Nabii Ellen White: Kubrashi viatu, kunyoa sharubu na kuoga siku ya sabato ni kujitafutia kupishana na Mbingu

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Wanateolojia na wanazuoni:

Imani ya Kikristu haimilikiwi na mtu yeyote.Imani ya Kikritu inalindwa na kuboreshwa kwa mijadala ya kiueweledi.Kanisa katika kipindi chote cha uhai wake, tokea Kanisa la Mwanzo, limepitia katika mijadala mbalimbali ya kitaalimungu. Historia juu ya jambo hili iko wazi.Misimamo ya Mafundisho mengi, juu ya mambo tunayoyafahamu leo, ni zao la mijadala ya hoja zilizo sheheni hoja za kiteolojia, historia na mantiki lukuki.

Pamoja na ukweli huo, Kanisa linaendelea bado kuitafiti imani na hata kwa kutumia njia za kisayansi.Ni kwa jinsi hii ndio maana siku hizi hata matukio yale ambayo huonekana kama yana sura ya kimiujiza au upekee sana huhitaji kuchunguzwa sana mpaka hapo inaonekana dhahiri shayiri kwamba mambo hayo au hali fulani inavuka matokeo ya kiasili au njozi tu za kawaida.

Leo ninalo jambo jingine ambalo linamhusu ndugu yetu mama Ellen White ambaye kuanzia miaka 1800,historia ya Usabato inamchora kama mama mwenye maono makubwa kuwahi kutokea katika Ukristu.Ni mama ambaye anasemwa kupewa maono yapatayo 2000.

Katika mojawapo ya maono hayo ni lile la yeye kuoneshwa jinsi Amri ya Nne ilivyokuwa kubwa kuliko zote:Amri juu ya sabato. Inasadikika kwamba katika maono yake,kuna siku moja alionyeshwa Amri hiyo ikiwa imezingirwa na utukufu kuonyesha jinsi Amri hiyo ilivyokuwa kubwa kati ya Amri zote kumi(10).

Basi, mama Ellen naye katika kuwasitizia waumini wa kisabato na watu wengine wenye maslahi katika kuhitaji kufika Mbinguni,,mnamo mwaka tarehe 25,Mei, 1882, alisema hivi:

"The violation of the fourth commandment is not confined to the preparation of food. Many carelessly put off blacking their boots, and shaving , until after the beginning of the Sabbath.This should not be. If any neglect to do such work on a working day, they should have respect enough for God's holy time to let their beards remain unshaven , their boots rough and brown, until the Sabbath is past. This might help their memory, and make them more careful to do their own work on the six working days." (Signs of the Times, May 25, 1882).

“Panapohusika kuvunja Amri ya Nne ya Mungu haikuishii tu katika kujiandalia vyakula siku hiyo.Watu walio wengi kwa uzembe wanajichelewesha kuburashi viatu au kunyoa ndevu zao kiasi kwamba wanafanya hivyo ikiwa sabato imekwisha kuingia. Kufanya hivyo ni dhambi.Iwapo mtu yeyote anazembea kufanya kazi kama hizo katika siku za kawaida, ikiwa sabato haijawadia,ni vema basi kumpa Mungu heshima anayoistahili kwa siku hiyo takatifu kwa kuachilia ndevu za wahusika zikae hivyo hivyo na hata viatu vyao visalie vikiwa vimepauka hadi kumalizika kwa sabato.Kwa kufanya hivyo, kutasaidia watu kama hao kurejewa na kumbukumbu na hivi kuwa makini zaidi kufanya kazi zao katika siku za kawaida”.(Tafsiri ni yangu).

Kwa maelekezo haya,Ellen White alikuwa anakasirishwa sana na wale ambao walikuwa wanajaribu kucheza na sabato na kucheza na sabato maana yake ni kucheza na Mungu na kucheza na Mungu matokeo yake yako wazi ni kuingia Motoni.

Ellen White, hatunaye leo duniani kusema tumuulize ni kwa nini alifikiria watu kuburashi viatu vyao au kwenda saluni kunyoa ndevu baada ya sabato kuwa imeingia kwamba ilikuwa ni dhambi.Lakini kwa kuwa Ellen aliacha waumini wenzie hapa duniani,wakiwemo Wainjilisti.wachungaji na kile chombo kinachohusika na mafundisho (General Conference),tunawiwa kuuliza yafuatayo:

1.Je, kusafisha viatu.kuchana nywele, kunyoa sharubu, kuset nywele,kuweka wigi na mambo yanayohusiana na usafi wa mwili na mavazi kwa ujumla, ni kuvunja sabato?

2. Je,ikiwa kusafisha viatu na kufanya usafi wa mwili kama kunyoa au kuoga katika siku ya sabato ni kuvunja sabato, mambo hayo bado yanazingatiwa kikamilifu miongoni mwa wasabato wa leo?

3.Je,kama makatazo hayo ya Nabii Ellen White juu ya usafi hayafanyiki au kuzingatiwa vilivyo na wasabato wa leo, wataingia vipi Mbinguni wakati wanaivunja Amri ya Mungu kukicha?

4. Je,kama wasabato hawazingatii jambo la kutofanya usafi siku ya sabato,ni nani amewaruhusu kukaidi jambo hilo la kuvunja sabato? Na je kabla Ellen hajaaga dunia alipata kuondosha katazo hilo?

5. Je,ikiwa kufanya usafi wa mavazi au mwili ni kuvunja sabato,je,maelekezo hayo ya Nabii White yanatanuka hadi kuwazuia wasabato wasioge siku ya sabato na wala kupiga mswaki?

BASI,kwa wale wadau wanaohangaikia kukutana na Mungu kupitia kuziishi Amri,karibuni sana tujadili jambo hili kwa maana kupuuza tunaweza kujikuta tunapishana na uzima wa Milele.
 
Mitale na midimu karibu kipande hii tuyajenge.....,

Asante sana SANCTUS ANACLETUS,nime mtag huyo bwana kwa sababu namuelewa vizuri,ila ana tatizo moja tuu,akija utaliona.
 
nasikia hata kutembea kunakipimo chake pale ulipotupa jiwe likaishia hapo hutakiwi kutembea ukazidi hapo
 
Sijaona shda kwnye maandish yake hayo.sabatho ni ishara kati yetu na MUNGU.ni alama ya utambulishn km MUNGU yupo.km umepewa siku 6 ufanye kazi na 7 ni ya MUNGU umeshndwa nn kufanya maandalio ya sabatho?Mungu ni wa utaratibu.zaburi 33;11
Hivi umemsoma vizuri mwandishi...???
Umesoma na kuielewa hiyo quotation toka kwa EGW...???

Hebu rudia kusoma kisha uje.....,
 
Sijaona shda kwnye maandish yake hayo.sabatho ni ishara kati yetu na MUNGU.ni alama ya utambulishn km MUNGU yupo.km umepewa siku 6 ufanye kazi na 7 ni ya MUNGU umeshndwa nn kufanya maandalio ya sabatho?Mungu ni wa utaratibu.zaburi 33;11

1. Kwa hiyo hamuogi siku ya Sabato kwa maelekezo hayo ya Ellen White?
 
EGW ameacha majanga ulimwenguni lkn leo wafuasi wake hawalitambui na hawataki kutambua,zaidi hupambana na Kanisa Takatifu Katoloki la Mitume.

Ni majanga makubwa sana. Kwa mtu ambaye hajasoma alichokifanya huyu mama unaweza asielewe unachokiongelea. Ni majanga tu. Sisi tutaendelea kuwawekea wahusika.
 
Mitale na midimu karibu kipande hii tuyajenge.....,

Asante sana SANCTUS ANACLETUS,nime mtag huyo bwana kwa sababu namuelewa vizuri,ila ana tatizo moja tuu,akija utaliona.

Mimi mtandao ulikuwa Wa "kumlika na tochi" wakati naanda uzi na hivi nikashindwa kum-tag.
 
Back
Top Bottom