Bernard bakari
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 407
- 781
Napenda nichukue Fursa hii kutoa yangu ya moyoni kuwa katika uamuz wangu wa kutompa mheshimiwa magufuli kura yangu sijutii na wala sitojutia kwa hichi ninachokiona ndani ya serikali anayoiongoza.
Serikali hii ya awamu ya tano imejaa chuki, kisasi, Uonevu, Dhuluma, Uminyaji wa demokrasia na mambo mengine kadha wa kadha.
Tanga alifukuzwa mtu siku ya pili baada ya kutishia watu na bastola, kwa awamu hii ya tano tunasema alitumbuliwa leo hii mkuu wa mkoa wa Dsm anavamia kituo cha habari na mitutu sita anapongezwa ni ukosefu wa maadili pamoja na upendeleo wa hali ya juu.
Rais anaongea kwa kujinasibu kuwa alienda kuchukua fomu mwenyewe na alishinda mwenyewe amesahau kabisa wapiga kura waliosota kwenye jua kusubiri zamu yao ya kupiga kura.
Rais anadharau habari ya kwenye mitandao amesahau waziri wake Ndalichako alichukua hatua juu wa wanafunzi wanye kusomea shahada ya elimu kutoka chuo cha mkwawa na DUCE walipompiga vibaya mwanafunzi wa sekondari kule mbeya, baada ya kuona matukio kwenye mitandao ya kijamii leo habari hizi za mitandao ya kijamii zinaitwa udaku.
Wakati nakua nilisikia kuna makabila hayafai kupewa urais kabila mojawapo nililolisikia likitajwa ni pamoja na wasukuma ni mambo ya utani lakini najiuliza au walikuwa wanaogopa mambo kama haya au yalitabiliwa na wazee wa kale
Mwisho napenda nimshukuru mungu kwa kuniongoza na kunipa maarifa ya kutokuwa mmoja wao wa wale waliochagua Rais mwenye roho mbaya,Roho ya kisasi mwenye ubaguzi wa hali ya juu, mwenye kujua kila kitu baya na mema, uchumi kasoma yeye, Sheria anaijua yeye, mkandarasi yeye, mwana diplomasia yeye, Roho hii ya ubaguzi nawaambia Tanzania haitatuacha bure, machozi ya wale wanaonewa hayataenda bure mungu atatenda miujiza mungu awape baraka na matumaini kwa wale wote waliotumbuliwa kutokana na chuki binafsi, kisasi, ukabila na ubaguzi wa aina yeyote. MUNGU IBARIKI TANZANIA