mbwembweeeee afu ndo wsnaponya wakati yesu alikuwa anaponya tu hqkuna mbwembwe wala kelele
kuna kitu kinaitwa hisia, kuna mwingine akion Mungu anafanya kuptia yeye huweza achili hisia zake pia kwa kupiga kelele n.k Ila njia sahihi ni kukaa karibu na MUNGU na roho wake atakufunulia mengi
 
hata shetani anajua historia ya maisha ya mtu... manabii wa uongo walitabiriwa toka zamani sana...
nabii wa kweli lazima aenende kwa sheria na ushuhuda..
hawa wengine wamekalia kuwaahidi watu utajiri,kuponywa,mafundisho yao ni yaleyale kila siku... jamani ufalme wa Mungu ni zaidi ya kuponywa magonjwa,ni zaidi ya utajiri. Mtu ukiwa na shida omba mwenyewe na Mungu atakusikia.

very true bro
 
kwa mtu asiye soma bible raisi sana kudanganyika soma Matayo 24 utapata majibu walishatabiliwa mapema hao hamna tofauti kati yake na mganga mwingine wa kienyeji Mungu atusaidie wengi wana abudu wasichokijua
 
Ananisikitisha sana anachonganisha hadi ndugu, alimwambia mama mmoja kwenye mkutano mbeya, Eti tatizo linalomsumbua mwanae mume wake ndio kafanya ushirikina loh!!! mama akamwambia mume wangu alishakufa siku nyingi sana, aliona aibu akaanza kujibalaguza eti oohh!! alifanya hivo kabla hajafa, mweee!!! wakati ukiangalia mtoto ana mtindio wa ubongo.
 
Ni tapeli tu na hana akili, unamwambiaje mtu fulani ndie aliekuroga,unatengeneza jamii ya namna gani,watu wengine watamchukuliaje yule alietajwa na nabiu kama mchawi, hii haina tofauti na mganga wa kienyeji.
sawa
 
Back
Top Bottom