Nabii anakuja, jiandae kumlaki

Nabii anakuja, jiandae kumlaki

Eti kafuga ndevu awe kama Petro.
Au kama Yesu mwenyewe,kaazi kweli kweli.

Lakini maandiko yako wazi kuhusu watu hawa! 1Petro 2:1-3 inasema hivi,"1Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu,kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo,watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza,wakimkana hata Bwana aliyewanunua,wakijiletea uharibifu usiokawia.2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hapo njia ya kweli itatukanwa.3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa;ambao hukumu yao tangu zamani haikawii,wala uvunjifu wao hausinzii." Mathayo 24:24 ni wazi zaidi,inasema,"Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo,nao watatoa ishara kubwa na maajabu;ili wapate kuwapoteza kama yamkini hata walio wateule." Na Bwana Yesu mwenyewe akizunguzia siku za mwisho anasema katika Mathayo 24:11 "Na manabii wengi wa uongo watatokea,na kudanganya wengi." Kwa hiyo tunajua manabii wa uongo watajitokeza katika siku hizi za mwisho.Swali la muhimu ni kwamba,kila mmoja wetu amejiandaaje kuujua uzushi wao?
 
Hata Tito naye ni Nabii
Ila Tito ni nabii wa pombe. Alikuwepo mmoja zamani, sasa amekwishafariki alijiita Mtume wa Pesa. Mwaka 2013 alikuja Kenya nabii toja Nigeria akisema yeye ni nabii wa wanawake. Sioni mfano kwenye maandiko manabii aina hiyo. Leo manabii fake wanawavua watu nguo za ndani, wanachumbia nje ya imani na pia kutaka kuwanunulia zawadi wachumba wao magari ya kifahari ili wawakubali. Wanawanywesha wafuasi dettol, wanawalisha majani na wanapanda juu yao na kuwakanyaga wanapohubiri. Shidaaaah.
 
Tunausubiri ujumbe wake aliotumwa na Mungu
 
Hili neno "Nabii" limekuwa misused sana siku hizi. Kila mchungaji nowdays anajiita nabii.
 
Tuliambiwa kuwa mitume/manabii wa Mungu wa mwisho ni Mtume M.S.W na upande wa pili ni Yesu Kristo. Lakini ukiendelea kusoma biblia maandiko yanasema nyakati za mwisho watu watakuja kwa jina langu naona ndiyo hao mitume na manabii ambao binafsi nawaita fake wamekuwa wengi sana siku za hivi karibuni wakiwa na lengo la kujitajirisha kupitia sadaka zetu(Mnisamehe kwa nitakaye kuwa nimemkwaza).
Mliambiwa na nani
 
Nabii huyo kashushiwa kitabu gani, na wapi kashushiwa hicho kitabu,?? Au ndio anakuja kufilisi waTz, maana vyuma vimekaza mitaani nabii anataka sadaka
 
Tuliambiwa kuwa mitume/manabii wa Mungu wa mwisho ni Mtume M.S.W na upande wa pili ni Yesu Kristo. Lakini ukiendelea kusoma biblia maandiko yanasema nyakati za mwisho watu watakuja kwa jina langu naona ndiyo hao mitume na manabii ambao binafsi nawaita fake wamekuwa wengi sana siku za hivi karibuni wakiwa na lengo la kujitajirisha kupitia sadaka zetu(Mnisamehe kwa nitakaye kuwa nimemkwaza).


cc: Mch. Mwingira, Gwajima, TB Joshua, All Nigerian Pastors, Mama Rwakatare, Kakobe, Mze Wa Upako, etc.
 
Vp sauli Ambaye baadae aliitwa Paulo nae alikua msanii ?
Yule ni mfuasi tu kama walivyokua kina Petro. Kama una maana ya utume siyo unabii basi ni kweli Saul ni mtume ila sina hakika S.W. ni mtume wa nani
 
Umejuaje kama anadanganya Mkuu na akija wa kweli utamjuaje ili uamini ?
Mkuu katika siku hizi za mwisho ni lazima tujiandae kwa kujivika silaha za Mungu,ili tuweze kubaini uzushi wa manabii wa uongo.Katika kitabu cha Waefeso 6:10-18 tunaona silaha hizo, nazo ni kama ifuatavyo:-
1.Kuwa hodari katika Kristo na katika uweza wa nguvu zake.
2.Silaha zingine ni kama ifuatavyo:-
i)Kulijaza neno la Mungu kwa wingi ndani yetu.
ii)Kutenda haki kama neno la Mungu linavyoagiza.
iii)Kumhubiri/kumtangaza Kristo kwa wengine.
iv)Kuliamini neno la Mungu kama lilivyo.
v)Kuupokea wokovu.
vi)Kumpokea Roho Mtakatifu.
Mkuu silaha hizo zikiwemo katika maisha yetu,tutamjua yupi nabii wa uongo na yupi wa kweli,vinginevyo tutayumbishwa kama bendera.
 
Hilo ulilolisema kama mitume wa mwisho ni yesu na mohamed uliambiwa na nani? Kama una reference tupatie mkuu ama siyo huo pia ni uzushi tu
Je wewe kwenye mafundisho ya imani yenu hamkufundishwa juu ya mambo haya??Jaribu kupitia mafundisho yake ulete mrejesho.
 
Tuliambiwa kuwa mitume/manabii wa Mungu wa mwisho ni Mtume M.S.W na upande wa pili ni Yesu Kristo. Lakini ukiendelea kusoma biblia maandiko yanasema nyakati za mwisho watu watakuja kwa jina langu naona ndiyo hao mitume na manabii ambao binafsi nawaita fake wamekuwa wengi sana siku za hivi karibuni wakiwa na lengo la kujitajirisha kupitia sadaka zetu(Mnisamehe kwa nitakaye kuwa nimemkwaza).
Si kweli. Sehemu gani ya Bible inasema Yesu KRISTO ndiyo mtume Na Nabii wa mwisho?
 
Mkuu katika siku hizi za mwisho ni lazima tujiandae kwa kujivika silaha za Mungu,ili tuweze kubaini uzushi wa manabii wa uongo.Katika kitabu cha Waefeso 6:10-18 tunaona silaha hizo, nazo ni kama ifuatavyo:-
1.Kuwa hodari katika Kristo na katika uweza wa nguvu zake.
2.Silaha zingine ni kama ifuatavyo:-
i)Kulijaza neno la Mungu kwa wingi ndani yetu.
ii)Kutenda haki kama neno la Mungu linavyoagiza.
iii)Kumhubiri/kumtangaza Kristo kwa wengine.
iv)Kuliamini neno la Mungu kama lilivyo.
v)Kuupokea wokovu.
vi)Kumpokea Roho Mtakatifu.
Mkuu silaha hizo zikiwemo katika maisha yetu,tutamjua yupi nabii wa uongo na yupi wa kweli,vinginevyo tutayumbishwa kama bendera.
JINSI YA KUWATAMBUA MANABII/WATUMISHI WA UONGO AMBAO YESU NA MITUME WALIONYA—SEHEMU YA NNE

Bwana Yesu asifiwe,

Biblia imeonya sana juu ya ujio wa watumishi wa uongo ambao kusudi lao ni “kudanganya wengi” (Mathayo 24:4,5,24; 1 Timotheo 4:1). Neno linasema imani chanzo chake ni kusikia (Warumi 10:17). Ndio maana Yesu alituonya na kusema “angalieni sana jinsi msikiavyo” (Luka 18:8).

Hivyo unaposikia neno, linakujengea imani ndani yako. Kama siyo neno la Kristo, linakujengea imani ambayo haitokani na Kristo. Na kwa sababu mwenye haki anaishi kwa imani (Warumi 1:17), ni muhimu sana awe na imani ambayo msingi wake ni neno la Kristo.

Yesu alipokuwa anawatuma wale sabini, neno linasema, “Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake” (Luka 10:2).

Hivyo kutokana na maneno ya Yesu, “watenda kazi ni wachache.” Lakini tunajua kabisa katika nyakati hizi, “watenda kazi ni wengi.” Maana yake watumishi ni wengi. Hivyo ni dhahiri kuwa wapo wengi ambao hawakupelekwa na “Bwana wa mavuno.”

Mtume Paulo baada ya kumaliza huduma yake kwa Waefeso, aliwaita wazee wa kanisa na kuwapa maneno ya kuwajenga. Alisema, “Na sasa, tazameni, mimi najua ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko hamtaniona tena” (Matendo 20:25).

Paulo aliendelea kuwaambia, “Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa—mwitu wakati wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao. Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi” (Matendo 20:29—31).

Paulo alizungumza wazi tena kwa machozi kuwa baada yake, watatokea mbwa—mwitu wakali kwa ajili ya kulivuruga kundi. Neno linasema, kwa muda wa miaka mitatu usiku na mchana aliwaonya juu ya hawa mbwa—mwitu. Hii inaonyesha jinsi Mungu anavyotaka tupone ili mbwa—mwitu wasitudanganye na kuhubiri injili nyingine.

Paulo aliwaambia wazi injili aliyowahubiria ni “Ufalme wa Mungu” kwani ndiyo injili ambayo Yesu alihubiri na pia akaagiza ihubiriwe (Luka 4:42—43; Luka 9:1—2; Luka 10:11). Lakini sote tunajua kuwa injili ambayo hatuisikii sana ikihubiriwa ni “injili ya ufalme wa Mungu.”

Pia Paulo aliwaambia Wagalatia kuwa mtu au malaika ambaye atahubiri injili tofauti na alaaniwe (Wagalatia 1:8—9). Yesu mwenyewe alijua kuwa hawa “mbwa—mwitu” watakuja na injili nyingine na siyo kuuhubiri ufalme wa Mungu.

Lakini tupo nyakati za mwisho ambapo yale maneno ya Yesu yatakwenda kutimia: “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, na kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja” (Mathayo 24:14).

Hivyo moja ya njia ambayo itatusaidia kujua kama kuna udanganyifu ni aina ya injili inayohubiriwa. Yesu alitumia miaka mitatu na nusu kuuhubiri ufalme wa Mungu. Pia baada ya kufufuka, kabla ya kupaa mbinguni, Biblia inasema aliwatokea wanafunzi wake kwa siku 40 na kuzungumza nao juu ya ufalme wa Mungu (Matendo 1:2—3).

Injili ya ufalme inatusaidia kuweka tumaini letu katika mambo ya mbinguni, na siyo ya ulimwengu huu. Paulo aliwaandikia Wakolosai kuyatafuta na kuyatafakari yaliyo juu Kristo aliko (Wakolosai 3:1—2).

Hivyo angalia injili inayohubiriwa inakupa kuyatafuta/kuyapenda ya wapi. Kama ukihubiriwa na ukapokea moyo wa “kuyapenda ya ulimwengu,” unajua wazi hiyo ni injili ya udanganyifu na haitokani na Mungu.

Biblia imeweka wazi, “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele” (1 Yohana 2:15—17).

Hivyo kuwa makini na injili ambayo inakufanya uweke hazina duniani. Yesu alisema, “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako” (Mathayo 6:19—21).

Yesu anatukumbusha kuwa tusiweke tumaini katika mambo ya duniani. Anayeingia katika ufalme wa mbinguni ni yule ambaye anayatenda mapenzi ya Mungu pekee (Mathayo 7:21).

Katika Bible Study tuliyokuwa nayo week hii, Mungu alileta somo lenye kichwa kifuatacho:

“JINSI YA KUUONDOA UONGO ULIOPANDWA NDANI YA MOYO WAKO ILI UIPOKEE INJILI YA UFALME WA MUNGU.”

Moja ya kitu nilichosema ni kwamba “ni rahisi kumtoa mtu kutoka katika uongo lakini ni vigumu kutoa uongo ndani ya mtu.” Kwa mfano, kuna mtumishi ambaye ulidhani ni wa Mungu na umekuwa ukimsikiliza na kuamini neno lake (imani chanzo chake ni kusikia) kwa muda wa miaka mitatu.

Halafu baada ya hapo, Roho Mtakatifu akakufunulia kuwa huyo ni muongo na ukatii hiyo sauti na kuacha kumsikiliza tena. Hivyo unakuwa “umetoka kwenye uongo.” Lakini uongo ambao ulipandwa ndani ya moyo wako kwa miaka mitatu na umekujengea “imani fulani.”

Kuutoa huo uongo siyo rahisi na Yesu Kristo pekee ndiye anayeweza kuuondoa. Ukisikia neno la ufalme na kulipokea moyoni mwako utaijua kweli ya Mungu na kuwekwa huru (Yohana 8:32).

UJUMBE AMBAO MUNGU ALINIPATIA MAY 31, 2018

Kwa wale ambao tupo kwenye kundi la maombi kupitia simu, hii ni tarehe ambayo tulikuwa tunaenda kutimiza mwaka mmoja tangu hii huduma ya maombi kwa njia ya simu ianze.

Nashukuru Mungu kuwa kulikuwa na shuhuda nyingi ambazo watu walizitoa kwa kile Mungu alichowafanyia katika maisha yao ya kiroho. Baadhi ya vitu ambavyo watu walimshukuru Mungu ni vifuatavyo:

1. Ongezeko la nguvu ya kuomba. Kuna watu ambao mwanzo walikuwa hawawezi kuomba kwa muda mrefu lakini Mungu amewasaidia na sasa wanaweza kuomba kwa muda mrefu.

Mfano kuna watu ambao kwa kuwa wanaingia kwenye maombi na kujitoa kwa Mungu, sasa wana nguvu ya kuomba hata masaa 12 wakati mwanzo hawakuweza kuomba zaidi ya saa moja.

Kuna siri kubwa sana katika maombi ya muda mrefu. Yesu alikuwa anafanya maombi ya muda mrefu wakati wote. Kabla Yesu hajachaguwa mitume 12, Biblia inasema aliomba usiku mzima (Luka 6:12—13).

2. Vipaumbele kubadilika. Kuna watu walishuhudia kuwa kwa sasa vipaumbele vyao na agenda zao za kuombea zimebadilika kabisa. Kipaumbele chao kimekuwa ni kuutafuta ufalme wa Mungu kwanza (Mathayo 6:33) na kutumia muda mwingine kuomba ufalme wa Mungu uje kwao (Mathayo 6:9).

Na pia kujifunza kuomba “sawasawa na mapenzi ya Mungu” (1 Yohana 5:14—15) na kuongeza kiwango cha maombi kujibiwa. Hivyo zile agenda za kimwili ambazo watu wengi ndizo wanaombea (pamoja na kwamba Biblia imesema tusivisumbukie hivyo), wameziondoa katika vipaumbele vyao.

Kwa sababu hiyo, maisha yao ya kiroho na kumjua Mungu kunazidi kuongezeka. Kumbuka neno la ufalme linatakiwa likupe uhitaji sana wa mambo ya rohoni. “Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa Mungu ni wao” (Mathayo 5:3).

Binafsi siku ya tarehe hiyo (5/31/2018), Mungu aliniletea ujumbe kupitia ndoto kwa ajili yetu sote ili tuweze kusimama imara katika Kristo na neno lake. Usiku huo niliota ndoto mbili na nikaelewa kitu Mungu anasema.

NDOTO #1:

Nilikuwa mahali sipafahamu nikaonyeshwa mayai ya kuku. Huyo kuku alikuwa mweupe na mayai yake muda wa kutotoa ulikuwa bado. Lakini mahali pale mayai yalikuwepo hapakuwa salama na nilihisi kuwa yanaweza kuvunjika.

Hivyo nikiwa ndotoni, nikapata wazo la kuyahamisha na kuyaweka mahali ambapo ni salama. Nilianza kuhamisha mayai mawili na kuyaweka mahali pa usalama. Ndipo nikaona kama kuku mweupe (sikumchunguza vizuri) akija kwenye yale mayai.

Ghafla akafika na “kudonoa” yai moja likavunjika na nikaona ka kifaranga ambako hakajakomaa. Nilishangaa na kujiuliza “kwa nini huyu kuku amefanya hivi?” Nilijua muda wa yale mayai ulikuwa bado na nilijua yule kifaranga atakufa.

Baada ya hapo nikaanza kumtazama na kumuangalia vizuri yule niliyedhani ni “kuku mwenye mayai” ndipo nikagundua siyo kuku bali ni “bata” mweupe na baada ya hapo nikashtuka.

UJUMBE WA NDOTO:

Mungu alikuwa anatuonya juu ya ujio wa wale wanaovaa mavazi ya kondoo walakini ni mbwa—mwitu wakali (Mathayo 7:15) (ila hapa Mungu alitumia kuku na bata ila ujumbe ni ule ule). Nilipoyaweka yale mayai ambapo ni salama, nilidhani anayekuja ni kuku mwenye mayai.

Hii ni sawa na jinsi ambavyo kuna watumishi wanakuja nawe unadhani ni “wachungaji wa kundi.” Ila baada ya kuleta uharibifu, ndipo unafahamu hawakuwa wa kweli. Ndio maana mwanzo yule bata alipokuja, sikumchunguza kwani nilijua tu kuwa atakuwa kuku.

Kitu kingine cha kujifunza ni kwamba mayai yalipokuwa mahali ambapo niliona “siyo salama,” yule bata hakuwepo. Ila baada ya kuyaweka mahali salama ndipo akaja ili kuleta uharibifu.

Hapa tunajifunza kuwa lengo la Shetani kuleta uharibifu kwa watu waliokwisha kutoka kwenye himaya yake. Yaani wale wanaoitafuta kweli ya Mungu ili wawe “mahali salama.”

Kusudi la Shetani ni kuwadanganya yamkini hata walio wateule (Mathayo 24:24). Wateule ni wale “waliotengwa kwa ajili ya kusudi la Mungu.” Ndio maana baada ya mimi “kuyatenga” mayai mawili, ndipo bata akaja kuleta uharibifu.

Hiyo ndoto ina ujumbe zaidi ila Mungu anatuonya sote kujihadhari na watumishi wa uongo wanakuja wamevaa mavazi ya kondoo kumbe kusudi lao ni kuliharibu kundi ambalo Mungu amelitenga kwa ajili ya kusudi lake.

NDOTO #2:

Ndoto hii ilikuwa halisi sana utadhani haikuwa ndoto. Kitu cha ajabu ni kwamba nilipokuwa ndotoni, nilifahamu kuwa “nipo ninaota na kuna ujumbe wa Mungu.” Hivyo ndotoni nilihakikisha ninakumbuka matukio yote.

Ndoto ilikuwa hivi: Niliota naenda airport ili nisafiri ila kwa muda ule sikujua naenda wapi. Nilikuwa na mabegi mawili. Moja dogo la mkononi ambalo huwa nalitumia katika huduma na lingine kubwa kidogo ambalo mtu unaweka vitu kama nguo, viatu na vingine.

Nilikuwa kama mazingira ya huku Marekani kwani nilipoulizwa passport nikasema “nina green card” hivyo nikaruhusiwa. Lakini sikuitoa green card kuionyesha. Baada ya kupita kwenye ukaguzi nikawa naenda mahali ambapo ndege zipo.

Mahali hapo hapakufanana na airport ya kawaida kwani nilitakiwa niende na nipite kwenye geti ambalo ni kama la nyumba (vitu vya ndotoni wakati mwingine vinakuwa tofauti na uhalisia). Njiani nikiwa ninaenda, nikaona mtu ambaye mguu wake wa kushoto unachechemea (ndoto ya kuchechemea mguu ipo kwenye kitabu cha ndoto).

Nilimhurumia hivyo nikasimama na kumuombea akapona hapo hapo. Nilipoenda mbele kidogo, nikawa nimekaa mahali nikaona nina kadi zangu za bank halafu zilikuwa kama zina uchafu.

Hivyo nikawa nazifutafuta vumbi baadae nikaendelea kuelekea ndege ilipo (mpaka sasa sikujua ninasafiri kwenda wapi). Nilipokuwa nakaribia lile geti, nikaanza kuona linafungwa. Hivyo nikaanza kuongeza nguvu ili nifike kabla hawajafunga.

Lakini muda ule nilihisi kuna nguvu ambayo ilikuwa inajaribu kunivuka kwa nyuma hivyo nikawa naenda kwa shida mpaka wakafunga geti. Bahati nzuri ni kwamba wakalifungua tena nami nikaingia.

Kulikua kuna ndege nyingi hivyo nikahitaji kujua naenda wapi ili nijue ndege ya kupanda. Nilichukua simu mfukoni na kuangalia napotakiwa kwenda na nikaona natakiwa kwenda ISRAELI. Baada ya hapo, nikawa naenda ndege ya kwenda Israeli ilipo nikashtuka.

UJUMBE WA NDOTO:

Ndoto hii ina ujumbe muhimu ambao Mungu alikuwa anatupa sote. Kwanza kabisa kipaumbele cha kwanza ndotoni niingie kwenye lile geti kwa ajili ya safari yangu. Kipaumbele cha Mungu kwetu ni tuutafute kwanza ufalme wake na haki yake (Mathayo 6:33).

Nilipokuwa nakaribia getini ndipo niliona geti linafungwa. Kumbuka kuna matukio mawili niliyafanya njiani: kumuombea aliyekuwa anachechemea mguu na kusafisha kadi za bank.

Kumuombea mtu kunasimama badala ya “kazi ya Mungu” na kusafisha kadi za bank kunasimama badala ya mambo ya dunia hii (pesa ndio tunatumia kununua mavazi na vitu vingine).

Kumbuka ndotoni nilikuwa nina mabegi mawili (moja la huduma na lingine la vitu vingine). Unaweza kuona kwa sababu ya “kuombea mtu” na “kusafisha kadi za bank,” kidogo nishindwe kuingia.

Ujumbe Mungu aliokuwa anatupa sote ni kwamba “huduma ya Mungu” na “mambo ya maisha haya” SIYO kipaumbele. Ufalme wa Mungu ndio kipaumbele. Kuna watumishi ambao wanajikuta wanasongwa na mambo ya huduma na wanaacha kuyatenda mapenzi ya Mungu.

Kwenye Biblia kundi la kwanza la watu ambalo walishindwa kuingia katika ufalme wa Mungu ni watumishi ambao wanasongwa na mambo ya huduma lakini hawayafanyi mapenzi ya Mungu.

Yesu alisema, “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitakapowambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu” (Mathayo 7:22—23).

Kundi la pili la watu ambao Biblia inatuambia walishindwa kuingia kwenye ufalme wa Mungu wale wanaosumbuka na mambo ya dunia hii (hasa pesa). Biblia imetoa mifano juu ya matajiri waliotegemea mali kushindwa kuingia katika ufalme wa Mungu (Luka 16:22—23; Mathayo 19:23—24).

Hivyo katika ndoto hii, Mungu alikuwa anatukumbusha kuwa kipaumbele cha kwanza na cha muhimu katika maisha, ni sisi kuupata kwanza ufalme wa Mungu na mengine yafuate. Kufanya kazi ya Mungu ni muhimu lakini ukiona kazi za Mungu zinakuwa muhimu kuliko Mungu mwenye hizo kazi, kuna shida.

Ile nguvu ambayo ilikuwa inajaribu kunizuia ni mpango wa adui kuzuia watu wasiingie katika ufalme wa Mungu.

Neno linasema, “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu” (Luka 16:16).

Katika ndoto hii, Mungu alikuwa anatukumbusha sote kuwa kuutafuta ufalme wake iwe kipaumbele cha kwanza katika maisha yetu.

MUHIMU

Katika nyakati hizi za mwisho, Biblia inasema kuwa watu wengi watafuata roho zidanganyazo. Hivyo ndugu yangu mpendwa, simama katika Kristo. Weka imani yako kwake na muombe Roho Mtakatifu ndiye akuongoze katika kweli yote (Yohana 16:13).

Tupo nyakati ambazo mbwa—mwitu ni wengi sana na kwa macho ya kibinadamu huwezi kuwaona. Ndio maana ni muhimu kusoma sana neno la Mungu na kulielewa ili adui akijaribu kupanda magugu ndani ya moyo wako, uwe na neno na uyaondoe.

Somo litaendelea,…

Jacob & Devota Makaya
Kingdom of Heaven Ministry
 
Huyu jamaa huwa namwelewa sana jinsi anavyojenga mantiki kwenye mafundisho yake. Hata katikati ya jalala lenye uchafu mwingi huwa kunakuwa na vitu vya maana na vyenye thamani.

Hata kama simwamini lakini ni fundi sana wa kujenga hoja!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom