Nabii Flora Peter wa Mbezi Beach...

" ongea kwa sauti", ni maneno aliyomwambia muumini wake ili kuwahadaa waliohudhuria.
Sasa hivi kuanzisha kanisa ni sawa na kufungua Hardware, ni kupiga hela kwenda mbele kutoka kwa wajinga.Biblia wanazo lakini wanapotea.
Kwa nini nabii Flora anahamahama? Is she looking for greener pasture?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchungaji wangu atabaki kuwa Gwajima wa ufufuo na uzima, maana hii nisaa ya ufufuo na uzimaaaa wiiiiih.
Hata mumsemeje simwachi sitoki kwake.


SAWA SAWA. NAONA KABAKI.
 
Naomba nifunguliwe na nyie hapa swala la hawa manabii kutumia mafuta ,sijui maji ya upako ni sahihi?.
Na je lipo au lina mofano kibiblia??
 
Watu mnadanganywa na kupigwa pesa kama hamna akili. Yeyote aingie YouTube halafu aandike "Paramahasa Nithyananda~The Third eye." Huyo ni mwalimu wa kiroho huko India anawafundisha watu kuhusu "Jicho la tatu" na kuna kitu kinaitwa "Chakras na Kundalini" hayo masomo yanapatikana huko India wanawafundisha watu kujitambua na kuona mambo yaliyo fichika, na kushinda changamoto za Ulimwengu, ikiwemo kutabiri, kuona mapepo, kuponya magonjwa na mengine mengi. Elimu hiyo sasa hivi imeenea kote ulimwenguni, huku Africa tumelala Sana hatutaki kujifunza Acha tupigwe na makanjanja waliojitambua. Mtu akikutabiria tu eti tayari kawa nabii.
Wajinga ndio waliwao. Hata kuna threads kadhaa humu ziliwahi kuzungumzia kidogo elimu hii. Tafuta thread ya Pascal Mayalla #physic power (uwezo/ nguvu za kutenda miujiza.)
Jambo la kujiuliza, kwanini hawapendani na wakati wote wanahubiri Injili ya Kristo? Mwenye akili na afahamu. Wapi Nabii Elisha alimponda nabii Eliya? Wapi Nabii Yesu alimponda nabii Musa? Sasa tazama hawa Manabii wa sasa wanavyopondana kwenye makanisa yao kupitia mitandao ya kijamii, kila mmoja anamwita mwenzie feki yeye ndio Originally, hapo kama una akili timamu utagundua kuwa hamna kitu ila wanagombania tonge tu. Kama ni kweli wanamtangaza Yesu Kristo kwanini kwenye sticker zao wanaweka picha zao badala ya picha ya Yesu? Anae-promotiwa hapo ni Yesu au yeye mwenyewe? maana picha kwenye sticker anaweka yakwake. Nina mifano mingi tu.
Jamani mambo ni mengi muda ni mchache,,,
Ngoja ninywe chai ntaendelea wakati mwingine.
,,,,,very soon Nitakuja kuwaanika hao Manabii wenu feki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…