Nabaguliwa kisa dini na kabila


Wasabato na Wakatoliki wapi na wapi? Labda unatafuta tu credits kwa kujiambatanisha. Nyinyi ni Wafarisayo na Yesu alipata shida sana na nyinyi. Kama mliamua kuishi kama Walawi, mbona basi nisione mkitoa sadaka za kuteketeza?

Wakatoliki tunakula Kambale na Kitimoto
 
Samahani kwa maoni yangu..il hamna lolote wewe tafuta mijihela.
I mean struggle and get really loaded....
Haayo ubaguzi maneno tuuu,sema umaskini tuu unasumbua..
Waswahili husema..penye udhia,rupia hutiwa njiani.....
Adios man..!
 
Mimi ni kijana wa kikurya afu msabato sijawahi kukataliwa kwa misingi hiyo japo wanauliza eti nyie wakali majibu hapohapo ina maana nyie wachaga wote ni wezi na majambazi? Inamaana kila mzaramo ni kiruka njia? Huo ni mtazamo uliopitwa na wakati ni kweli kulikuwa na tamaduni mbaya za kukeketa sio wakurya tu hata makabila mengine hapa Tanzania hata nchi nyingine za Afrika kusini bado wanakeketa,kupiga wanawake kumepitwa na wakati siku hizi watu wako bize kimaisha zaidi hayo mambo yalikuwa zamani wakurya tuko civilized bana,je mliosoma huko vyuoni mtakubaliana na mimi kuwa wakurya ni vipanga kwenye masomo wako bright,pia wakurya ni viongozi huko mashuleni na vyuoni? Mkurya hapendi mwenzake aonewe yuko radhi kukupigania hata kama hakujui, wakurya ni mashujaa na wachapa kazi,wapi unamwona mkurya mzembe au goi goi,Mkurya amepigania nchi ya Tanzania wakati wa Mvamizi Idd Amini,acheni kupotosha watu nani alifanya kazi Musoma akabaguliwa? Mbona sisi sio wabaguzi!!Nauliza swali,kila kukicha unasikia matukio ya kikatili kila kona Tanzania hayo yote wanafanya wakurya?
Huyu jamaa aliyeleta huu uzi kasema yeye sio mkurya sasa kwanini analeta madhaifu ya kuachwa na wachumba mkurya hayuko hivyo hata kidogo,sifa ya mkurya ni kwamba mwanamke akimkubalia tu kosa hamwachi hata kama ana shida gani,anadhibiti ndoa vilivyo hususani kitandani mwanamke haoni hata haja yaku-cheat kamapenzi wamekuwa kwa kula vyakula vya asili n.k
 
foolish age... wow!

Shida yako hujitambui, na hiyo ndio sifa kubwa ya FOOLISH AGE. Hebu angalia hii statement yako

sina uhakika kama nitakuja kupenda tena, ni ubaguzi ... ubaguzi tu:shut-mouth:


Haya ni maneno ya watoto. Mwanaume haishi kwa ridhaa ya moyo wa mwanamke. Bado hujakua, unausikilizia uchi kiasi kwamba unaamini huwezi kuishi bila huyo mwanamke. Kinachokuathiri ni upweke-moyo wa kitoto na sio mapenzi.

Ungekuwa umekomaa, usingesikitika kwa ndugu wa huyo mwanamke kukubagua, bali ungeshukuru kuwa umepata fursa ya kuwabaini mapema kabla hujaingia kwenye mahusiano.

Cha pili, utoto wako umeshindwa kukupa nafasi ya kubaini kuwa; mwanamke anayekuwa twisted na mawazo ya familia yake hafai kuwa mke.

Sasa we rukaruka na kejeli ukadhani mi umri wako, mi najua madogo huwa wanawaza nini na ndio maana umeanza kusema eti baada ya miezi sita umezama kwa mchaga, nini hiyo kama sio balehe?
 
e

tatizo sio dini, tatizo ni true love

Dini nayo ni swala la muhimu ili kuzuia maumivi ya baadae kwa sababu ya dini . kumbadili mwenzio kutoka dini yake kuja kwenye dini yako mara nyingi huleta migogoro ya kifamilia na tukumbuke ndoa zinazo tambulika kwa mungu ni za kidini na wala sio za selekari bado kuna umuhimu wa kutafuta mwenza wa dini moja ili kuondoa tafaruku za kifamilia
 
Huo ndo ukweli unaokabiliana nao japo ni mchungu na huwezi kulazimisha iwe kama unavyotaka, unajua maishani kuna mambo mengine yanafanywa magumu sana japo sio magumu. Lakini wewe usikate tamaa na ukitaka KUPENDA KWANZA JUA KWA HAKIKA MSIMAMO wa huyo umpendaye kuhusu masula hayo mawili. Inagawa yeye anaweza asiwe na shida lakini akashawishiwa na ndugu zake kama yule wa kwanza. Lakini uskate tamaa utapata wa kwako tu
 
Na wewe kama unampenda siunahama tu kwani Sabato nini bana.Ila kama humpendi baki hapo ulipo
 

Lakini nyie mmejikita kwenye agano la Kale
 
Pole kaka yangu.
Naomba unitumie private sms then ntakwambia nini cha kufanya.
Thanks.
 

@ mwana!
Hujui ulisemalo nakuombea kwa jina la Yesu ufunguke ujue maandiko kama wasabato! Haya maandiko yako agano la kale?

YESU ALIAMURU PEPO WAWAINGIE NGURUWE, KWELI NGURUWE HAWAFAI!
Mathayo 8:28-32, marko 5:1-20, luke 8:26-39 Walipofika pwani ya nchi ya wagerasi inayoelekea Galilaya alikutana mtu mtu mmoja mwenye pepo hakuvaa nguo siku nyingi na hakukaa nyumbani ila makaburini,alipomwona Yesu alipiga kelele akasema kwa sauti kuu nina nini nawe Yesu,mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese,Yesu akamwuliza jina lako nani? Akasema jina langu Jeshi,wale pepo wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni,wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale nguruwe,basi Yesu akawaamuru pepo wakatoka kwa mtu Yule wakawaingia wale nguruwe,nalo kundi la nguruwe liliteremka gengeni kwa kasi ,wakaingia ziwani wakafa maji.
 

NGURUWE NI NAJISI!
Walawi 11:7 Na nguruwe kwasababu yeye ana kwato,ni mwenye miguu iliyopasuka kati,lakini hacheui,yeye ni najisi kwenu,msile nyama yao wala msiguse mizoga yao hao ni NAJISI KWENU.
Torati 14:8 Na nguruwe kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui huyu ni NAJISI KWENU msile nyama zao wala mizoga yao msiiguse.
Walawi 11:10 Na hao wote wasio na mapezi na magamba waliomo majini ni MACHUKIZO KWENU
Walawi 11:29 kenge mjusi hao ni NAJISI
Walawi 11:13 Kisha ndege hawa watakuwa MACHUKIZO tai,mwewe,kunguru,bundi,korongo.
 

Nakaubaliana nawe kimantiki, lakini kijamii na hasa wazazi wetu na jamii inayotuzunguka inakuwa ngumu kukubaliana na wewe kuanzisha familia na mtu wa dini/kabila nyingine, na hii hupelekea hata ukatengwa na familia japo si moja kwa moja.

Nadhani inabidi kulinganisha jamii yako ilivyo na kuona madhara yanayoweza kukupata (kutengwa) kutokana na mitazamo yao, ikiwa wana mitazamo chanya dhidi ya dini/kabila tofauti bas sawa. Kila siku katika maisha mtu hawezi hata kukuwazia ww kuwa rafiki yake kwa kuwa tu mnatoka dini tofauti.
 
Lakini nyie mmejikita kwenye agano la Kale

Taja ni sehemu gani tumejikita katika agano la kale ili nikupe fungu linapoana kwenye agano jipya,narudia Yesu hakuja kutangua torati bali kuitimiliza soma hapa chini uone Yesu ananena kwenye agano jipya maneno yaliyosikika agano la kale.

Mathayo 5:21,Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa,Usiue na mtu akiua itampasa hukumu
Mathayo 5:27,mmesikia kwamba imenenwa usizini,lakini mimi naawmbia kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Hizo baadhi ya amri kumi kutoka agano la kale,kwa hiyo unamaanisha tuvunje amri kumi kisa ziko agano la kale?
 
Pole sana mkuu, time will heal machungu yako
 
Ha ha ahaa haa mkuu umenifurahisha sana nyama wanakula ila sio zote hasa hasa yule mnaomwita noah .ni najisi!!
 
...kaka likuepukalo lina kheri na wewe...kuwa na subira, Inshaallah Mungu atakujaalia mke aliyepanga yeye na wepesi utatawala katika mambo yenu. Usiwe na wasiwasi.
 
Pole sana ndugu yangu ndo yale ninayosemaga kila siku mwanaume msomi wako ni yule asiesoma,kama killa aliesoma ataoa alyesoma mwenzake sasa wasiosoma wataolewa na nani?? wachana nao hao waliosoma oa haraka asiesoma wala hataangalia upuuzi huo,na hakika watakukumbuka milele mana hakuna atakae waoa wala hawatampata yule mwenye sifa wanazozitaka wao,kumpata mwanaume wa kuoa siku hizi ni kazi maisha magumu subiri kidgo tu watakukumbuka sana wakina wanakaribia kuzeeka na hakuna aliehata chumbia.
 
acha kuficha ukweli na unafiki...mimi mwenyewe ni mjaluo tena mkatoliki katika familia yetu kunawasabato wengi sana ila nataka niihakikishie jf wasabato ni wasumbufu sana na wabaguzi tena wakishajua wewe ni mvaticani watatumia hiyo nafasi kukudhoofisha na kukudhihaki....nawaunga mkono hao madada coz najua huyo jamaa kwa usabato wake alikuwa anawadhihaki ndio maana imekuwa raisi kwao kukimbia..nawajua kwasababu ni ndugu zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…