Nabaguliwa kisa dini na kabila

Aisee umesahau wasabato ni marufuku kula kiti moto na pombe aisee,lakini pasaka wanafanya siku tofauti na wakristo wengine wanaita meza ya bwana ndo pasaka yao. kuhusu krismas hakuna maandiko kwenye Biblia yanayosema kuhusu krismas au ya kuwa krismas ni tarehe 25/Desemba,mimi nina rafiki msabato kinachonifurahisha wasabato ni kama wanazuoni wanabisha kwa kujenga hoja,kwa facts wanasoma Biblia vilivyo ukibisha unapewa kifungu.
 
Mkuu kuna rule of engagement inayosema, If you can't beat them, join them.
Hao wanawake wamekuwa fair sana kwako kwa kukueleza sababu zao katika mapenzi cha kushangaza wewe hujawa fair kwao kwa kutokuwaeleza kwa nini usifanye wanachotaka ukifanye badala yake unalalamika tu.
Hivi umeishajiuliza kwa nini kabila na dini yako inakuwa ni tatizo kwao. Inawezekana tatizo unalo wewe badala ya wao.
OPEN YOUR EYES na ujipime kwanza kama kweli unataka mapenzi na wao
 
Aisee umesahau wasabato ni marufuku kula kiti moto na pombe aisee,lakini pasaka wanafanya siku tofauti na wakristo wengine wanaita meza ya bwana ndo pasaka yao. kuhusu krismas hakuna maandiko kwenye Biblia yanayosema kuhusu krismas au ya kuwa krismas ni tarehe 25/Desemba,mimi nina rafiki msabato kinachonifurahisha wasabato ni kama wanazuoni wanabisha kwa kujenga hoja,kwa facts wanasoma Biblia vilivyo ukibisha unapewa kifungu.
 

hata wewe ni mdini pia, kwanini umlazimishe mwenzako kuwa sabato masalia angali wewe hutaki kuwa Mkatoliki? acha udini kama unataka kuoa binti wa kabila na imani nyingine kubalianeni lakini kila mtu abaki na imani yake kama wewe hutaki kubadili dini yako na yeye anataka kubaki na imani yake pia.
 
I think its a time for u-sabato kupitiwa upya..coz unaonekana kama ni dini au imani ya dunia nyingineeeee...enzi zile za zinjatrophus au kina homo-habilis sapiens. Kama dini/iman inakataza kunywa soda..nina waswasi na hizi blackberry, i-pads, i-phones etc...na sikuhizi zimekuja tena galaxy, mara nokia lumia....bado mi-face book, twirraaaaaa, whtsup etc.

Hii dini yako kaka ipo ki-kale sana kwa mwanamke wa 21st century kukubali kuolewa nawe....kama vip bora hata uwe mlokole wa kwa kakobe au ma arwakatare....coz mwisho wa siku ishu ni kwenda mbinguni kupitia njia ya yesu kristo.

Kuhusu suala la ukuryaaa a.k.a u-musoma, ni suala la kukubaliana na mpenzi wako na ikiwezekana anunue dol kubwaa linalofanana naye ili siku ukitaka kumtandika migumi unapiga hilo doll lake hasira zako zinatulia...and for curiosity...

Mbona ugomvi wenu wa huko tarime wa mapanga na mingumi mkija dar munauacha hukohuko?...sijawahi kusikia mkurya kumpiga mzaramo au hata msukuma.
 
Hata nami siwezi olewa na msabato; na ukizingatia mapenzi ya siku hizi unajifunza kumpenda mtu, so kigezo cha compatibility kwenye Imani ni muhimu. And for you guys huwa mnatuona wakatoliki ni waovu kuliko shetani mwenyewe; kiasi kwamba vita yenu na ukatoliki ingehamia kwa shetani, mbigu ingekuwa yenu.

Ushauri wangu, tafuta mchumba kanisani kwenu. Issue ya kupigwa hakuna mdada anavumilia hivyo jua the moment unalift Mkono kumpiga mtu ni sawa na kumpa talaka plus jela.
 
Daaa kuwa msabato gafla inabidi ujipange lolz!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
bora umekuwa muwazi.

Kwa freelanders ni ngumu kwa kweli.

 

Na jamaa zangu 12 wanatokea wote Msoma na wote wa wasabato
 

Mh. Mimi ni msabato ila nnachoweza kusema ni kwamba watu wanakuza na kupotosha mambo mengi.
.. wasabato wanakunywa soda aina zote, iwe cocacola, fanta au sprite/pespi.
.. kweli baadhi ya samaki watu hawali ila kama mmekutana na mtu, mnapendana, hiyo si issue kabisa.
.. most SDAs wanakunywa chai na kahawa sana tu, kuna mafundisho ynatolewa kuwa chai, kahawa, hizo soda zina side effect ila we are not forced to stop drinking, it's one's choice.
.. ni kweli kuanzia ijumaa tunapumzika na kupumzisha mwili na akili, for me hili ni jambo zuri as in, kama nimefanya kazi kweli for six days, i have the reason to relax, hata hivyo labda niseme kuwa kwa maisha ya mjini na ajira za sjku hizi, wasabato wengi wanashindwa, including myself, huko vijijijini kwetu kweli hayoyanafanyika.
.. mambo ya youth organisations yapo madhehebumengi, kwa hiyo pathfinders, adventist youth na mengineyo sidhani kama yanamfanya mtu asipende kuishi na msabato.
.. kutengeneza nywele, nakuomba angalau uje kanisani siku moja uone jinsi gani wanawake wanavyojiremba, it's natural that a woman must look pretty, and our women aren't exceptional. Wanajiremba, wanatengeneza nywele, japo hawatogi masikio.
 

Dada Kaunga, wasabato hawana itikadi yoyote mbaya, ni imani tu iliyojengeka kwenu kwamba dini yetu ya kizamani, haiko compatible na madhehebu mengine, we see u catholics like any other, we respect u but differ in the way we understand bible, biblia ni very complicated kitabu, everyone has his own way of understanding it.

Jaribu msabato and u will never regret.
 

Kwanini wewe umekuwa mbaguzi kwa watu wa musoma na wasabato kiasi hicho?. Yaani mpaka unasema hutopenda tena kisa hao marafiki wa wili waliokukataa?. Wewe ndo mbaguzi mkubwa, tena mkubwa zaid ya hao mabinti!. Usiwatenge wasabato wenzio, sifa waliyopewa ni yao. Usiwatenge wa musoma wenzio.hukutaka kubadili dini basi tafta msabato. Umeambiwa watu wa musoma wababe basi uwe mnyenyekevu au pendekeza mu msoma mwenzio
 
sikitiko sikitiko penzi na dini hakika havipingani
bora kupishana elimu ila si imani ya dini
sishauri msababto kuoa msabato ila moyoni amani inaleta
 
Sijaona ubaya hao wapenzi wako kukwambia ukweli, kwanza wameelezea vikwazo vya penzi kati yako na wenyewe.

Ukweli ni uhuru.

Endelea kuwalaumu maana hata wewe hujaamua kuyapatia tiba matatizo yako,tafuta msabato pia mkurya yanini shida'
Kwani Wakurya wanatoka Musoma? wacha kuropoka.
 
Pole sana kaka yangu.
Ni changamoto ambazo wengi tunazipitia siku hata siku but kumbuka MKE MWEMA MTU HUPEWA NA MUNGU. Naamini unalifahamu hilo, so be patient kaka yangu.
 

Tatizo ninaloliona kwako ni kuwa bado hujakuwa na uzoefu wala ujuzi (experience) wa kutosha wa kuanzia kutongoza mpaka ya kudili na wanawake bado. Moja ya sifa za mwanaume mwenye uzoefu ni kuweza ku take control ya relationship yako.
Bahati mbaya zaidi ni kuwa aina ya wasichana unaokutana nao ni wasichana wajanja (au unaweza waita watoto wa mjini) ambao mara moja wanakuwa wamekusoma udhaifu wako. Wewe Kaa chini ujiulize kwa makini sana kumbe kabila lako na dini yako ni tatizo (vitu ambavyo naamini unawafahamisha mara tu baada ya kuanza mahusiano yenu na si mwishoπŸ™‚.
Sasa jiulize hivi; Wao huwa wanangoja na kufurahia nini na wewe siku zooote hizo mpaka pale inapofikia Mzee mzima unapomwaga ajenda ya kuchukua mzigo jumla jumla ndio wao wanakuwa wanaanza kupangua majeshiπŸ™‚. Hapa naweza kuamini tu kuwa labda kinachowaweka ni kuwa unahonga sana tu maana hizo ndio sifa za watu wa MusomaπŸ™‚. Hivyo kwa muktasari tu ni kwamba umekuwa zile aina ya relationship ambazo wamarekani wanaita FWB - yaani Friendship with Benefit (au ita mambo ya FezwaπŸ™‚ huku wewe binafsi ukiamini kuwa ni "mapenzi". Na ndio maana pale unapotaka kuchange gia na wao wanachange gia kupitia sababu dhaifu kwa mtu ambaye tayari wanamjua ni dhaifu na kuishilia mbali.

Hivyo ni sawa mwanaume uko kwenye relationship na mwanamke anayekuhonga mahela au zawadi kedekedei au una enjoy tu sex yake (wanaume tunasema umepata mahala pa kuponeaπŸ™‚ lakini ili hali moyoni mwako humpendi kabisa kuwa mpenzi wake wala kuwa mke wako hata kwa dakika tatuπŸ™‚. Halafu mwisho wa siku awe king'ang'anizi wa kudai ndoa na wewe si utamtemela mbali huko aishieπŸ™‚. kwa hiyo ndiyo kesi yako bwana.

Lakini bado kijana mdogo take your time kuwafahamu vema wasichana unaokutana nao. Uliza maswali magumu toka mwanzoni kabisa kuwa (What are they looking for in terms of relationship) naamini bado wapo wasichana waaminifu ambao wako tayari wala hawana vya kuchezeana akili na kutoa visingizio vya kuhuni.

Mwisho kwa taarifa yako tu ni kwamba mimi leo hata nikiingia mahala kama Zanzibar au Pemba bado ninaopoa mpenzi japo dini yangu wala kabila langu wala lafidhi yangu havifanani kabisa na watu wa pande za huko kabisa. Lakini ndio mwanaume lazima uwe mjanja na mwenye kujiamni na kuweza kutake a control of your relationshipπŸ™‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…